Mke wangu kanipa wakati mgumu

Kwa maisha mliyoishi miaka 30, sioni shida kwenye hizo meseji.

Mawasiliano ya kawaida kabisa hayo, kama hayakupendezi ni vyema kumwambia ayasitishe muendelee kuishi kwa amani.
Nifah,ni kweli uyasemayolakini roho inauma , nakubaliana na wewe , lakini naona kama mahusiano yalikuwapo muda mrefu , nimeacha kazi miaka miwili iliyopita nikaanza kuona dalili za dharau hivi, ndio nikaanza uchunguzi na kukutana na hayo.

Nimepanga kumuuliza kesho.
 
Lakini upendo utsendelea tena ndugu yangu kuishi na mtu wa namna hii,
Kumbuka nimeishi naye miaka yote hiyo kumbe slikuwa na mambo yske,

Nasikia uchungu sana kama ni kweli alikuwa ni malaya, nashindwa hata kuongea naye vizuri,

Kila akiongea naona ni tapeli fulani,

Lakini swali langu lipo palepale , je nimuulize?
 
Hizi meseji ni za kawaida baba na wanawasiliana kama marafiki wakawaida tu.
 
Uttoh2020, kwa jinsi unaona hizo chart, kwa muono wako , je ni nzuri kwa Mume, au zinatia mashaka
 
Hizi meseji ni za kawaida baba na wanawasiliana kama marafiki wakawaida tu.
Tatizo hapo sioni message yoyote kama ni marafiki wa kawaida tu,

Maana kama ni urafiki , labda ningeona wanazungumzia kitu fulani, lakini naona ni kama mke wangu anataka kitu kwako
 
Tatizo hapo sioni message yoyote kama ni marafiki wa kawaida tu,

Maana kama ni urafiki , labda ningeona wanazungumzia kitu fulani, lakini naona ni kama mke wangu anataka kitu kwako
Hapo sasa ni kuwa ni marafiki walio zoeana na jamaa anaonekana hana haiba ya kutoka na mke wa mtu.

Ni wanawake wote au niseme wengi wanatabia kama za mkeo.
 
Wanaume kama nyie mtakufa maskini.

After 30yrs of living together ndio unajifanya kumfatilia?

Au umepata kigoli unamtafutia Sababu?

Au ni Stori ya kutunga hii.

Wewe ni Mzee ndugu yangu kua na heshima.
 
I can figure it out uko around 50+, kuna umri ukifika hata mke achepuke it doesn't bother. Vipi watoto wote ua uhakika ni wako?

Anyway, mwambie tu kuwa umejua. Halafu usifanye kitu.
Aisee, inahitaji moyo,
Je nimwambie hilo tu, au inatakiwa nijue zaidi kwa kumuhoji
Ni kama walikuwa na mahusiano ambayo kwa sasa hayako active, japo wakati wowote wanapasha kiporo...ni muhimu umuhoji akupe maelezo yasiyotia shaka kabisa maana ukinyamza sonona itakumaliza.
sawa ushauri mxuri sana, hilo la kupasha kiporo ndio linaniumiza, maana sitamwamini tena, ni maisha bila kuaminiana hayana maana
 
Wanaume kama nyie mtakufa maskini.

After 30yrs of living together ndio unajifanya kumfatilia?

Au umepata kigoli unamtafutia Sababu?

Au ni Stori ya kutunga hii.

Wewe ni Mzee ndugu yangu kua na heshima.
Kufuatilia mke sio kitu rahisi hivyo, nimesema kuna vitu ambavyo sio vya kawaida nimeviona toka kwake ndio nikaamua kufuatilia,

Na kweli nimegundua mambo kama hayo.

Lakini ndugu yangu kwa umri huu , halafu nione vitu kama hivi si ndio kufa mapema huku
 
Huyo mwanamke kwanza kabisa anakudharau.
Badala ya kusema umestaafu, anasema umeacha kazi upo tu nyumbani.
Ni hilo neno ndio ndio limeniudhi sana , kwa nini amwambie nimeacha kazi ni nipo tu nyumbani,
Inaamanisha kuwa kwangu nyumbani ni kama anamfamisha kuwa , hana nafasi vizuri tena kama zamani
 
😂😂😂😂 umetusahau backbenchers bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…