Unaanzaje kumuita mgeni wako "lijitu"? Maadili ya mTz yanaanza kupotea polepole.
Sijaona popote mtu kakukemea juu ya uropokaji wako huo, inamaana wanakusapoti!
Hivi msayansi wa mambo unayoshuku, anaweza kujianika hivyo hadi ukahisi?
Nadhani wife wako ni mtu na nidhamu zake.
Watu huwa wanawekewa pazia usoni na asione, ubaradhuri unafanyika mbele yake.
Wenziyo mambo hayo huyafanya kwa mtindo wa kucheza "game" na wakifunga wanafurahi. Wanaona raha sana kuucheza huo mchezo na wewe ukiwepo. Ukiwa umetoka, wanapumzika hawaufanyi, bali hukusubiri ukiwepo.
Unatengewa chakula, ukianza kula tu, ndo muda mzuri wa kukuvunjia heshima na hauwezi kuhisi, Ama kama ni nje kidogo, hachepuki hadi utaporejea nyumbani ,unaagwa kabisa, kukujengea imani. Unawekewa pazia kwa kutumia common sense za kawaida tu na hauwezi kuhisi lolote.
Nilichotaka kusema ni kwamba, mbaya wako hawezi kuijonesha kama anavojenga mazoea mgeni wako, hata siku moja nakwambia.
Acha kuhisihisi wageni na kuwaita majina ya ajabuajabu eti lijitu.
Udhaifu huo ukiendelea nao, ipo siku utakuja kuchapiwa na mtu unayemwanini na kumuona ni legelege, lofa mchunga ng'ombe.