Mke wangu hampendi mtoto wangu niliyempata kabla ya ndoa

Kumbuka kuna waliobakwa na waliokimbiwa na waume au wake zao na kuachiwa watoto.

Siungi mkono kwa wanaozaa nje ya ndoa wakiwa ndani ya ndoa
Kubakwa huwa ni rare case pia kukimbiwa na mume sio excuse ya kutafta mserereko na kuacha watoto wateseke maisha huwa ni vita Kali sana, ka mtu ulizaa jiandae kwa lolote lazima tuwe na huruma na tufikirie vyema watoto na kuja na mbinu za kuwalea vizuri kuepusha abuse, na watoto kuharibikiwa kiakili, sikuhizi watu hawana ndoa wao ni kuzaa tu vile Wana mayai bila kufikiria ulezi.
 
Mtu anajijua hayupo tayari kulea halafu wanatiana mimba

Hivi hii nayo ni hoja ya kujitetea kwani!
Yani St Anne Hawa wanaume wao kila mwanamke akimtani ana mwambia nizalie na wengine hawajaoa ila wametia mimba mabinti zaidi ya kumi then akikuoa mwanaume anakukusanyia ka shule uwalee na haya maisha yalivo magumu hivi , na watoto wote mtawapa kweli huduma za msingi kama ada na shule nzuri.
Pia Kuna wanawake na wao wakishaona mwanaume yuko vizuri kipato na ana vitz wanategesha mimba Ili wapate child support then hao wakizaa wanategemea mwanamke mwingine eti awasaidie kulea huyo mtoto kilazima na akigoma eti roho mbaya anayo
 
Kila mtu apambane na zigo lake.

Nashangaa watu wanalialia humu, wanatafuta sympathy kisa makosa yao wenyewe! ..
Watazidi kupambana na hali zao,,,mtu akitaka fairness hapa duniani basi ajiheshimu asitotoe hovyo.
 
Sikuhizi watu kuzaa nje hata hawajali hicho kitu mwishowe ndio kuleta migogoro na kuleta shida kwenye ulezi wa watoto maana inakuwa kufichwa fichwa tu kwa watoto
 
Kila mtu apambane na zigo lake.

Nashangaa watu wanalialia humu, wanatafuta sympathy kisa makosa yao wenyewe! ..
Watazidi kupambana na hali zao,,,mtu akitaka fairness hapa duniani basi ajiheshimu asitotoe hovyo.
Ni kweli kila mtu tu apambane na Hali yake ya maisha na asitafte lawama kwa watu wengine kisa starehe aliyoi fanya tena, wanaume wao huwa hawajali kazi Yao kuchojoa tu zip then baadae Wana force mambo sijui ya upendo.
Maisha yenyewe magumu kila kitu kimepanda ukimpata mpenzi badala mu enjoy mnaletewa agenda nyingine woooi
 
😂😂 you dont even know where your spirit will be after death let alone ability to guide your kids after death.

...Mimi sitetei wanaozaa nje wakiwa ndani ya ndoa.

...Natetea waliokuwa na watoto kabla ya ndoa maana baadhi yao (sio wote) walizungukwa na mazingira ya bahati mbaya sana.

Roho ya ubinafsi ni zao la shetani,sisi watu weusi hali hii tunayo sana...na hili linaonekana sana kwako na habari ya 'fighting for my eggs'

Tuache roho mbaya na ya ubinafsi.Wenzetu wazungu wanabarikiwa sana kimaisha kwa kuwa focus yao ya kusaidia ni beyond 'eggs',siblings and the like primitive ideas. Wenzetu wana vision kubwa zaidi wanafocus kusaidia communities and the world at large(eg.Madonna na Angelina Jolie wanalea zaidi ya watoto 10 wasio wao tena wengine ni blacks na wanaishi nao na wamewaingiza ktk urithi wao)...na hii ndio tabia ya kufanana na Mungu,maana Mungu anaruhusu mwanga wa jua kwa kila binadam wema kwa wabaya na sio wema pekee.BE A BLESSING TO THE WORLD AND NOT JUST YOUR FAMILY...it is selfishness and satanic .

...Think beyond the box,and stop being narrow minded person as to be a selfish mother with no legacy when you die.
 
You are daaaamn wrong,,tunaishi kwa word ambayo iko structured my dear,, social value structure our f*cking society,, hata hierarchy iko socially constructed,

By nature man ni aggressive from the genes (xsome number 27 if i am not mistaken), so just because we're aggressive doesn't mean we can move around and fight with anyone or rape,, bloody NO., Following the structure of the society haiepukiki maybe kama u are a tyrant.

A mom should feel the pain of a person,, hata kama hajamzaa yeye

But unfortunately miss we can't put ya kwa that category ya being a mom,,, but waweza kuwa a mother, that's what you are

In our society what u stand for ni morally wrong,, no one can change that,, misimamo yako ikipingana na ya Society hyo ni chaos tayari

U want your ideology itumike! Right? Nenda katengeneze your own society au deconstruct hii structure tuliyonayo now, then rebuilt yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi siishi kwa wrong perception za society ambazo huwa zimepitwa na wakati I live in my own world, free like molecules in H2O and I enjoy it, sifungwi na jambo lolote kile, kitu unachokiamini I don't believe it, hasa hyo ya pain za uzembe ni I don't care kabisa, life is to short to stress myself minding people's busineses jamani woooi
 
Mawazo ya kizazi cha sneki yaani unampendaje mtu umchukie yule anaempenda yeye? Alooh kuna watu mna roho kama ina kipande cha chuma ndani
 
Wengine humu wanashauri eti kumpeleka mtoto akalelewe na bibi,huku ni sawa na kumtupa mtoto.

Upungukiwi kitu kulea mtoto usiemzaa,KUMBUKA UKIFA LEO WATOTO WAKO WATAFANYIWA KAMA ULIVYOWAFANYIA WATOTO WA WENZAKO
Fact na ni kwa matured tu ndio wenye kulielewa hili
 
Sema una roho mbaya sana! Wapo wenye upendo wa kweli, kama wewe huwezi usisemee mioyoyo ya watu! Kuna watu wamelelewa na mama wa kambo kwa mapenzi mazuri mno. Baki na roho mbaya yako, usiambukize watu wengine. , Kwan ukimpenda utapungukiwa nini!
Kma umeolewa na una watoto, umejaribu kupiga hesabu, ukifa sasa ivi ni nani atakaa na watoto wako????? Hao watoto sio wote unakuta baba zao wameachana na mama zao, kuna vifo, we unafikiri unadumu milele, au una guarantee utamaliza malezi ya watoto, had wajitegemee!!! hata vitabu vya dini vinasisitiza kumpenda jirani yako kama unavyojipenda!
 
Jibuni hoja yangu msikimbilie roho mbaya hivi unazaaje mtoto then utegemee asiye mamake akulelee, watu acheni uzembe Dunia ya Sasa ni ubepari sio kuzaa kutegemea huruma za wasio mama kulea starehe zenu na mtu asije kusema wengine mbona wanafanya hivi hao hawana kazi za kufanya.
Acheni zinaa zenu zinazo gharimu watoto wenu mxieeeew zenu kweli
 
Usingizie vifo hyo inajulikana hapa tunaongelea walio hai na tatizo linalokua daily nyie mnasingizia roho mbaya kweli?
 
Na wewe acha tamaa zako zinazogharimu utu wako!

Hela unapokea then mtoto hutaki kupokea! Hakuna mapenzi hapo maana kama utashindwa kumpokea na kumpenda mtt mdogo asie na hatia,mtu mzima mwenye hatia kibao utamuweza? Mapenzi ya kufuata hela hatuyataki.

Ni heri mtt abaki maana ni kwangu ndio nyumbani kwake na ni ndugu na damu yangu ila wewe uondoke tu maana una kwenu...kwa baba yako.
 
Usingizie vifo hyo inajulikana hapa tunaongelea walio hai na tatizo linalokua daily nyie mnasingizia roho mbaya kweli?
Kwa nini azae nje tuanzie hapo?

Kwa nini anazini nje na wewe mkewe upo?

Tibu mapungufu yako ktk ndoa yako,vinginevyo utaletewa watt tu hakuna namna,tatizo limeanzia kwako.
 
Wanawake ni viumbe wabinafsi sana,wao humtazama mtoto kama mke mwenza yaani wanakuwa kama wanamuona mwanamke uliyezaa naye na siyo mtoto kama mtoto.
Wivu wao ndiyo hupelekea chuki.
Wanaume wachache mno wanaonyanyasa watoto wa wake zao.
 
Sisi tumelelewa kuishi na watu,bila kujali ni ndugu yako au laa
Nimeanza kuishi na watu(siyo ndugu) hata kabla sijaoa.
Swali langu ni Je kuna ugumu gani kuishi na mtu mwingine achilia mbali mtoto wa mumeo/mkeo?basi watu tunatofautiana sana.
 
Kinachopondwa na kuchukiwa Ni tabia za wanawake husika.

Sio mtoto,
Sijawai sikia au kuona mwanaume anamchukia mtoto wa single mother Hata sikU moja.

Wengi wanaoishi na single mother, wanalea effectively watoto wao.
hatuwapendi ila hatuna nafasi ya kutekeleza chuki zetu ,mwanamke anakaba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…