Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Mke wangu kapangiwa kazi Mkoani

Habarini wapendwa.

Wadau, Mke wangu kapata kazi Taasisi moja ya Kiserikali lakini Kapangiwa Mkoani (Shinyanga). Tupo na watoto wawili sasa, mmoja ni mdogo ananyonya (Mwaka mmoja).

Sasa nina changamoto moja,

Kwanza nimemshauri kwa kuwa ndio anaenda kwenye mazingira mapya asiende na watoto awaache, ila yeye anahisi hataweza bila watoto hasa huyu mdogo, hiki kitu kinaniumiza kichwa sababu hatujui ni lini taasisi yake itakubali kumhamishia hapa nilipo.

Wazoefu naomba mawazo yenu!

Ahsante:
Fimbo ya mbali haiui nyoka
 
Duh umenifurahisha sana mkuu,eti kama ndoa tulizo nazo sisi,sidhani kama ni kweli,nakushauri usiweke fikira na akili zako kwa mwanamke.


Siku ukigundua ayafanyayo utakufa kabimba ka ngi, usikute mkeo anachepuka kila siku huku wewe wajisifu una stable family


Acha kabisa
usijifariji, long distance relationship ni hatari kuliko chochote, ukiishi mbali na mke upendo huwa unapungua, pia hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza kuishi mwezi mmoja bila kudukuliwa. jiandae kwa magonjwa ya zinaa, kuchapiwa na kupungua upendo kwasababu wewe utapata mchepuko ukapunguzia upando huko na yeye atapata wa kumkuna atapunguzia upendo huko. wazungu wanalijua sana hili ndio maana huwa hawaruhusu.
 
Mbona sioni shida hapo mkuu au Kuna kingine hujasema hapo kipato kwa familia kinaongezeka baada ya miaka 3 anaweza kurejea kuja dar akiwa na kazi
Mkiwa pekee Kila mmoja atapata mda wa kutafakari upya na kuona umuhimu wa mwingine
 
Nipo nae hapa, tunataka kuingia raundi ya TATU[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Mbona sioni shida hapo mkuu au Kuna kingine hujasema hapo kipato kwa familia kinaongezeka baada ya miaka 3 anaweza kurejea kuja dar akiwa na kazi
Mkiwa pekee Kila mmoja atapata mda wa kutafakari upya na kuona umuhimu wa mwingine
Umesomeka Mkuu
 
Back
Top Bottom