Mke wangu kaacha ndoa yake kisa kazi

Nilimuambia avumilie kidogo,,,nitamfungulia BIASHARA,,,,ila yeye ana tamaa ya haraka,,, afu kibaya Zaidi...anayemtafutia kazi Mme wa mtu,,,NYUMBA ya Jirani wakati MKE wake hajui chochote
Wanakulana hao, mwambie mke wa jamaa na nyie mpeane. Usiponiheshimu sikuheshimu, ukinivurugia ndoa yangu nakuvurugia yako pia.
 
Huu ushauri wako umempa huyu ambaye miaka mitano hana uwezo wa kutafuta kibarua kwa mke wake wa ndoa, wala hawezi kumpa mtaji. Mimi hata hela sina ila ndani ya miezi mitatu naweza mpatia mpenzi wangu kazi, sembuse mke kwa miaka mitano nishindwe.

Ndio huyu mtu unamwambia apeleke mtoto nyumbani atafute msaidizi? Eti apangishe nyumba yake atafute ndogo apange. Kwa hela ipi. We unahisi kwanini mke wake alihangaika kutafuta kazi.

We ukimsoma malalamiko yake hapa unaona hii IQ aliyotumia hapa ni ya kijana aliyejenga na anayeweza mudu gharama za mfanyakazi wa kulea mtoto?
 
Kwa hiyo alifanya kusudi kutomtafutia mke kazi ?
 
Sasa kilichomkimbiza ni nini hasa?Kama alikua na nia njema si angesema tu huyo ni flani,nilimuomba anitaft
 
Umewahi kuona wapi mwanamke anajielewa akakimbia na kumuacha mume na mtoto wa 2yrs? Binafsi sijawahi kuona, mwanamke ataondoka na mtoto no matter what, kwanza sisi wanaume na malezi ya siku kwa siku wapi na wapi!

I feel for the guy ila maamuzi magumu yanahitajika, nasoma hapo eti mama anaamua kulala chini ili tu asimpe jamaa tunda.

Hapo hakuna mke wa kutengeneza nae maisha
 
Kwa uzoefu wangu huwa ndoa haziitaji ushauri toka kwa mtu hapo ni wewe mwenyewe ufuate vile moyo wako unataka.

Mana waeza shauriwa sivyo kesho na kesho kutwa mkayazungumza akarudi hapo wale waliokushauri ndo wanapokosa pa kuweka sura zao.
 
Lea mwanao huyo ndio damu yako hatakuacha mpaka kifo n beyond
Jibu la kikomavu sana hili.

Maana kwenye masuala ya ndoa, 'washauri' hamtakiwi kushauri kuivunja bali kuiunganisha.

Maamuzi madhubuti ni ya wanandoa wenyewe na wa kuivunja ndoa ni mahakama.

Ingawa kwa wazoefu wa hizi mambo, hapo hakuna ndoa.
 
Haya mambo huwa yanaanzia mwanzo pale mnapoanza mahusiano yenu na mwishowe huwa yanajijenga, waeza kuta we mwenyewe humshirikishi mkeo kwenye vitu vyako unafikiri naye akiwa na vya kwake atakushirikisha kweli?
 
Nimempa ushauri kulingana alivyojieleza coz hajaweka financial status yake na hajasema kama anaishi kwake au nyumba za kupanga na ndo maana nikampa option achague atakayoweza yeye. Oa ndo ujue maisha hizo ya kumpa gf wako zitakosa cku moja ndugu yangu T14 Armata
 
Dahh sema mambo ya ndoa bana, huwezi jua huko ndani kuna shida gani inayopelekea mke kuwa vile! Mwanamke hawezi kumzalia mtu halafu aje awe vile! Amegeuka kitu kingine sababu ipo! Huwezi tu kuamka asubuhi humtaki mme/mke wako! Mambo ni mengi sana hapo katikati!
 
Kizazi hiki kinapitia misukosuko mingi ya kimahusiano kwa sababu kimejiondoa kwenye utamaduni wa maisha waliyopitia wazee wetu ambao ulikuwa bora sana wakati wote.

Kuacha kuwashirikisha wakubwa zetu kututafutia wenza kutoka kwenye asili zetu,leo wa Musoma anaoa Lindi wa Lindi anaoa Iringa wa Iringa anaoa Mbeya alimradi vurugu huu mchanganyiko kusonga mbele ni vigumu kwa sababu hujui unakooa wana kiburi kiasi gani tofauti na baba au mjomba angekutafutia mke nyumba ya jirani kule kwenu nyumba anayoifahamu vizuri.
 
📌
 
Nilimuambia avumilie kidogo,,,nitamfungulia BIASHARA,,,,ila yeye ana tamaa ya haraka,,, afu kibaya Zaidi...anayemtafutia kazi Mme wa mtu,,,NYUMBA ya Jirani wakati MKE wake hajui chochote
Kwa life style na uchumi wa sasa ni % chache sana ya wanaume wanaweza kutimiza mahitaji yote ipasavyo.
Kwa hiyo miaka mitano am sure ungekua na nia au uwezo wa kumfungulia biashara ungekua ungekua ushafanya hivo.
Kaona hauwezi ndo maana anaamua kutafuta kazi bado unamuwekea vikwazo 😳 wanaume zama zimebadilika em na nyie badililikeni hamna mtu asopenda vitu vizuri jamani!
 
🥰
 
Lea mtt wako, aliyeondoka sio damu Yako kwa ufupi
 
Sasa kilichomkimbiza ni nini hasa?Kama alikua na nia njema si angesema tu huyo ni flani,nilimuomba anitaft
Wanawake ndivyo wlivyo ndugu yetu! Malizeni mambo yenu taratibu tu..!
 
Yaani mkuu nna uhakika wa 100% hiki ndo kimetokea!
Mwanaume anaona mradi kannua dona na dagaa ndani basi kamaliza,ukae upauke aanze kusema mke wangu hajipendi akatafute mchepuko 🤣🤣🤣
We need to do better kama wazazi kubadili hii mentality ya watoto wa kiume sasa,la sivo wataishi maisha magumu sana miaka ijayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…