Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Maelezo meengi yanatuchosha tu yangeandikwa kwa aya mbili. Kila mtu ana interest zake kama wewe unavyopenda pombe. Kwenye familia bana usichukie vitu anavyovipenda mwenzi wako kama havina madhara. Mfano kama anapenda mpira, tamthiliya, katuni. Hivyo ni vitu vya kuchangamsha akili.

Maelezo meengi yanatuchosha tu yangeandikwa kwa aya mbili
Sawa mkuu Nimekuelewa, nitajirekebisha kwa hilo.


Kwenye familia bana usichukie vitu anavyovipenda mwenzi wako kama havina madhara
Sikua na nia mbaya mkuu, nilikua naomba ushauri tu hapa jukwaa pendwa, ndo maana members Mnatoa maoni, mimi au mwingine kama anakutana na hili naye Atajifunza pia. 🙏
 
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale 🤝.
• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "

• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.

• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.

• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.
"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.


• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.

• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.


• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.

• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."

• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.



😎Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu ✍️✍️✍️✍️.


View attachment 2856301View attachment 2856302View attachment 2856303
Kwa hiyo hilo nalo ni Tatizo..!? Naona mnatuchukulia poa hapa, kila Ujinga mnaleta hapa Jukwaaani.
 
Hivi karibuni baada ya kuwa nasoma sana mada za JF, nimeanza kuhisi kuwa uwezo wa watu kiakili kadiri siku zinavyoenda unapungua...

Sasa ukitafakari malalamiko ya mleta uzi, huoni kabisa mantiki ya kulalamika kwake...

Wabongo hebu tutumie muda kutafakari mambo kwa kina kidogo kabla ya kuwa na hitimisho la fikra zetu...
 
Hata Mimi na mke wangu tunapenda katuni , tunaangalia na wenetu , tunaimba na kucheza,, Tumeangalia sana ,puss in boot last wish, saiz tunaangalia chicken run 2, oya mzee mleta Uzi angalia katuni ni tamu kuliko muvi, angalia finding Nemo mzee utajutia , mwisho wa siku utajikita addicted na animation
Upo kama mimi sasa mimi nimeambukiza wote kupenda katuni ninapenda animation mno hakuna animation inayotoka nisiwe nayo, kwenye hizi movie studio napochukua wamenipa na jina la Mzee wa animation nikionekana tu wanajua nilichofata nina hard disk kama tatu zimejaa animation tupu maana ulevi huu umeanza tangu zamani nilipofika chuo nikaanza kuzitunza kwenye disk huwa sifuti kabisa,kiufupi animation movies ndo movies namba moja nazozipenda,
 
Angalia kwanza umri wa mkeo yawezekana kipindi unamuoa ulimkomaza aliruka stage
😐, Amekulia life ya kawaida tu, Labda style ya maisha ameanua kuwa karibu na cartoon, lakini ni too much,
 
Mkuu, mi sijaoa ila issue ndogo iyo achana nae kabisa. Mpe Hi Sana Shem.
 
Ni kawaida tu hata mimi pamoja na utu uzima wangu napenda sana kuangalia katuni..!
😀😀, Aise, Toka nilipo fikisha miaka 24 hivi, cartoon niliwatupilia mbali pamoja na movies za kihindi.
 
Binafsi huwa namshangaa sana mtu anaefurahia katuni,ingawa tangu nilikua nawaona watoto wenzangu wakizifurahia lakini sikuwahi kutaman hata kuona kwa dakika


inafsi huwa namshangaa sana mtu anaefurahia katuni
Hata Mimi cartoon wapo kushoto kabisa, kiujmla huwa siwaelewi
 
Kwa hiyo hilo nalo ni Tatizo..!? Naona mnatuchukulia poa hapa, kila Ujinga mnaleta hapa Jukwaaani.
• Usiwaze mkuu, kama kuna kitu hakipo sawa, kuhusu ME, kilete,
•. But sorry kwa kukukwanza 🤝

• Lakini mkuu, mwanamke ni sehem ya ubavu wetu hivyo tuna haki ya kuwachambua 😋
 
Back
Top Bottom