Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.
Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?
Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?
Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?
Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?
Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.
Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.
Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?
Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.
I guessUtakua unampenda au unamla shemeji yako wewe, kwa nini unamuonea wivu? Hapa inaonyesha kabisa jamaa ana interest na mdogo wa mke wako ila wewe unataka ku justify kwa kumpa kesi ya kumtaka mkeo
[emoji28] [emoji28] [emoji28] tutabuni mbinu mpya sio ya kishamba kama Hilo lijitu mpaka jamaa anastukaha haha hapana usitake ninyimwe pesa
Naweza kukuunga mkono ila anachokodea tu huyu jamaa ni kukaa na boxer hadharan,,ila kila kitu anafanya sababu asionekane hawajibikiUnamuonea wivu mdogo wake mkeo. Boss wewe ni hatari. Jokes!!
Mimi naona huyo jamaa amepata treatment nzuri sana ambayo labda hajawahi kupata katika maisha yake, mfn mazingira ya hapo home, upendo, vyakula, nidhamu, townlife, kuthaminiwa, uhuru nk. Sasa hivi vitu ni kama vinamfanya arudhishe fadhila, ama niseme kucompensate ili aonekane ni mtu wa faida, ndio maana utamuona ana give back upendo, anatamani afue, apike, aoshe vyombo nk. Hii yote ili asionekane mzigo hapo home na pia aonekane si lelemama. Ni wanaume wa mkoani hua wapo hivyo boss.
Pia nahisi mke wako anakujali sana kukwambia upunguze kitambi uwe kama hilo lijitu, hii ni kwa afya yako, ila kwasababu tayari umeshamchukia lijitu, unaona km vile upo insulted. Kiuhalisia mkeo yupo sahihi sana, jivunie boss kua na mke anaependa ndugu wa kila aina, km mkeo angekua hovyo hayo yote unayoyasema kuhusu hilo lijitu yangefanyika kwa siri mno.