Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Usicheze na mijitu ya mikoani hapo ukizubaa tu na kama ulikuwa unapiga kamoja ndo basi tena.
 
Ninaamshukuru mungu kwani ni Binamu yako na sio Binamu wa mkeo.
 
kitu cha ajabu ni kwamba, unaruhusu mtu mzima aje kuishi nyumbani kwako, hilo kosa huwa silifanyi na sitakuja kulifanya, na nikilifanya huyo anayekaa kwangu lazima nimuweke chini nimpe vigezo na masharti ya kuishi pale ndani, hata kama kwa mwezi mmoja lazima atimize vigezo na masharti ili aondoke tukiwa rafiki. la sivyo, na kama ni mfanya kazi aende akapange guest ili tusivunjiane heshima. kitendo tu cha mtu mzima kuja kuishi au kufikia kwako kinaonyesha hana heshima huyo hivyo unaweza kumfukuza tu hana umuhimu huyo. binafsi kwamfano mimi nikisafiri sehemu, hata kwa dadangu tu hata awe na nyumba kubwa namna gani siwezi fikia. nitakosa uhuru halafu tunawezavunjiana heshima, kulinda heshima yangu huwa sifanyi hilo kosa, sasa yeye kama mtu mzima na hajiongezi namna hiyo ujue huyo hana umuhimu kwako na hana faida kwasababu uelewa au akili yake ndogo, fukuza tu hilo halitaelewa kama limefukuzwa halina akili. au mkanye.
 
tajiri! kuwa na amani na wageni! Huwa hawafanani! Humdhaniaye ndiye huwa siye
 
Huyu atagonga mkeo na mdogo wake mke wako watajijua wote wamegongwa na jamaa na hawatakuwa na shida wataendelea kugongwa kila mtu na muda wake..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ni lijitu au binadamu punguza chuki kujaa kifuan kwanza lol
 
ha hahahahaha kwanza hilo jitu lisipomgonga wife wako basi wengine wenye mwonekano wa hilo jitu watamla, fanya mazoezi ya kutafuta pesa kwa bidiii zaidi achana na likifua ila piga mazoezi kishikaji usipate magonjwa....

hilo lijitu liambie liache mazoea na wife hawa tunawaita wazee wa kutengeneza mazingira anaweza kuwagonga wote wa kike humo ndani kiutani utani tu kuwa makini... huwa hawatongozi yani ..

kama unaweza liambie hilo jitu lisepe tu mazoea hutaki jitu kubwa
Yoo look very experienced miss Chagga
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].....[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119].....
 
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.

Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.

Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.

Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.


Kwa hayo Macare kwa Mke wako huna lako.. Utakuja Kutupa Mrejesho...
 
Back
Top Bottom