Darmian
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 17,289
- 46,624
Hila hizi ndoa hizi..kudadadeki,mimi na hasira zangu naweza kumvunja mtoto wa mtu miguu..Nami mke wangu n mchafu na mvivu sana
Akiamka hatandiki kitanda Wala kukunja neti, haoshi vyombo Wala kufagia. Yeye akishaamka n kuoga na kuperuzi mtandaoni basi.
Mdogo angu wa kike ndo anafanya usafi na kupika chai. Akanunue vitafunwa, yeye kakaa kwenye kochi tu.
Mwenzio kuepuka kupata msongo. nimeamua kujifulia nguo zangu, kufua mashuka na neti.
Kufagia uwanja jioni kwani asbh naenda Job.
Wala sina ugomvi nae kabisa sasa. Akija mama ake ama wageni wa kukaa siku mbili tatu ndo ataamka asbh kufanya kazi.
Siku aliyekuwepo mama angu na mama ake nikatoa mashuka na nguo zangu kwenda kufua, akaniomba niziache atafua yeye. Nikamwambia mbele ya wazazi ntafua mwenyewe Kama navyofanyaga, lini yeye akanifulia?
Yaani siku zote hufanyi usafi ila wakija kina Mama ndo ujifanye unafanyaga?..nitakuzaba vibao,seriously..huu ni ujinga..
Japokuwa huwa siwazi kumpiga mtoto wa kike,ila kwa hili lazima nikunase vibao.