Mke wangu anatelekeza chumba chake na kwenda chumba cha mtoto

Mke wangu anatelekeza chumba chake na kwenda chumba cha mtoto

Ni kawaida mimi nina chumba na mke ana chumba chake
nikitaka game naenda chumba chake nakula narudi chumba changu au nalala kwake

Sio lazima wanandoa mlale pamoja daily inachosha
Am out!
Kwani hao ni wanandoa au wasimbe tu?
 
Wakuu kwanza kabisa napenda niutangazie umma kuwa bila kulazimishwa wala kushawishiwa nimeamua kwa dhati kutowatetea single mothers kwenye lolote. Acha wapambane na hali zao. Hawa viumbe wana namna nyingi za kukuharibia utulivu. Kuwatetea ni kupoteza muda.

Mimi nilivuta single mama mmoja mwenye mtoto wa chini ya miaka 10 kwa ile style ya SOGEA TUISHI.. ni mwezi kama wa 4 tangu tuanze kuishi pamoja. Alikuja na mwanae ila baadae akaongezeka mtoto mwingine wa kaka yake. Kwa sasa nyumba ina watu wanne. Binafsi sikuwa na tatizo lolote tangu mwanzo kwa sababu nyumba ninayoishi ni kubwa ya kutosheleza.

Bado hatujafanya utambulisho rasmi ila tayari familia zetu zinafahamu tumekuwa wapenzi wa zaidi ya mwaka na tayari tumeanza kuishi pamoja. Siku za hivi karibuni akaanza kusisitiza sana nianze mchakato wa kumuoa. Nikamjibu sawa ila anipe muda kidogo maana kwa sasa kuna mambo ya kikazi yamekaa vibaya mno kiasi kwamba uchumu umeyumba hatari. Wakati ninafikiria labda mwenzangu kashaelewa ghafla wiki moja iliyopita akaibuka kwa msisitizo zaidi nimtambulishe rasmi kwetu na kutuma mshenga.

Nilimjibu kama nilivyomjibu mwanzo na kumwambia kama hataki kunielewa achukue uamuzi wa kurudi kwao kwanza au ikimpendeza hata kujitoa kwenye uhusiano ni sawa tu. Binti alilia sana na kunitupia lawama nikambembeleza tukafanya tendo kisha tukalala. Nikajua kesi imeisha maana mechi ilikuwa ya kiwango cha juu.

Cha kushangaza akaanza utaratibu wa kulala kwenye kochi sebuleni na kuhamisha nguo zake zote kwenye chumba cha watoto. Pia kaanza kutumia public toilet & bathroom. Nguo anabadilishia chumba cha watoto. Siku ya kwanza nilimuuliza kwanini unalala kwenye kochi akajibu mwili wake unauma hivyo kochi lipo sawa kwake.

Kiukweli naona kama nachezewa akili na ninataka nimwambie aondoke na atarudi nikikamilisha utaratibu nyumbani kwao. Ninahisi kubaguliwa ndani ya nyumba yangu.

Ninaamini hapa JF nitapata ushauri ulionyooka. Tafadhalini mnishauri kama kumwondoa hapa ni sawa au sio sawa.
Cha kwanza,wewe ni MPUMBAVU sana,Pili:-hiyo sio mke wako
 
Back
Top Bottom