Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.

Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.

Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.

Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.


Nahisi huyu ni mume mwenzio, ulikuwa tu hujuwi mchezo uko vipi. Haiwezekani mwanaume na akili zake avue nguo zake abakie na chupi tu akifua nguo zake na mke wa mtu mwingine. Kama ulichelewa, huenda ulishaliwa tayari na pengine jamaa anakusanifu tu.
 
binamu mbona mm sikua na nia mbaya mm nilimuelewa tu mdogo wa mkeo

kama vp ngoja nimalize na wife wako ili uwe unanilaumu ki haki
 
Ndo shida ya wanaume wa dar..!! sasa wew kifua tu kimekutisha., hadi unaliacha linakutawala kiasi icho.. linakoelekea litakufukuza sasa hapo ndani na huo mkitambi wako...!!
Ni suala la muda tu mkuu
 
Nyumba ni yako alafu mgeni akupande kichwani!!! Unashindwa nini kumuita kando na kumwambia avae nguo!?
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] wanaume wengine shida
 
Unamuonea wivu mdogo wake mkeo. Boss wewe ni hatari. Jokes!!

Mimi naona huyo jamaa amepata treatment nzuri sana ambayo labda hajawahi kupata katika maisha yake, mfn mazingira ya hapo home, upendo, vyakula, nidhamu, townlife, kuthaminiwa, uhuru nk. Sasa hivi vitu ni kama vinamfanya arudhishe fadhila, ama niseme kucompensate ili aonekane ni mtu wa faida, ndio maana utamuona ana give back upendo, anatamani afue, apike, aoshe vyombo nk. Hii yote ili asionekane mzigo hapo home na pia aonekane si lelemama. Ni wanaume wa mkoani hua wapo hivyo boss.

Pia nahisi mke wako anakujali sana kukwambia upunguze kitambi uwe kama hilo lijitu, hii ni kwa afya yako, ila kwasababu tayari umeshamchukia lijitu, unaona km vile upo insulted. Kiuhalisia mkeo yupo sahihi sana, jivunie boss kua na mke anaependa ndugu wa kila aina, km mkeo angekua hovyo hayo yote unayoyasema kuhusu hilo lijitu yangefanyika kwa siri mno.
huu ushauri unaompa nadhani humtakii mema..yaani bro nyumba inaungua kabisa na wewe unamshauri mwenye nyumba achochee kuni?!!
 
Chezea vidume wa mikoani wanatengeneza sex body
Midume ya dar inabuluza vitambi tu nguvu za kiume zenyewe zimeuliwa na chips mayai ya kizungu na kachori
 
Kumbe yule Udakuztz Kule Instagram anatoaga story kujitagutia Followers.Story kama ilivyooo.
 
Binam.....
Hivi ndio mambo gani ya kuja kunianika huku jf....[emoji45] [emoji45]
Kama uliona nakukera, kwanini haukuniambia tukiwa nyumbani, kuliko kunileta huku mitandaoni..[emoji25] [emoji25]
Basi sawa.
Leo ukirudi toka kazini, hauto nikuta hapa nyumbani kwako. Na nikifika kijijini nitamueleza shanga ambae ni mama yako, kwa yote haya ulivyo nitendea
Acha misifa
 
Nilipoiona hii story Kule Insta.Udakuz tz ameidakaaj.Nilichekaaaa.Jamaa kwanza punguza hasira.Huyo Jamaa ananenepa wewe unakonda ndani ya nyumba yako mwenyewe.Ushauri.Weka Camera ya Kificho.Utapata jibu.Kuliko Kubunibuni.Utakuja gombana na ukoo Bure.Just do that.
 
Nahisi huyu ni mume mwenzio, ulikuwa tu hujuwi mchezo uko vipi. Haiwezekani mwanaume na akili zake avue nguo zake abakie na chupi tu akifua nguo zake na mke wa mtu mwingine. Kama ulichelewa, huenda ulishaliwa tayari na pengine jamaa anakusanifu tu.
Ushauri mbaya sana
.Je unataka wakauane??kuwa na Huruma.
 
Binam.....
Hivi ndio mambo gani ya kuja kunianika huku jf....[emoji45] [emoji45]
Kama uliona nakukera, kwanini haukuniambia tukiwa nyumbani, kuliko kunileta huku mitandaoni..[emoji25] [emoji25]
Basi sawa.
Leo ukirudi toka kazini, hauto nikuta hapa nyumbani kwako. Na nikifika kijijini nitamueleza shanga ambae ni mama yako, kwa yote haya ulivyo nitendea
[emoji3] [emoji3] [emoji3] amsha dudeeee
 
Back
Top Bottom