Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Habari wadau wa jukwaa hili pendwa,

Naomba nienda moja kwa moja kwenye mada.

Mimi nimeoa na Mungu amenijalia watoto wawili. Nafanya kazi sekta binafsi na mke wangu sasa ni mama wa nyumbani. Mke wangu kabla sijamuoa alikuwa amenunua kiwanja chake makao makuu ya wilaya na mimi pia nilikuwa nimenunua kiwanja changu katika wilaya hiyo hiyo ila kwenye tarafa mojawapo.

Tulipooana tuliamua kuishi wilayani, kipindi hicho mimi nilikuwa sina kazi ila yeye alikuwa na kazi japo si mshahara mkubwa na alikuwa kwenye kata mojawapo katika wilaya hiyo nami nilikuwa nimepanga makao makuu ya wilaya, ambapo yeye ndiyo alinunua kiwanja.

Mwaka mmoja baada ya ndoa nikaajiriwa mkoa mwingine hivyo nikamuacha yeye na mtoto, yeye akiwa bado anafanya kazi.
Nikaanza kujenga msingi kwenye kiwanja changu na sikuendeleza nikaachia kwenye msingi. Baadaye nikapiga msingi kwenye kiwanja chake.

Mwaka moja baadaye yeye akaachishwa kazi pale alipokuwa anafanya kazi, ikabidi niwachukue nikae nao mjini. Lakini nikaona ni gharama sana kupanga mjini na mshahara ni mdogo, nikaamua kuchukua mkono nikaendeleza msingi katika kiwanja chake kwa maamuzi kwamba, niendeleze hata vyumba kadhaa halafu niirudishe familia wilaya wakakae huko, mimi nichukue chumba kimoja kupunguza gharama.

Hili pia lilichangia na mgogoro, nikaona siku moja nitapoteza kazi halafu sina pakukimbilia wakati natafuta kazi nyingine. Nikaanza ujenzi na taratibu zote halmashauri nilifanya kwa jina langu. Nikajenga vyumba viwili nikaweka na umeme nikahamisha familia. Kwa sasa wana miezi kadhaa nakuwa nawatembelea walau kila mwisho wa mwezi.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kwamba mke analeta jeuri kwenye hiyo nyumba, kwa kiasi fulani amebadilika, maana juzi kati tulitofautiana jambo fulani dogo nikagundua kiburi kimempanda sana.

Pili, sasa hivi anapambana hati iwe kwa jina lake. Kwa sasa tuna harakati za kuweka maji anajitahidi ajaze fomu yeye kwa jina lake na pia juzi nililipia hela B con na imewekwa sasa yeye anataka kujiandika kama mwenye nyumba.

Ebu naomba ushauri wenu nimuache ajiandike? Nia yangu mimi ni kulinda ndoa yetu, maana naona yeye kama akipata umiliki atanisumbua na tutasababisha mgogoro utakao wasumbua watoto wetu.

Ebu naombeni ushauri kulingana na uelewa na uzoefu, maana mimi kama baba mwenye nyumba ni wajibu wangu kulinda familia yangu, wakina mama wanadanganyika haraka sana. Natarajia kumpiga marufuku harakati zote kwa mamlaka niliyonayo ila nasubiri ushauri wenu.

Asanteni.
Bwana Mbuzi ipo hivi.
Kiwanja yes ulinunua na haukujenga. Hivyo ujenzi umeufanya ukiwa ndani ya ndoa.

Bila kwenda mbali sana, unawajibika kumuongeza mke kwenye umiliki wa hiyo nyumba.

Wengi watakushauri kulingana na hisia zao na siyo facts
 
Muache aandike,acha roho ya kimaskini. Kwani akiandika tatizo lipolyse wapi ?Atazikwa nacho in case akitangulia kufa ?
 
Bwana Mbuzi ipo hivi.
Kiwanja yes ulinunua na haukujenga. Hivyo ujenzi umeufanya ukiwa ndani ya ndoa.

Bila kwenda mbali sana, unawajibika kumuongeza mke kwenye umiliki wa hiyo nyumba.

Wengi watakushauri kulingana na hisia zao na siyo facts
Kiwanja ni chake alinunua yeye kabla sijamuoa nami nonacho changu ila first priority kwa ajili ya kukaa familia na watoto kuweza kwenda shule ni kiwanja chake ndio maana nikaanza kukiendeleza chake japo hata changu nimepiga msingi. Tatizo ni yeye alivyoaanza kubadilika baada ya kuhamia na sasa ananyemelea umiliki. Sina tatizo kama umiliki ukiwa wake lakini akabaki na tabia yake ya awali lakini kwa dalili alizoonesha ndoa itakuwa mashakani
 
Kiwanja Acha aandike jina lake,kutaka au kulazimisha na jina lako liwepo si u gentleman ukizingatia alinnunua kiwanja yeye. Kujenga ktk kiwanja chake iwe kama umempa zawadi na isiwe sababu ya wewe kujimilikisha kisa vyumba viwili ulivyosimamisha
 
Huwezi kumwachia tu. Yaani mwachie tu afanye anavyotaka.

Ana akili za kimaskini sana.
 
Mimi alitaka tuandike majina yetu wote wawili kwenye hati. Nikafanya mpango likasndikwa jina lake tu.

Najua hata ikitokea mgogoro wanangu watakua mikono salama. Ikitokea nimetangulia mbele za haki kabla yake, hawatapata msukosuko kutoka Kwa ndugu zangu.

Mie naweza kuanza maisha popote nikaishi hata kwenye Banda, kama wanangu wako salama inatosha.

Pia ni fikra pitiful sana kuanza kuhangaika na umiliki wa Mali mnapikya kwenye ndoa, changamoto zipo kwenye ndoa zote, kujikuta sana kwenye nani anamiliki kipi kati yenu ni dalili ya mahusiano hafifu au ukosefu wa afya ya ndoa. Ni kama vile mnaishi Kwa kutegeana na wakati wowote mnaweza kutengana.
 
Kiwanja ni chake alinunua yeye kabla sijamuoa nami nonacho changu ila first priority kwa ajili ya kukaa familia na watoto kuweza kwenda shule ni kiwanja chake ndio maana nikaanza kukiendeleza chake japo hata changu nimepiga msingi. Tatizo ni yeye alivyoaanza kubadilika baada ya kuhamia na sasa ananyemelea umiliki. Sina tatizo kama umiliki ukiwa wake lakini akabaki na tabia yake ya awali lakini kwa dalili alizoonesha ndoa itakuwa mashakani
Niwie radhi kwa kutokusoma kwa makini post yako

Ni kwamba, umiliki wa nyumba ni wenu wawili na hili anzia ustawi wa jamii ngazi ya Tarafa ili kuweka kumbukumbu vyema na wana utaratibu wa kuwaelewesha wanandoa mambo haya.

Pia kumbuka hiyo nyumba imejengwa after marriage kila mali inayopatikana ni mali ya wote equally....

Unaweza kumtafuta mwanasheria akakushauri vyema kuhusu hili
 
Nakuongezea jambo.Kitu cha mke hubaki kuwa cha mke daima.Na cha mume huwa cha familia.Usipoelewa nakuchapa makofi bwana mbuzi.
Hahaha! Nipo tayari kuchapwa makofi kama nina kosa. Ninachong'ang'ania hapa Mimi sio umiliki bali ni madhara ya ndoa yetu baada ya umiliki wake maana kuna hali ambayo Mimi sinaandika humu baada ya kuihamishia familia pale kwenye hiyo nyumba ambayo kuna vitu nisipo virekebisha mapema vikikomaa vitakuwa na madhara makubwa kwenye mahusiano yetu ya ndoa na itaathiri ustawi wa watoto wetu kitu ambacho Mimi sitaki kitokee nikiwa hai nahitaji watoto wangu wakue katika maadili mema na niwape mahitaji yao kadiri ninavyojaliwa na Mungu
 
Mkuu tumia akili ili umfilisi biashara yake ili heshima irudi ndani ya nyumba, wanawake waki Afrika wakipata pesa wanaweuka.
Kumfilisi sitaki maana maisha haya huyajui nataka ajue biashara asiwe tegemezi maana huwezi jua nani anatangulia.
 
Niwie radhi kwa kutokusoma kwa makini post yako

Ni kwamba, umiliki wa nyumba ni wenu wawili na hili anzia ustawi wa jamii ngazi ya Tarafa ili kuweka kumbukumbu vyema na wana utaratibu wa kuwaelewesha wanandoa mambo haya.

Pia kumbuka hiyo nyumba imejengwa after marriage kila mali inayopatikana ni mali ya wote equally....

Unaweza kumtafuta mwanasheria akakushauri vyema kuhusu hili
Asante mkuu you are gentleman!!
 
Wanawake wengi siku hizi wamekua hawana hisia za mapenzi ya kweli (real love from within), hii hupelekea kutoishi katika ile misingi halisi ya ndoa na kuheshimu mamlaka ya baba kua kichwa cha familia na msimamizi wa mali.

Wamekua na mapenzi ya kuigiza hasa hawa tunaowaoa wakiwa wameshavuka 25+ maana wanakua tayari wana past experiences zao nyingi na ma-ex zinawafanya wawe na mixed feelings.

Kwa kifupi ktk kipindi cha uchumba wana uwezo mkubwa sana wa kuficha makucha yao hasa wakiona kuna fursa huko mbele. Watajitahidi kukuonyesha upendo wa hali ya juu ili mradi ujichanganye utangaze ndoa.

Kimbembe kinaanza mkishakua ktk ndoa focus yao kubwa huanza kua kwenye mali na watoto tu (ambao anaweza akawa amekubambikia pia). Wengi wanaamini wanaume hua tunakufa mapema, hivyo mali zikiwa kwa jina lake basi itakua nafuu kwake kuzilinda endapo ndugu zako wenye tamaa wataingilia kati (hawa mara nyingi hua hawana nongwa sana, ingawa ni rahisi kurubuniwa na ndugu zao wenye tamaa za mali muachane ili wanufaike wao).

Lakini wengine wameenda mbali zaidi ambapo mali zikiwa kwa majina yao hupandwa na viburi na kujiona wao ndio "wakuu wa kaya" na kumdharau moja kwa moja mwanaume ambae alipambana kuifikisha familia ilipo. Kundi hili ni lile linalorubuniwa na ma-ex au majamaa yanayowatongoza tongoza ovyo kila siku na kauli zao mbiu hua "kama vipi tuachane tu!". Yani muachane ili umuachie mali aendelee kudanga na mabwana zake au mwanaume wa ndoto zake ambae alishindwa kua nae wakati mpo kwenye ndoa.

USHAURI: Kijana jipange, hakikisha kabla haujaoa una mali zako ambazo kimsingi atakuja kuzikuta mkiwa mmeshaoana. Haya mambo ya kuchuma pamoja ktk ndoa yamekua ya kiduwanzi siku hizi. Otherwise KATAA NDOA! THESE H*** AIN'T LOYAL ANYMORE!!! Nakaribisha povu [emoji36]
Umemaliza
 
Habari wadau wa jukwaa hili pendwa,

Naomba nienda moja kwa moja kwenye mada.

Mimi nimeoa na Mungu amenijalia watoto wawili. Nafanya kazi sekta binafsi na mke wangu sasa ni mama wa nyumbani. Mke wangu kabla sijamuoa alikuwa amenunua kiwanja chake makao makuu ya wilaya na mimi pia nilikuwa nimenunua kiwanja changu katika wilaya hiyo hiyo ila kwenye tarafa mojawapo.

Tulipooana tuliamua kuishi wilayani, kipindi hicho mimi nilikuwa sina kazi ila yeye alikuwa na kazi japo si mshahara mkubwa na alikuwa kwenye kata mojawapo katika wilaya hiyo nami nilikuwa nimepanga makao makuu ya wilaya, ambapo yeye ndiyo alinunua kiwanja.

Mwaka mmoja baada ya ndoa nikaajiriwa mkoa mwingine hivyo nikamuacha yeye na mtoto, yeye akiwa bado anafanya kazi.
Nikaanza kujenga msingi kwenye kiwanja changu na sikuendeleza nikaachia kwenye msingi. Baadaye nikapiga msingi kwenye kiwanja chake.

Mwaka moja baadaye yeye akaachishwa kazi pale alipokuwa anafanya kazi, ikabidi niwachukue nikae nao mjini. Lakini nikaona ni gharama sana kupanga mjini na mshahara ni mdogo, nikaamua kuchukua mkono nikaendeleza msingi katika kiwanja chake kwa maamuzi kwamba, niendeleze hata vyumba kadhaa halafu niirudishe familia wilaya wakakae huko, mimi nichukue chumba kimoja kupunguza gharama.

Hili pia lilichangia na mgogoro, nikaona siku moja nitapoteza kazi halafu sina pakukimbilia wakati natafuta kazi nyingine. Nikaanza ujenzi na taratibu zote halmashauri nilifanya kwa jina langu. Nikajenga vyumba viwili nikaweka na umeme nikahamisha familia. Kwa sasa wana miezi kadhaa nakuwa nawatembelea walau kila mwisho wa mwezi.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kwamba mke analeta jeuri kwenye hiyo nyumba, kwa kiasi fulani amebadilika, maana juzi kati tulitofautiana jambo fulani dogo nikagundua kiburi kimempanda sana.

Pili, sasa hivi anapambana hati iwe kwa jina lake. Kwa sasa tuna harakati za kuweka maji anajitahidi ajaze fomu yeye kwa jina lake na pia juzi nililipia hela B con na imewekwa sasa yeye anataka kujiandika kama mwenye nyumba.

Ebu naomba ushauri wenu nimuache ajiandike? Nia yangu mimi ni kulinda ndoa yetu, maana naona yeye kama akipata umiliki atanisumbua na tutasababisha mgogoro utakao wasumbua watoto wetu.

Ebu naombeni ushauri kulingana na uelewa na uzoefu, maana mimi kama baba mwenye nyumba ni wajibu wangu kulinda familia yangu, wakina mama wanadanganyika haraka sana. Natarajia kumpiga marufuku harakati zote kwa mamlaka niliyonayo ila nasubiri ushauri wenu.

Asanteni.
Usiruhusu hicho kitu,kataa kwa nguvu zote,huyo anakujaribu aone uta Fanya maamuzi gani,
Weka msimamo mpaka aogope,
Wa kwangu alishawahi kuleta story kwamba viwanja ninavyo nunua tuandike majina yetu wote wawili,nikamwambia kama anaona maisha yake hayana uhakika kuwa na Mimi,na Mimi kama mmiriki wa mali zinamfaidisha yeye na watoto,basi abebe vitu vyake asepe,aende akatafute dume limnunulie viwanja!!
Miaka mitano imepita sasa,alishika adabu,amekubali matokeo
 
"Ndugu zako wanakuombea sana usipate mali ila wanakuombea usalama na amani.Mpenzi/Mke wako anakuombea Upate mali ila hakuombei usalama na amani anataka ufe arithi mali"

Mwisho wa nukuu
 
Back
Top Bottom