Mke wangu hana hamu ya kufanya mapenzi na mimi. Nifanyeje?

Mke wangu hana hamu ya kufanya mapenzi na mimi. Nifanyeje?

Kama ishu ipo kwa muda mrefu, maana yake pengine alilazimika tu kuolewa na wewe, hakua amekupenda.

Na sasa anastrago kua karibu na wewe sababu hana hisia na wewe, hivyo inakua ngumu kwake kua wa kwanza. Na hata unapomfata wewe sometime ni basi tu sababu hana jinsi ila angeweza angekua anakunyima kabisa kila siku.

Suluhisho hapa ni kuachana na hii ndoa ili kuepusha mabaya zaidi uko mbele. Usiangaike nae sana itakuumiza zaidi mana swala la kumbadili mtu hisia haliwajawai kua wazo zuri. Iyari siku zote ni bora zaidi.

Pole sana aisee. Japo hii ni kawaida na inaweza mtokea mtu yoyote
 
Hamuwezi kufikiria sababu nyingine zaidi ya hii ya kijinga? Pendeni wake zenu nyie viumbe mnawatreat vibaya halafu wakibadilika na kuacha kuwajali kama mwanzoni mnadikiria kuna mwanaume mwingine.
Huyo mke ana maumivu ya muda mrefu, mume hamjali anamchukulia poa.
Mtoa mada atafakari ni wapi alikosea.
Visamehe bure vitoto vya form two vya hapa jukwaani mkuu. Yaani havinaga comment nyingine zaidi ya "unachapiwa".
 
Naomba ushauri kuhusu changamoto yangu ya ndoa

Ninaishi na mke wangu, lakini kuna jambo ambalo limekuwa likinisumbua kwa muda na sijui nifanye nini. Katika maisha yetu ya ndoa, mara nyingi ni mimi ndiye ninayeanzisha suala la ukaribu wa kimapenzi. Kwa upande wake, mara nyingi haonyeshi hamu au kuhitaji ukaribu huo, na wakati mwingine nikijaribu kuanzisha, nahisi kama vile namlazimisha.

Hali hii imenifanya nianze kujiuliza maswali mengi. Je, ni kawaida katika ndoa mmoja kuwa na hamu zaidi kuliko mwingine? Je, mwanamke hapaswi pia kumhitaji mume wake na kuonyesha hisia zake, au ni kawaida mwanaume kuwa ndiye anayeanzisha kila mara?

Kuna wakati najiuliza kama labda hanipendi tena kama zamani. Kinachoniumiza zaidi ni kwamba hajawahi kuniambia wazi tatizo ni nini, na mimi pia sijui kama kuna kitu ninachokifanya ambacho kinamfanya ajisikie hivyo.

Nimejaribu kufikiria sababu mbalimbali, lakini sitaki kumhukumu wala kumshinikiza. Nataka kuelewa tu kinachoendelea na nijue namna sahihi ya kulishughulikia jambo hili.

Kwa wale wenye uzoefu wa ndoa, mnafikiria nifanye nini? Je, nimkalishe chini na kuzungumza naye kwa uwazi kuhusu suala hili? Na kama mke wako hataki ukaribu wa kimapenzi mara kwa mara, unajuaje kama ni suala la upendo, msongo wa mawazo, changamoto za kiafya, au kuna tatizo lingine ndani ya ndoa?

Naomba ushauri wa kweli kutoka kwa watu wenye uzoefu.
Nenda YouTube Wazungu wameongelea sana hii mada.
 
Wanawake sometime ni viumbe visivyoeleweka vinataka nini na lazima wajue huwezi kumpata mwanaume ambaye ni perfect asie na mapungufu huyo mwanaume hayupo Dunia wakijua hili hawatapata shida mfano niliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye nilimpenda nilijitoa kwake japo nilikuwa sikuwa na pesa kiasi hicho lakini nilijitahidi kwa uwezo wangu nilikuwa Nampa zawadi bila kuniomba, sometimes nakutumia muamala bila kuniomba, namshauri kwenye mambo ya msingi, nilikuwa simcheat, nilikuwa humble kakwe na ni mkali akifanya ujinga na kwenye sex nilikuwa vizuri kiasi ambacho anapendea tufanye weekend badala ya katikati ya wiki huwa anaona ninamshoka nakumfanya awe mvivu kesho yake kwenda kazini pamoja na yote haya alinicheat na mfanyakazi mwenzake na kila kitu kikavurugika hapo ndio maana huwa nashindwa kuelewa jinsia yenu
Ulikuwa vizuri kwenye sex hadi akawa anataka mfanye weekend tu, katikati ya wiki hataki maana inamfanya awe mvivu kesho yake....
Mkuu umejisoma vizuri kweli hapo? Mtu akiwa anakukuna vzr huwa hatujali ni siku gani ya nazagamuano. Haipo hiyo ndugu...
 
. Mbona unatoa conclusion isiyo na kichwa wala miguu.. 🤔 🤔 🤔

. Unasema tupende wake zetu, nyinyi huwa mnapenda wanaume zenu.??? Zaidi zaidi mnamiliki mahawala kibao huko mitaani hata mkiwa ndani ya ndoa na mnafika mbali zaidi munaleta na mimba ndani ya nyumba.. 🚮 🚮 🚮
Hakuna conclusion yoyote nimetoa. Nyie ndo mnasena atakuwa na nwanaume mwingine, hiyo ndo conclusion mmetoa. Mimi nimeshangaa kwanini muwaze hivyo tu wakati sababu zipo nyingi?
 
Kama hakua hivyo mwanzo kuna mambo mawili yanayoweza kuua hisia kwa mwanamke.
1. Kumchiti halafu akajua 90% hisia zinakufa
2. Humfikishi kileleni asilimia kubwa mwanamke akiwa hafiki kilelen anaweza kupungza hamu ya kujamiiana
 
Ulikuwa vizuri kwenye sex hadi akawa anataka mfanye weekend tu, katikati ya wiki hataki maana inamfanya awe mvivu kesho yake....
Mkuu umejisoma vizuri kweli hapo? Mtu akiwa anakukuna vzr huwa hatujali ni siku gani ya nazagamuano. Haipo hiyo ndugu...
Tukifanya katikatika ya wiki kesho yake haendi kazini anakuwa amechoka ndio maana tukachukua huo uamuzi iwe weekend tu
 
ushauri wangu na niko serious kabisa wala sitanii. pamoja na ushauri mzuri uliopewa jaribu muda mwingi kufanya nae kazi za nyumbani pamoja kama anapika kaa jikoni uwe unasaidia. jaribu kama anafua nguo wewe uwe unasuuza na kuanika, kama anadeki wewe kunja nguo au nyoosha, najua unalo jukumu la kutafuta fedha pia jaribu hili na ufanye ndio utaratibu wako kufanta hata task moja pamoja na mkeo utakuja kuniambia kama hii shida itajirudia.
ndugu mtoa mada nakusihi zingatia huu ushauri wangu. Naelewa jinsi jamii yetu inavyouchukulia ushauri huu nakutia moyo pamoja na mambo mengine ulioshauriwa jaribu na hili
 
Back
Top Bottom