Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015, baada ya kuishi nae miaka kama 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani, nikamkuta mke wangu kak
Wote ni wachawi sema tu mwingine wa majini mwingine local ule wa kuroga.
Kwa sababu;
Mama alijuaje yaliyokukuta mpaka akakupa hiyo dawa?
Na wife uliporudi alijuaje umepewa dawa na badala yake naye akakupa.

Jamaa yangu,kimbilio lako ambalo ni salama ni kanisani tu tena kwa walokole pure.!
Ukienda kwa waganga utakua umewapeleka kwenye kikao cha usuluhishi na upatanisho ila sio kuyaondoa hayo madudu.
 
Hapo Wote ni Wachawi au Tayari Wameshatendeana ubaya si unajua Tena Mkwe na Mama Mkwe Hawapatanagi kwa Asilimia kubwa. Tafuta Solution kwa Wengine Maana Ukikubali dawa Ya Mmoja Wapo Ujue Utaharibu Ndoa Yako

Daaah Pole sana. Mtihani mgumu sana Huu hasa ukija Kuambiwa Mke au Mama Ni Mchawi au Wote Wawili ni Wachawi

By the Way kama Ulilelewa na Mama basi Kuna Vitu Utajua Tu
 
Tatizo nao wachungaji wenye uhakika siku hizi wameadimika. Kuwajua ni shida sana. Hilo tatizo ilikuwa uwakusanye wote pigeni maombi ya nguvu ya saa nzima,hata kabla jogoo hajawika kila kitu kingekuwa wazi kwa kila mmoja
 
Wagombanapo Mafahali wawili ziumiazo Nyasi.

Kwenye hii vita Mkuu wewe ni Nyasi, hapo cha kufanya ni aidha tafuta Mtaalamu wako ambaye hafungamani na upande wowote, yeye ndiye akupe ukweli Wa nani hasa ni mbaya kwako.

Otherwise Fanya Ibada sana ili M/Mungu ndiye akusaidie kuwakabili hao wachawi.
 
Wenda wote ni wachawi wamezidina kete kila mtu anatafta mbinu ya kutengeneza chuki kwa mwenzie. Kusema mama ako hawezi kukudhuru icho kitu ondoa akilini mwako, mchawi hana cha rafiki wala mtoto yeyote yule anaweza kumdhuru mda wake ukifika.

Hapo usimuamin mtu anza kujitengenezea kinga ya kupambana nao( kama ni kusali /kuswali ongeza bidii) had ujue ukweli .
 
~ Mama ni mchawi na mke ana maruhani (majini).
~ Mama umeishi nae miaka yote hiyo (sijui kama ulishawahi kuona jambo au ishara yoyote inayohusiana na uchawi juu yake), mke umeishi nae miaka 7 na hakuna tatizo.
Hapo nyumbani una (wa) mtoto na je hajawahi kupata tatizo lolote lililopelekea kuwa na medical complications au mkalazimika kumpeleka kwenye tiba mbadala? Kama hili halijawahi tokea na muda wote umekuwa ukiishi nao kwa amani, jua kuwa wao kama wao wanavita vya kiroho vya kimaslahi.
Chakufanya: mtafute mchungaji mweleze yote kama ulivyotuelezea sisi then upate uponyaji wa kiroho kupitia jina lipitalo majina yote, yaani jina la YESU KRISTO.
 
Back
Top Bottom