- Thread starter
- #41
Da , kuwaita wazee wenzangu tena,?Samahani ndugu, kwa umri wako unaonekana ni mtu mzima na ulienda jandoni! Hii jamii forum huwa naichukulia ni kama mtaa au kijiji.
Itajengwa hoja kuwa hatufahamiani na tunatumia majina bandia lakini humo kuna watoto, wahuni, wavuta bangi, wanafunzi,watu wazima hovyo,wenye busara na hekima n.k (Ila huwezi kuwajua mpaka atoe majibu)
Swali: Je, upo tayari matatizo yako yote hata ya aibu mtaa mzima au kijiji uyafahamu??
Kwa umri wako umeshindwa kuwatafuta wakongwe wenzako mkakaa kikao na kujadili changamoto inayokukabili kwa utulivu mkubwa??
Hapa naona umewatangazia kijiji au mtaa! Vumilia majibu ya waliopoteza ndoa, waliokosa ajira, walevi, wavuta bangi, vichaa, wanafunzi, watoto, walioachwa n.k!
Nb: Ni mtazamo tu!
Sasa hapo si ndio nimetangaza mtaa mzima, bora hapa