Mke wangu hataki kutumia pesa yake kununua kitu chochote kwa matumizi ya familia

Mke wangu hataki kutumia pesa yake kununua kitu chochote kwa matumizi ya familia

Sasa nini maana ya ndoa!? Zamani mke alitunzwa na kumtegemea mmewe kwa kilakitu sababu hakuruhusiwa kufanya kazi wala kumiliki mali yoyote ila kwa kizazi hiki cha 50/50 haina maana kuwa na mke mfanya kazi ambaye hachangii chochote mezani. Bora abaki kuwa mama wa nyumbani asaidie kazi za hapa na pale.
#NDOA NI UTAPELI
#NDOA NI KWA WANAWAKE TU LABDA NA WANAUME DHAIFU
#KATAA NDOA
Huyo mwanamke mwenye kazi kama kununua chumvi tu hawezi, ataweza kuisaidia familia ukifariki!? Mke ni mama wa nyumbani nje ya hapo ni kujitafutia stress.
#THAMINI UHURU WAKO KIJANA
#KATAA NDOA
Mwaka juzi nilikuwa siwaelewi mkikataa ndoa ila sasa nimeanza kuwaelewa. Zamani before 1990 ndoa ilikuwa ni ya muhimu kwa sababu hakukuwa na sera ya hamsini kwa hamsini. In modern society, ndoa ni upumbavu kwa sababu hakuna correlation kati ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na Sera ya hamsini kwa hamsini.

KATAA NDOA. NDOA NI UFALA
 
Mke mwema anayetajwa kwenye maandiko METHALI 31 hakutajwa ni mbinafsi

METHALI 31:14
14. Huleta chakula chake kutoka mbali.

METHALI 31:27
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

Mungu anataka mke awe wa aina hii ndiyo maana hasa ya msaidizi

Hapo hauna mke uliooa malaya
 
Ulisha kufa umekufa, acha kuhangaika mambo ya nikifa itakuaje ishi maisha yako sasa ungali hai, ukishakufa Mungu atawapa familia yako namna nyingine ya kuishi

Lazima ufikirie KIFO wala sio swala kuogopa na lazima utengeneze presence yako baada ya kuondoka.

WATU ambao ni wabinafsi ndo huwa hawafikirii KIFO na kuamini mambo yatajiseti na mwisho kuacha familia yako ktk mikono ambayo sio salama.
 
Mke mwema anayetajwa kwenye maandiko METHALI 31 hakutajwa ni mbinafsi

METHALI 31:14
14. Huleta chakula chake kutoka mbali.

METHALI 31:27
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

Mungu anataka mke awe wa aina hii ndiyo maana hasa ya msaidizi

Hapo hauna mke uliooa malaya

Hakika kusaidiana muhimu Sana .
 
Mke wangu hawezi kutumia pesa yake kwa matumizi ya wote yaani hata nikikwama nikamuomba pesa ananiwekea na riba au hata nikiwa mbali yeye akanunua kitu ndani hata kama ni chumvi au sukari ukirudi anakwambia anakudai wakati alinunua kwa ajili ya matumizi yake.

Je nifanye nini!
Mwanaume ndio, msingi wa, familia, kama, ulivyo msingi wa, nyumba, hutqkiwi kulalamika kabisa, we mpelekee moto tu
 
Lazima ufikirie KIFO wala sio swala kuogopa na lazima utengeneze presence yako baada ya kuondoka.

WATU ambao ni wabinafsi ndo huwa hawafikirii KIFO na kuamini mambo yatajiseti na mwisho kuacha familia yako ktk mikono ambayo sio salama.
Hata ukifikiria, kifo hakibishi hodi anytime kinakuja, unafikiri waliokufa hawakuwa na mipango? ninachosema pambana kuweka maisha yako sawa, lakini sio upambane kwa kufikiria kifo, kwa sababu katika kupambana kwako ukikosa, kwa sababu unakifikiria kifo utajikuta unakikaribisha
 
Kwanini mkuu unakuwa muoga Sana hivyo
 
Kwanini mkuu unakuwa muoga Sana hivyo
Sio muoga kuna kiongozi wangu wa kiroho amekufa wiki iliyoisha na ameacha mke na watoto watatu, hao watoto bado wadogo, hoja yangu ni hii unafikiri yeye alikuwa hawezi kuhusu watoto wake? lakini je anajua watoto wake wataishije baada ya yeye kuondoka? ni hakika hajui lolote linaloendelea
 
Kwahiyo suluhisho ni lipi kwa mtoa mada?

Amuache ?

Ajaribu kumfundisha na kumpa elimu ya MAISHA namna ya kujali familia ?

Au atafute mama wa nyumbani tu?

Mimi ushauri wangu aanze kwa kumpa Elimu amuambue aachane na ubinafsi na ajue kuwa wanajenga nyumba moja .
 
Wewe jamaa utakuta ukishatoa hela ya kula ndio basi unashindwa ata kumhudumikia mkeo mahitaji yake kwa sabab ana vijipesa vyake

Lazima mwanamke awe mbinafs hela zake halaumiki ata kdg.
 
Kosa: Kutegemea pesa ya mwanamke.
Usimlazimishe mwanamke kukupa kitu chochote kile. Hakuna mwanamke anayependa kuangalia chini. Elewa nilichokiandika.

Cha kufanya: Endelea na maisha yako, timiza mahitaji yote yanayohitajika na familia yako, ila usisahau kujipenda pia, raise your attractiveness ili kuongeza value. Panua fikra zako kutafuta channel zaidi ya moja ya pesa, ukimkopa, fanya biashara , then rudisha pesa zake, tumia faida kuendeleza biashara yako. Usionyeshe uko needy na pesa yake, we ishi as if you don't depend on her.
Ndio maana wanaume tunakufa haraka..
 
Jukumu la kuihudumia familia ni la mume ila huyo mkeo hafai, anadai hadi chumvi huo ni ubinafsi na uchoyo uliokubuhu. Kuliko nioe mwanamke wa hivyo bora nisioe kabisa. Huyo maisha yakiyumba kidogo hakuna rangi ya dharau hutoacha kuiona.
 
Mke wangu hawezi kutumia pesa yake kwa matumizi ya wote yaani hata nikikwama nikamuomba pesa ananiwekea na riba au hata nikiwa mbali yeye akanunua kitu ndani hata kama ni chumvi au sukari ukirudi anakwambia anakudai wakati alinunua kwa ajili ya matumizi yake.

Je nifanye nini!
Piga chini hiyo mama utakuta ni kibenteni ndo kinakula hiyo hela
 
Kosa: Kutegemea pesa ya mwanamke.
Usimlazimishe mwanamke kukupa kitu chochote kile. Hakuna mwanamke anayependa kuangalia chini. Elewa nilichokiandika.

Cha kufanya: Endelea na maisha yako, timiza mahitaji yote yanayohitajika na familia yako, ila usisahau kujipenda pia, raise your attractiveness ili kuongeza value. Panua fikra zako kutafuta channel zaidi ya moja ya pesa, ukimkopa, fanya biashara , then rudisha pesa zake, tumia faida kuendeleza biashara yako. Usionyeshe uko needy na pesa yake, we ishi as if you don't depend on her.
Una point!
 
Back
Top Bottom