Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Mimi hakuna character maarufu wa kwenye cartoon simjui, nazijua na kuzipenda sana.
Na niko mbele kufuatilia, ikitoka tu mpya naruka nayo napeleka home tunaangalia.

Tofauti na mpira na drama za kikorea, napenda sana animation.
Hizo Cinderela, Barbie Mariposa, Little Mermaid n.k ndio kama sala ninavyozijua 😂😂
Luca,coco,Ratatouille etc
I like animation! Mimi binafsi ninaamini wanaotengeneza vile vitu wana akili sana na wako far ahead of time
 
Luca na Coco nazijua, hiyo nyingine nitaitafuta.

Umewahi kuangalia Kubo & the two strings?
Itafute aysee,ni kali sana! Kubo naijua!
Zingine hizi zitafute:
Encanto
Big hero 6
Finding Nemo
Zootopia
The Grinch
Hotel Translyvania zote
Spirited away
Frozen zote
Tangled
Madagascar
Despicable me
Sing zote
Elemental
Your name
Soul
Anza na hizo Nifah
 
Itafute aysee,ni kali sana! Kubo naijua!
Zingine hizi zitafute:
Encanto
Big hero 6
Finding Nemo
Zootopia
The Grinch
Hotel Translyvania zote
Spirited away
Frozen zote
Tangled
Madagascar
Despicable me
Sing zote
Elemental
Your name
Soul
Anza na hizo Nifah
Hapo nimeangalia 7, tatizo siku hizi niko busy nina mambo mengi ila hii list naitunza.
Asante
 
Mimi mwanaume lakini namshangaa mwanaume mwenzangu kuona kuna Jambo haliko sawa juu ya mkewe kisa kupenda katuni.
Ushauri wangu kwake afurahi na azidi kumpenda kama mkewe anapenda katuni na anashinda na watoto akisocialize nao muda mwingi huku akitimiza majukumu yake kama mama. Wengi tuliokulia maisha ya ushuani tunapenda katuni mpaka sasa
Nakazia
 
Mke yopo anajifunza kiingereza hujui cartoons zinafundisha kinge?

Mimi nilimpigia mshikaji wangu yupo rwanda anajua lugha nyingi nikamuomba aniambia ni njia gani nitajifunza ki spanish, ahaaaa akanijibu niangalie cartoons, nilichoka sana yaani mimi na uzee huu niangalie catoons kama mtoto?

So acha mkeo ajifunze watu tuna malengo moyoni lazima yatimie kimya kimya.
 
Usimlaumi mkeo binafsi Mimi Nina miaka 46 ninapendelea kuangalia katuni sana tu hasa Donald duck,tom&Jerry,goofy,pluto,Mickey mouse,luney tunes,tazmania,n.k Tena pamoja na wanangu wanne mkubwa ana miaka 11 ka mwisho ila sio Kwa umuhimu kana 3,tambua ndizo zilizonikuza nakataaje kuangalia uzeeni
 
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale 🤝.

• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "

• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.

• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.

• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.

"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.

• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.

• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.

• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.

• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."

• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.

😎Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu ✍️✍️✍️✍️.


View attachment 2856301View attachment 2856302View attachment 2856303
Analiwa huyo
 
Mtoa mada asitake mabadiliko ambayo yatamfanya ajutee....Shenzi, Pumbaa, Benzai and Ed in Lion King 😄😂
😅😅, basi ngoja nitulie tu, yawezekana uzee umesha nivaa tayari.
 
Back
Top Bottom