Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Acha kumtamani mdogo wa mke wako
Umeshaoa dada ake mdogo wake hupaswi kumuonea wivu
Jamaa akila its non of yur bisness
 
"Akili za kuambiwaaaaa, changanya na za kwako........"
 
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.

Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.

Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.

Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mkuu unaliogopa hilo jitu la miraba minne, lifukuze tuu kama linakukera
 
Hahaaaa. Hapo mrahis kuliwa ni shemeji yako na house girl, si ajabu ameshakula au ndio maandalizi.
Wanaume tukikutana na Ke tuna mbwembwe balaaa.
Hili ni fundisho, mgeni wa kiume akija kwako unamuachaje anaangalia TV na mkeo?
Yani nikifkiria story ya ili jitu napata hasira za kurudi tena kucomment.

Mijitu mingi ya mkoani akili zao zipo mikononi kwa ajili ya kilimo. Sasa ili jitu linaanzaje kushinda na boxer bila shati ugenini? Au ndio joto?
 
kitu cha ajabu ni kwamba, unaruhusu mtu mzima aje kuishi nyumbani kwako, hilo kosa huwa silifanyi na sitakuja kulifanya, na nikilifanya huyo anayekaa kwangu lazima nimuweke chini nimpe vigezo na masharti ya kuishi pale ndani, hata kama kwa mwezi mmoja lazima atimize vigezo na masharti ili aondoke tukiwa rafiki. la sivyo, na kama ni mfanya kazi aende akapange guest ili tusivunjiane heshima. kitendo tu cha mtu mzima kuja kuishi au kufikia kwako kinaonyesha hana heshima huyo hivyo unaweza kumfukuza tu hana umuhimu huyo. binafsi kwamfano mimi nikisafiri sehemu, hata kwa dadangu tu hata awe na nyumba kubwa namna gani siwezi fikia. nitakosa uhuru halafu tunawezavunjiana heshima, kulinda heshima yangu huwa sifanyi hilo kosa, sasa yeye kama mtu mzima na hajiongezi namna hiyo ujue huyo hana umuhimu kwako na hana faida kwasababu uelewa au akili yake ndogo, fukuza tu hilo halitaelewa kama limefukuzwa halina akili. au mkanye.
Yani kwa ufupi ilo jitu ni kulifukuza tu. Unaliita sebleni wakati ushakusanya nguo zake pamoja ili baada ya maongezi lisepe. Linaendaje beach mke wa mtu alafu mwenye mke hapewi taarifa?
 
inabidi nicheke tu ila umeandika kwa hisia sana! hilo jitu la ukweli sana linarudisha fadhila kama linafua lipo poa na mkeo ila ww uoga wako tu but be cautious ukute mkeo kadondoka tayari make a research first laasivyo kama huna uvumilivu mtimue aende zake
 
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.
Kikulacho kaka? Kikulacho, mwanaume yakishaanza machale kwenye boma lako hasa kwenye haya mambo ya mapenzi fanya hima, mwambie yeye na kifua chake na vyuma vyake aende au arudi alikotoka afanye hayo anayoyadandia hapo, wanaume tuko hivyo, hasa wale wasio na wake na makazi, tuko kama wanyama, usishangae jamaa ataanza kusikilizwa kuliko wewe, ghafla mambo yote unayofanyiwa wewe ataanza kufanyiwa yeye, wewe subiri tu, punde utasikia limebadilisha mawazo linaendelea kukaa likikupa sababu tele, tupa kule mkuu, those are red lights flashing in front of your eyes..usidharau hisia zako kabisa..heri awe adui kuliko kuleta tafrani hapo..
 
Huyu jamaa hajiamini tu ,kama mkewe ana mpango wa kumsaliti hata jamaa akiondoka wata-do tu
Yawezekana maana mkewe alikuwa akimwambia na wewe fanya mazoezi utoke kifua kama binamu yko ni hii ushaidi tosha kwamba mkewe anamkubali binamu kiaina alafu jamaa mtoa Uzi kasema yeye anakitambi kikubwa hahaha!!!! bado tu anang'ang'a macho!!!
 
Back
Top Bottom