Mke wangu hataki kunisamehe. Nifanyeje?

Mke wangu hataki kunisamehe. Nifanyeje?

Tuelezee makosa yako ili nasi tujaribu kukupa muongozo. Ila cha kwanza kwa wakati huu fanya toba kwa Mungu wako, kiri makosa yako na utoe sadaka.
 
Unaweza ukanipuuzia, ila kuna jamaa yangu aliachwa na mkewe miezi 6, lakini mwanamke alirudi mwenyewe tena kwa kuomba msamaha...
Ukimpata mganga wa kienyeji asie tapeli haichukui wiki 2 mkeo lazima arudi, labda kama umepost kwa mzaha.
 
Leo tarehe 28-07-2021. Usipokee simu yake, usimpigie wala kumtext sms mpaka tarehe 27 -08-2021.
Atakutafuta , atakuja kukuomba msamaha badala ya wewe kumuomba msamaha.
Atarudi nyumbani mnaendelea kuula ujana.
Ukijikosha tu kumtafuta utampa kiburi atakufanyia malipizi yaani atagawa nyuchi kwa kwenda mbele
 
Umeamini wanawake tuna nafasi kubwa, haya ujuaji wako umefikia wapi sasa?

Pambana bro....ila ujue sisi ni kila kitu kwenu
 
Siumesema waenda kaZini ni wasumbufu oa asiye fanya kazi uone. In short mahusiano hayakosi xhangamoto ila makosa ya kujirudia rudia makusudi ni hatari kuendelea na hayo mahusiano nfano umalaya wa mwenza wako daily
👍
 
Sasa mwanamke Hadi kuondoka huwa hana cha kupoteza kabisa na hata kuaga hamna umuhimu. Hata huko Police watafanyaje wamfunge arudi kinguvu[emoji23][emoji23][emoji23] kah, police wenyewe yao yamewashinda loh. Love ikifa police hawataweza kukusaidia hata kidogo
Nina maana ya kutoa taharifa tu kama kupotea kwa kitu chochote.
 
Asante ndugu asante sana ishu ni tukiwa wote anatakaga sana sasa inakuwaje huko au anavumilia.

Hahaa mkuu acha hizo.....

umefanya nicheke bure kwa jambo serious kama lako

Hizo mambo hazinaga makombo, hata akirudi hutajua njemba zilizojisevia
 
Jokajeusi yamekukuta tayari,we rud na Id yako ile tuliokuzoea nayo ambayo kutwa kucha ni kuwasema ambao hawajaoa bikra
Ahaaaa! huyu ndo wa kutusimanga tuliooa single mothers kisa aliooa bikira. Kwa taarifa yako ukiona mwanamke anaondoka kwako na haondoki na kitu, ujue anapata huduma na mahitaji kwa mume mwenzio.

Mpeni pole joka jeusi. Kidume cha bikira.
 
Ni aibu nilichofanya ila sihitaji mwanamke yeyote. Mke wangu nimeanza nae mbali sana tokea hatuna kitu. Siwezi kuruhusu tu mtu mpya kirahisi ana stahili kufurahia matunda ya nyumba sababu alikuwepo kipindi cha ku struggle
Ashaolewa sasa na wanaoweza kubembeleza. Wewe si huwezi kubembeleza? Acha walee halafu utakutana naye katakata ile sawasawa.
 
Ubaya ni kwamba hisia za mwanamke zikiisha huwa hazirudi kirahisi, yaani akishasema NO ni NO kweli, hapo hata kama akirudi hatakuwa na mapenzi yaleyale kama ya mwanzo kwasababu umeshavunja uaminifu.
 
Habari wakuu wa kaya. Iigweee

Nina account humu ila imebidi nifungue nyingine sababu tunafahamiana na baadhi ya watu humu na mimi ni mjuaji yani mbele za watu napenda kuonekana mwanamke hawezi kunipelekesha.

Nimemkosea mke wangu wa miaka 7 ya ndoa. Miaka 7. Tuna watoto wawili. AMEGOMA KUNISAMEHE AMEONDOKA, NAUMIA KUWAZA KUNA MWANAMME ANAWEZA KUMMLIKI.
Pole kwa ujinga uliofanya kwa mkeo. Ila naamini sasa ndio unaona umuhimu wake wakati hayupo ktk hinaya yako..na hofu kubwa ni pale unapowaza mtu mwingine akimmiliki wakati wewe ulishaona unaumiliki wa kudumu😀😀😀, anyways..nakushauri kwa sasa mwache kabisaa atulie ajifikirie kwanza....anahitaji kupata muda wa kutafakari maisha yake..hapo ndio anapima mizani ya ndoa na usingo upi unafaa.

So wewe jitahidi kuwa mpole...endelea kumjali na watoto..bila kumfuatilia maisha yake..hata siku ukiona kachelewa kurudi..usipaniki mbele yake..mpe heshima ktk maamuzi yake. Trust me...ukuonyesha hivo..atakupenda tena..na hata kama kuna mtu anamuwaza...ataona hapana..kuna kale kamsema..shetani unaemjua ni bora kuliko malaika usiemjua. Tulia..play gentle..cheza na wanao bila kumsema mam yao..kimsingi show love..baada ya mda...ataona mzani wa ndoa mzito kuliko single..na atarudi kwako!
 
Back
Top Bottom