Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Mke wangu hataki niendeshe gari alilonunua. Nakereka sana

Ndio tatizo la wanawake wa kuchuma wote, ulipoambiwa ujipange ndipo uoe uliona watu hawataki utiane kwa kujinafasi. Pambana na hali yako.
Kuna mwanamke mmoja aliwahi kuniambia kuwa mimi nimekutengeneza mpaka umekuwa hivyo ulivyo, nilimkata jicho hilo, akajikuta anaomba tu msamaha mwenyewe. Kwasababu yeye kaja na begi lake tu, kila kitu changu.
Hahahahhaha kmmmk walai! Kakutengeneza kwa ufundi upi alio nao?
 
Sisi ni watu wa ajabu sana. Hapo gari lingekua la mwanamke angelichukua bila hata kuomba. Na angepewa bila gubu. Shida sisi ni wabinafsi sana.

Sent From Galaxy S9
Lingekuwa la mumewe angelitumia freely na kuligonga pia kisha anapiga simu tu beby nimegonga pikipiki huku njoo unisaidie😅😅😅
 
Lingekuwa la mumewe angelitumia freely na kuligonga pia kisha anapiga simu tu beby nimegonga pikipiki huku njoo unisaidie😅😅😅
Hahahahhahahhah unanuna unaenda kutengeneza na maisha yanaendelea
Wanawake wa hivo ndo wanafanya mabachela wazidi kuwepo
 
Sasa ww unataka hizo kero zake azitolee mbinguni?? Eti social media kwani watu walioko huku kwwnye social media ndio hao hao waliopo huko mtaani ambapo angewafuata huko mtaani.
Acha kuwa na mawazo kama ya mtu aliyezaliwa kipindi cha Nyerere.
Tena hapa ndio pazuri maana identity ni anonymous hamna trace zitabaki wala kusambaa kwa story mtaani kama ambavyo ungeamua kumsimulia kinyozi wako au dada pale grocery unapokunywa!
 
Mimi nisingegusa hiyo gari. Halafu ndani mkishaanza hiki kanunua mke ni chake basi ndoa si imara tena.
Mke wa namna hio ni kujipanga mapema tu kununua shamba mahali huko na kuanza ujenzi mpya kimya kimya😎 tuwe makini sana na wanawake wetu hawa! Mko family ila gari ni lake hataki uguse kumaniner sio kwa mpare mimi.

Mke mbinafsi atakusumbua wewe na atawafarakanisha ndugu zako na wewe sababu ya kiroho cha choyo!
 
Ushamba tu ndo inamsumbua mkeo, yaani mpaka sasa kuna watu wanaringia gari tena suzuki, aiseee

Kuwa makini na mkeo fanya yako na jaribu kukaa hata miaka miwili hujagusa hiyo gari lake.
 
Lakini hili ni tatizo la jamii nzima hasa Tanzania wanawake hawana maamuzi kwenye mapenzi ndio maana hawawezi kutongoza mwanaume anayemtaka pia wanawake wanafundishwa kumpenda mtu mwenye kitu ndio maana sio ajabu kusikia mama anamkataza binti yake kuwa na mtu kwa sababu hana kitu "atakupa nini yule" kwaiyo hii madhara yake ni makubwa kwenye maisha ya ndoa kama anayokutana nayo mleta uzi
Very true wazazi ndo wanaharibu mahusiano ya mabinti zao...hataki mkwe masikini means haangalii upendo daah[emoji848]
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi

Mkuu ndio maana huku ni tofauti na mitandao mingine,ulishajiuliza kwanini watu wanapenda JF na kutumia fake id..
Zinasaidia sana watu wanakuwa free kupata ushauri na mawazo mapya.
 
Nimejikuta nawachukia sana watu wanaotoa siri za wapenzi wao hadharani, hivi unadhani nani anajali? inatusaidia nini>? Jifunze kumheshimu mke au mume wako, social media kamwe haiwezi kukusaidia matatizo yako zaidi utaishia kupata majanga zaidi
Kwa teknolojia ilipofikia sasa,forums kama JF zimekuwa msaada kwa watu wengi sana,ni njia rahisi ya kuweza kuwasiliana na watu wengi zaidi kuliko hata jinsi ambavyo unge share na ndugu.Hatukatai kuwa kuna ushauri mwingine wa kupotosha,lakini kama lengo ni kupata ufumbuzi huwezi kutoka bila ya kupata msaada wenye kujenga.Ikumbukwe hakuna anayemjua mwenzake ndio maana tunatumia hiden IDs ili mambo yaweze kuwa rahisi zaidi...
 
Aisee umenifurahisha sana kumbe tuko wengi kwenye hii kadhia 😂😂😂😂😂😂

Mimi mke wangu nimemfundisha gari mwenyewe alikua hajui a wala be mpaka amekua dereva na leseni nikamtafutia. Ni zaidi ya miaka mi 5 sasa tangu aanze kuendesha gari. Katika kipindi chote hicho, yeye ameshagonga gari, kukwangua, kupasua taa, vioo, kugonga miti, mageti, nk mara zisizohesabika. Mimi sijawahi kugonga hata inzi!

Cha ajabu sasa nikiwa naendesha mimi utasikia "eh, punguza mwendo bana unakimbia sana" (hapo niko speed 30), "ongeza mwendo, we huoni hilo semetrela nyuma..? Au paki kwanza lipite!", "hii kona umekatia mbali sana", "unaona hiyo gari mbele, unaona..?", "washa indiketa tunaingia pale...", "mpigie honi huyo bodaboda utamvaa", "washa full bana mimi sioni mbele..", "mbona umeovatekia karibu hivyo?"... yaani mi hua saa nyingine naishia kucheka tuu..🤣🤣🤣🤣
Ha ha ha huyo ni psychopath
 
Back
Top Bottom