Pamoja mkuuSawa mkuu Nimekuelewa, nitajirekebisha kwa hilo.
Sikua na nia mbaya mkuu, nilikua naomba ushauri tu hapa jukwaa pendwa, ndo maana members Mnatoa maoni, mimi au mwingine kama anakutana na hili naye Atajifunza pia. 🙏
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja mkuuSawa mkuu Nimekuelewa, nitajirekebisha kwa hilo.
Sikua na nia mbaya mkuu, nilikua naomba ushauri tu hapa jukwaa pendwa, ndo maana members Mnatoa maoni, mimi au mwingine kama anakutana na hili naye Atajifunza pia. 🙏
😎, Nimekupata mkuu, nilikua nahisi labda kuna kitu hakipo sawa, maana hata utoke - uludi yeye yupo tu kwenye cartoon..
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale 🤝.
• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "
• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.
• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.
• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.
"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.
• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.
• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.
• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.
• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."
• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.
😎Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu ✍️✍️✍️✍️.
View attachment 2856301View attachment 2856302View attachment 2856303
Nipo sana napenda kufurahi, katuni zina upekee wake😄, kumbe na wewe upo mkuu?
[emoji1787][emoji1787] huyo ni tapeli na mdananda Nick ni character wangu pendwa kwenye animation movie ya ZootopiaDuuh..mpka avatar inasadifu.[emoji3577][emoji23][emoji23]
😀😀, Hapana mkuu, mimi nipo na Movie za kitalibani,Angalia animation izo tena kwa umakini sana, utasema ulichelewa wapi kuangalia katuni
1. Coco
2. Encanto
3. Chicken run 1 and 2- hapa nipo naangalia part 2 ya mwaka huu bonge la animation, na mafunzo ya kutosha.
4. Despicable 1, 2 and 3
5. The inclidibles 1and 2
6.Moana
7. The lion king 1,2 , 3 and 4 namba nne imerudiwa kwa kuwa na Kila kitu kimya
8. Madagascar 1,2, and 3, I like to move move song ila , na
9. Marry Madagascar
10. Bellerina ,bonge la animation na mafunzo ya kutosha,
11. Zootopia ,Kuna wimbi mkali kweli wa Shakira unaitwa I will try everything
12. Ratoutole - bonge la animation
13. Puss in boot 1 and 2, huta jutia bonge la animation hasa part 2 last wish ,
•Hatari sana mkuu, 😀,Bro,mimi binafs niko addicted sana na cartoon,naangalia tena naangalia tena nikiwa ma kijana wangu,na imekuwa sehem ya fundisho kwake,tena hata majina nakutakia,Rango,prince moana...etc
Mimi mwanaume lakini namshangaa mwanaume mwenzangu kuona kuna Jambo haliko sawa juu ya mkewe kisa kupenda katuni.Kuna wanaume hamna jema.
Akitulia ndani kuangalia katuni na watoto shida, akiwa mzururaji wa kwenye vidogoro nayo shida.
Ni nini mnataka??
Mke akiangalia Cartoon kuna shida gani!?• Usiwaze mkuu, kama kuna kitu hakipo sawa, kuhusu ME, kilete,
•. But sorry kwa kukukwanza 🤝
• Lakini mkuu, mwanamke ni sehem ya ubavu wetu hivyo tuna haki ya kuwachambua 😋