Mke wangu hampendi mtoto wangu niliyempata kabla ya ndoa

Mke wangu hampendi mtoto wangu niliyempata kabla ya ndoa

Mmekutana mme/mke ana watoto mnakubaliana kuoana inakuwaje watoto wasiwe huru Na baba yao Na kuja kukaa na baba yao au mama yao
Mke akishaolewa anaona anammliki mme kuliko wengine
Kama mama kashaolewa na ME mwingine?
 
Mwanoa ni ndugu yako ni damu yako,mwanao hawezi kukusaliti ata ukiwa maskini,mgonjwa nk.

Mwanamke asiyempenda mwanao huyo hakupendi maana kama anashindwa kumpenda mwanao(damu yako) anawezaje kukupenda wewe?

Hiki ndicho kipimo cha mapenzi yake kwako,kama hampendi mwanao it's a wake up call for you...achana nae haraka before it's too late.

Mtoto hana hatia yoyote kwa yaliyotokea uko nyuma.
Ndoa na watoto ni vitu 2 tofauti.

Upendo upo tofauti mkuu.
Unavyompenda MUNGU wewe ni tofauti unavyompemda Baba yako na pia ni tofauti utakavyompenda mama yako. Ni upendo tofauti kabisa.

Wewe unavyompemda mama yako ni tofauti utavyompenda mkeo.
 
Hivi mwanamke kumkataa/kumchukia mtoto wako uliyezaa kabla ya kumuoa. Kuna mapenzi hapo? Yaani hampendi Mwanao je wewe atakuwa anakupenda kweli?
Hii ni ngonjera au shairi?

Mama yake ulimwacha wapi?

Jawezi mpenda hata kwa udi na uvumba ila atapretend tu
 
Hayo mambo ya mwanamke kutokumpenda mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa inabidi mwanamke ayaseme kabla ya ndoa ili kumrahisishia mwanaume maamuzi. Sio wakati wa urafiki na uchumba unajifanya kumpenda sana mwanangu ila baada ya ndoa ndio mtoto anaanza kuwa mbaya.
 
Mama wa huyo mtoto yuko hai?
Kweli kabisa maana u single father/mother unasababishwa na mengi ikiwemo KIFO. Unataka mtoto huyo alelewe na nani kama siyo wewe mpenzi wa mamake/babake?
 
Jujaelewa point ya msingi. Ngoja nikufafanulie kidogo. Kabla ya maisha ya ndoa, mwanamke alijua kuna mtoto tayari aliyezaliwa kabla ya yeye kuolewa. Na akakubali kuwa atampokea na kumpenda. Baada ya kuingia ndani na kupata ujauzito ndio akaanza kuonyesha figisu zake juu ya Yule mtoto. Na baada ya muda akaanza kudiriki kutamka wazi kuwa hawez kuishi na huyo mtoto na siku aliletwa yeye ataondoka. Mtoto alipoletwa akaona Hana ujanja akabadilika na kusema asamehewe Yuko tayari kumlea mtoto na kumpenda. Swali ni Je kuna mapenzi hapo? Anastahili kukaa na huyo mtoto? Anastahili kuitwa mke????????????
Naona ukumbuke story ya nabii Ibrahimu na Mkewe Sarah baada ya kuzaliwa Isaka, alimfanyaje Hajir?

Mwanzo 21:12
 
Katika hili pachiko, inaonesha Mkuu cariha anayo maslahi na hoja inayoendelea. Hata hivyo, ni vema kuukubali upendo wa Baba kwa watoto wake hata kama hukubali au kuridhia mahusiano na nasaba yao. Kubali hata kiaina ili na wengine waweze kupona.
 
Watu mliozaa kwanini huwa mnapenda ku force watoto wenu wapendwe na wengine kilazima hasa ukichukulia mitoto yenyewe huwa mikorofi imeathiriwa na ugomvi wenu wa mahusiano yali yovunjika na ni watoto wasio pendeka hata ufanyeje wataona huyu sio mama yetu.

Kuku tu mwenyewe huwa anakimbiza vifaranga visivo mhusu sembuse binadamu, na kama kweli ulikuwa na upendo why haukupatana na uliyezaa naye mkamlea mwanenu yeye aligoma then una force mtoto apendwe na mpenzi wako mpya.

Mpenzi wako kaja kwako ku enjoy mahusiano na sio kuhangaika na mtoto asiye mhusu
Unahitaji maombi!
 
Nakazia
Kuku Tu Mwenyewe Anafukuza Vifaranga Visivyo Vyake
""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Mbinguni Una Nafasi Yako Tena Utakaa Kwenye Kivuli
Ukiwa~Zoom Kama Jiwe
Kwa hiyo na wwe uko tayari kumpanda Mama yako kama Kuku anavyofanyaga!? Kweli nimeaamini, kuna binaadamu nao wana akili kama za kuku!!
 
Back
Top Bottom