Mke wangu baada ya kupata kazi na mshahara mnono ameanza kunidharau

mbona hiyo ni kawaida, ulitakiwa uelewe kabla ili ujiwekeze kisaikolojia
 
Pole sana jitahidi kusimama kama Baba wala usiwaze sana kila jambo huwa lina mwisho wake.
 
Kwa ufahamu wangu mwanamke yoyote akikuzidi kipati lazima aanze zarau na kwa hapo kaka Kuna uwezekano mwingine Kuna njemba inawekeza Cha muhimu ni kumzidi kipato zaidi ya hapo zarau hazitaisha
 
Hii huwa napita nayo sana hadi wife anasemaga hawezi kunishauri kwa sababu simsikilizi ila marafiki wakinishauri nawasikiliza
 
Mtani Mzab Mbona hasira kama zote yalishawahi kukuta nini?

Mana toka uanze kuchangia huu uzi unatuita Kenge tu?

Hebu tube heshima yetu bana kama wanawake.
Ndio yalishanikuta kenge yule nimemlisha ananenepa tuu siku nimekosa kibarua eti kenge analitoa limdomo lake mwanaumeume gani huna mbele wala nyuma kama mche wa sabuni....kweli mtu kukulisha na kukuvalisha miaka yote katetereka kidogo tayari kawa mche wa sabuni😑😑😑

Hapana aise nyie ni kenge ikija suala la kutokuwa na shukrana na uvumilivu.
 
Acheni kulialia
Pambana na hali zenu.

Hili taifa wanaume wamekuwa waombolezaji sana kuliko wanawake.
Nini kinafanya wanalialia, je kinaweza kubadilishwa?
Miaka ya huko nyuma wanawake walikuwa wanalialia ila ukaja mpango wa women empowerment but men were left behind. So kulia kupokezana kila gender ishinde mechi zake tu. Jamii hamuonei huruma mwanaume.
 
MZEE MWENZANGU.....

UMEMALIZA KILA KITU.....HUU UZI UNGEISHIA HAPA TUENDELEE NA MIJADALA MINGINE....View attachment 3275930
VIJANA WANATAKA KWANZA MPAKA WAEXPERIENCE HIYO KITU LABDA NDIO WATAONA UHALISIA.

ILA INFACT VIJANA INABIDI WAWE WANAELEWA MISINGI YA KIUME,BONUS BOOK HIYO YA KUFIKA MALENGO YAKO BILA KUSUMBULIWA NA HAO VIUMBE🀝
 

Attachments


Uza hiyo nyumba na Kiwanja lipa mkopo wa wenyewe panga Malezi bora ya watoto; Huna mke hapo, washaanza kumla, mpige matukio aende zake, atakuja akuue na mawazo, nasikitika hutanielewa!
 
Mpige tukio hata kumla kichwa otherwise na wewe utapata ugonjwa wa sukari na ndo hapo anataka,wahi biashara asubuhi,kama yuko tayari mpeleke kwao.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwanza pole sana.
Hapo cha kulalamika kikubwa ni hizo dharau labda lakini kamwe usilalamike kwa sababu ya majukumu ambayo umetimiza kama baba mf. Hiyo ya kujenga nyumba na kuhudumia familia yako
Kingine wanaokushauri muachane unamuacha ili kitokee nini,ufundishe moyo wako kuishi naye namna hiyo maana ukimuacha ndio mwanzo wa kutangatanga na watoto hao mnawapeleka wapi??

Halafu hata huku nje sio salama pia utampata mtu naye atakuWa mwema mwanzoni lakini ukamuweka ndani ukakuta ni shida tupu bora hata uliyekuwa umemzoea.
Kama hana madhara ya kifo au kukupa kilema chochote ishi naye kwa namna aliyochagua.

Pole sana kwa mikopo ila itakwisha na maisha yako yatarejea kwa upya tena...ni swala la muda tu braza utakuwa sawa ila mara hii usifuate ushauri wake sana.
 
Mwanaume analiaje sasa?
Ukiona mwanaume analialia basi tatizo lilitokea mbali, hqkumdhibiti mke wake toka mwanzo.
Ni matokeo ya mkusanyiko wa kupuuzia viashiria vya dharau ama uvunjifu wa heshima.

Suhuhisho ni wanaume kuweka mipaka, toka unajuana na mwanamke wako inatakiwa kuwa na mipaka yako ya nidhamu ambayo huwezi kuvunjiwa.
The same applies to women..mtu asivuke mipaka akakudharau.
Unajua uhuru ni kitu kizuri, lakini usipite mipaka hadi kufika hatua mtu anaweza tu kuropoka lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…