Mke wangu kanipa wakati mgumu

Mke wangu kanipa wakati mgumu

Nyamaiso

Senior Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
166
Reaction score
244
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeishi na mke wangu zaidi ya miaka 30, lakini nilihisi ana bwana wa pembeni, nikaanza kufanya uchunguzi, kweli nikafuma baadhi ya msg , ambaxo kwa tabia yake kwangu aliyonionesha kwa miaka hiyo tuliyoishi, niliona si kawaida.

Mbaya zaidi hizo msg alizokuwa anatuma kwa huyo bwana( siwezi kumwita hawara kwa sasa) ilikuwa ni kama yeye anataka mahusiano yaendelee, maana mwanaume alikuwa akimjibu kwa mkato tu.

Mke- kwema, kimya
Mume/ baada ya siku tano/- kwema nipo, sawa
Mke- mmm sawa hiyo vipi,
Mume/ safi
Mke — mvua tu

Baada ya wiki
Mume— mzima wewe
Mke—upo poa wewe
Kwema tu, hofu kwako,
Kimya jamani, naona umetupa jongoo na mti wake,
Jua kali tu ee utadhani limeshuka.

Mume, nipo , hujibu SMS zangu!
Mke— saa ngapi tena wewe ndio hujibu.
Mume—- hahahaa upo!

Mke— nipo kuzeeka tu ndio kumepamba moto.

Mume—- aaa baba ajambo

Mke—- yupo tu aliacha na kazi sasa hivi yupo tu nyumbani.,
Mume—/ poa

Mke tena baada ya wiki
Mke —Upo kaka, za uzima!

Mume— poa.

Baada ya kushindwa kuvumilia na kuepusha kuona maajabu zaidi, nimeamua kulileta hili hapa ili mnisaidie, mke wangu bado nampenda, lakini nataka nijue nini kinaendelea,

Swali je nimuulize au nivumilie kidogo.

Watoto tunao wanne na wana maisha yao.
 
Screenshot_20240520_183825.png
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeishi na mke wangu zaidi ya miaka 30, lakini nilihisi ana bwana wa pembeni, nikaanza kufanya uchunguzi, kweli nikafuma baadhi ya msg , ambaxo kwa tabia yake kwangu aliyonionesha kwa miaka hiyo tuliyoishi, niliona si kawaida...
I can figure it out uko around 50+, kuna umri ukifika hata mke achepuke it doesn't bother. Vipi watoto wote ua uhakika ni wako?

Anyway, mwambie tu kuwa umejua. Halafu usifanye kitu.
 
Kama una above 50 msamehe tu, hakuna jipya, wote wanaliwa Kaka. Utakuja kufa bure Kaka yangu.

Pia ukiona mwanaume hana interest hivyo, ujue mkeo anamchuna na hana time naye kabisa.

Wanawake wote wako hivyo hivyo, tunaomba Mungu tu uzima na tusipate magonjwa Kaka.
 
nimeishi na mke wangu zaidi ya miaka 30, lakini nilihisi ana bwana wa pembeni,
Samahani ndugu, kwa umri wako unaonekana ni mtu mzima na ulienda jandoni! Hii jamii forums huwa naichukulia ni kama mtaa au kijiji.

Itajengwa hoja kuwa hatufahamiani na tunatumia majina bandia lakini humo kuna watoto, wahuni, wavuta bangi, wanafunzi, watu wazima hovyo,wenye busara na hekima n.k (Ila huwezi kuwajua mpaka atoe majibu)

Swali: Je, upo tayari matatizo yako yote hata ya aibu mtaa mzima au kijiji uyafahamu??

Kwa umri wako umeshindwa kuwatafuta wakongwe wenzako mkakaa kikao na kujadili changamoto inayokukabili kwa utulivu mkubwa??

Hapa naona umewatangazia kijiji au mtaa! Vumilia majibu ya waliopoteza ndoa, waliokosa ajira, walevi, wavuta bangi, vichaa, wanafunzi, watoto, walioachwa n.k!

Nb: Ni mtazamo tu!
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeishi na mke wangu zaidi ya miaka 30, lakini nilihisi ana bwana wa pembeni, nikaanza kufanya uchunguzi, kweli nikafuma baadhi ya msg , ambaxo kwa tabia yake kwangu aliyonionesha kwa miaka hiyo tuliyoishi, niliona si kawaida.

Mbaya zaidi hizo msg alizokuwa anatuma kwa huyo bwana( siwezi kumwita hawara kwa sasa) ilikuwa ni kama yeye anataka mahusiano yaendelee, maana mwanaume alikuwa akimjibu kwa mkato tu.

Mke- kwema, kimya
Mume/ baada ya siku tano/- kwema nipo, sawa
Mke- mmm sawa hiyo vipi,
Mume/ safi
Mke — mvua tu

Baada ya wiki
Mume— mzima wewe
Mke—upo poa wewe
Kwema tu, hofu kwako,
Kimya jamani, naona umetupa jongoo na mti wake,
Jua kali tu ee utadhani limeshuka.

Mume, nipo , hujibu SMS zangu!
Mke— saa ngapi tena wewe ndio hujibu.
Mume—- hahahaa upo!

Mke— nipo kuzeeka tu ndio kumepamba moto.

Mume—- aaa baba ajambo

Mke—- yupo tu aliacha na kazi sasa hivi yupo tu nyumbani.,
Mume—/ poa

Mke tena baada ya wiki
Mke —Upo kaka, za uzima!

Mume— poa.

Baada ya kushindwa kuvumilia na kuepusha kuona maajabu zaidi, nimeamua kulileta hili hapa ili mnisaidie, mke wangu bado nampenda, lakini nataka nijue nini kinaendelea,

Swali je nimuulize au nivumilie kidogo.

Watoto tunao wanne na wana maisha yao.
Sasa si uvumilie mpaka upate uthibitisho? 🙂
 
Back
Top Bottom