Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Mwanamke tajiri hana roho ya kimaskini, kinachosumbuwa hapo ni umaskini wa roho tu.

Kumbe hata wanawake huwa wanatangulia kufa pia na kumuacha mume na Watoto.
Inafikirisha sana , ila tutafika tumechoka sana
 
Mapenzi ya mbali kwa dalili hizo inaonyesha kabisa kuna jamaa anamkaza, ukiandika jina lake ndio mwanzo wa kukuchinjia baalini, wewe fanya hivi hapo hakuna ndoa hapo ni kuliana tyming, endeleza kwako wekeza kwa siri, anza kujiandaa kufukuzwa hapo na kuachwa..
 
Acha kiherehere na ubabe, kiwanja cha mkeo wewe ulitumwa nini kwenda kukijenga? Ulifanya hivo ili baadae uje upate auheni ya kwamba una viwanja viwili vyote ni mali yako kwamba uviandike jina lako kisa tu wewe ni baba wa familia? Muachie mama wa watu kiwanja chake aandike jina lake anavyotaka maana hiyo ni mali yake aliitafuta kwa jasho lake. Wewe si unakiwanja chako kwanini usikinjenge kile? Au unampango wa kumuacha?? UNA UBINAFSI WA VIWANGO VYA PHD mkuu
 
Kuburi gani? Wewe sema tu unataka kumkwapua mama wa watu mali yake kupitia neno “ana kiburi”
 
Si ndiyo hapo sasa🤝
Kiwanja Acha aandike jina lake,kutaka au kulazimisha na jina lako liwepo si u gentleman ukizingatia alinnunua kiwanja yeye. Kujenga ktk kiwanja chake iwe kama umempa zawadi na isiwe sababu ya wewe kujimilikisha kisa vyumba viwili ulivyosimamisha
 
Muitie Polisi chap
 
Mwenyewe nimewaza. Huenda mwanaume ana michepuko huko anakoendaga kukaa mwezi, Kwahiyo mama wa watu kasanuka. Isitoshe hata kama huyo mama aliongea maneno mabaya kwamba “najuta kuolewa na wewe”…….. hayo maneno yana maana sana, mtu hawezi tu kuongea ghafla bila kuwepo na mazingira yanayoendana na hayo maneno. PERIOD
 
1. Kwa kuwa, umekiri kwamba ninyi ni wanandoa (mmefunga ndoa), na,
2. Kwa kuwa, umekiri pia kwamba mna watoto wenu wa wawili ambao wamezaliwa ndani ya ndoa.
Hivyo Basi, suluhisho sahihi zaidi kuhusiana na hili suala lako ni:-
(I) AIDHA, Ardhi hiyo mnapaswa kuimiliki kwa pamoja nyinyi wote wawili kwa umiliki wa pamoja (Joint Occupation or by means of Occupation in Common.
(a) Mmiliki Ardhi hiyo wote kwa pamoja kwa umiliki wenye maslahi yasiyogawanyika, yaani Joint Tenants (Matrimonial Property).
Majina yenu wote wawili (jina lako na la huyo mwanamke) yawepo kwenye Hati ya Umiliki wa Ardhi, hii itaondoa utata na wasiwasi wa kudhulumiana hiyo Ardhi.
(b) Mmiliki Ardhi hiyo wote kwa pamoja kwa Hisa, yaani Common Occupiers in Shares. Mnaweza mkagawana Hisa za umiliki wa hiyo Ardhi, kila Mwanandoa anaweza akamiliki Ardhi hiyo kwa Hisa ya 50% au vinginevyo kwa kadiri mtakavyokubaliana ninyi wenyewe kwa hiyari yenu.

( ii) AU, Wote wawili, yaani wewe na mkeo mnaweza mkajitoa kwenye suala la Umiliki wa hiyo Ardhi, badala yake Ardhi hiyo muimilikishe kwa Watoto wenu na nyinyi mkabaki kuwa wasimamizi tu wa Ardhi husika (Guardianship) hadi hapo watoto wenu watakapofikia umri wa utu uzima wa miaka 18 au zaidi.

NB: Nimeshauri kulingana na uzoefu wangu binafsi wa kimataifa, yawezekana pengine ushauri wangu unakinzana na matakwa ya Sheria za Tanzania, Sina uhakika kuhusu suala hili lakini.
Lakini sehemu nyingi Sana ambazo nimewahi kuzuru, ushauri Kama huu umesaidia Sana katika kutatua Migogoro Kama huu wa kwako.
Naomba kuwasilisha.
I stand to be corrected!
 
Muandikishe tu kwaajili ya watoto,mbona hakuna shida sema hapo kwa kiburi ndio tabu
Fanya tu umemjengea na wanae huna hasara
 
A man who show affection is not a real man. Pesa nitafute mm afu nikuandike wewe awapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…