Huntsman,
Ni changamoto za maisha . Ila usiwaze wala kufikiria habari ya mchepuko. Tatizo haliwi solved na tatizo .
(1) Kina mama wana tabia ya kuongozwa na hormones na feelings . Ndio wiring yao ilivyo. Pengine kuna neno kali au aina ya huduma hukusema basi ameshaconclude kuwa humpendi. Kosa lake kubwa ni kusema hamna tatizo. Mkuu, kaa nae au toka nae mueleze umuhimu wa open communication, umuhimu wa kuambiana mmoja anapokea na effects za kutotoa ushirikiano kwenye maongezi
(2)Tambua kuwa tendo la ndoa kwa wanawake na wanaume linakuwa viewed differently. To most men its a biological /physocal neeed kwa mwanamke ni emotinal/ pychological need. Jinsi mnavyoendesha mipango yenu, maongezi yenu yanachangia kiasi kikubwa kuwa mwanamke kuenjoy au kukokuenjoy tendo zima. Mfano katika mipango yenu mawazo yake hayasikilizwi au humpi sababu kwa nini mawazo yake hayafai . Au kuna jambo anaomba na anajua lipo ndani ya uwezo wako na hulifanyi wala humwambii kwa nini hulifanyi au unapangaje. Kingine kama kuna mambo unatumia ubabe/ nguvu ili yafanyike ilhali yeye hajaridhika nayo. Simaanishi kila wakati ufanye anachokataka yeye, la hasha ila kujadiliana na kureason naye kwa nini unaamini hoja yako ina nguvu.
Kama mahusiano yenu ya nje hayana mvuto amini kabisa mwanamke hawezi kuwa na hamu na wewe . Akiwa nayo anajoforce. Utaingia kwenye mawazo mabaya kuwa anachepuka kumbe ana nyongo ya kutomjali , kutompenda, kutomshirikisha mambo ya watoto, fedha, mipango ya familia .
Ufanye nini: Kama unahisi hili ni moja ya tatizo, basi jenga desturi ya kuongea nae, kumshirikisha na kusikia mawazo yake (si lazima utekeleze bali mpe nafasi atoe mchango). Pia jenga desturi ya kuwa nae na kutoka kama wanandoa -sio kutoka na watoto bali nyie wawili. Sio msubiri kualikwa na watu kwenye shughuli zao bali nyie wawili
(3) Madabiliko ya mwili: Sijui umri wenu ila isije kuwa mkeo anasumbuliwa na hormonal imbalance inayepelekea kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kuwa na hasira. All in all vyote hivi havihitimishi yeye kukujibu vibaya , ila msamehe tu na rejea namba moja, ongea nae na mueleze madhara ya kutokuwa tayari kuongea na kueleza hisia zako.
Katika yote mwombe Mungu ili umoja wenu uzidi kuimarika , binadamu tu dhaifu ni kwa neema za Mungu tu tunaweza .