Mke wangu, Umetafuta adhabu umekosa hadi umeamua kuniadhibu hivi?

Mke wangu, Umetafuta adhabu umekosa hadi umeamua kuniadhibu hivi?

Mwanamke mpaka anamvulia nguo mwanaume tofauti na mumewe basi maana yake upendo wake wa dhati upo huko ndiyo maana akakuchukulia wewe kama option tu.

Yaani hata iweje kamwe usirudiane na mwanamke msaliti atakudharau kupitiliza halafu ukajuta zaidi ya sasa mkuu.
We jidanganye tu🤣 mwanamke hana maamuzi kwenye mapenz anaweza kumpa unyumba yeyote atakaye fanikiwa kumshawishi yani kuna jamaa hata mke wako awe anakupenda vipi ukimwachia nafasi lazima amegwe tu
 
Mtanzania2020 Unajua kuwa wewe ulikuwa mwanamke mwaka jana.

🤣🤣🤣 Hawa vijana wanatuonaje sijui.
 
Ila mke anauma hata km ni chai ila km ni kweli pole sana mke anauma na unaweza usikae sawa kwa mda
 
Mimi ni Mwl na nina miaka minne kazini niliajliriwa 2022. Nina mke ambae nilimuoa mwaka 2020 na nimebahatika kuzaa nae watoto wawili mmoja wa kiume miaka 4 na mwingine wa kike tarehe moja April anafikisha miaka miwili.

Kuna mkasa umeniumiza sana nimeamua kushare maumivu na wengine kwenye ukurasa wako angalau kwa comments za ushauri na na faraja inaweza nijenga nikawa mtu mwingine.

Iko hivi: mwezi December mke wangu aliomba aende kumsalimia mdogo wake ambae ameajiriwa mkoa naofanya kazi (Morogoro) ila Wilaya tofauti na nilipo mimi kidogo ni mbali

Basi nikampa nauli na kila kitu akaondoka na binti mdogo kwenda huko, kakaa siku zikaenda holiday hiyo sasa huwa ni utaratibu wa kumjulia hali mke wangu asubuhi saa 12 kabla ya kuamka na jioni saa 2 kabla ya kulala

Basi bana tarehe 23 Dec jioni nikamcheki shortly akadai alikuwa na kazi akaniomba apumzike hivyo basi tarehe 24 mapema kama kawaida nikamcheki asubuhi hakuwa anapatikana, basi usiku the same hakuwa anapatikana

Ikanibidi nimcheki shemeji ambae ni mdogo wake akanijibu kuwa hayuko poa amelala nikajipa moyo kesho nayo ni siku.

Tarehe 25 Dec asubuhi nikamcheki hakuwa anapatikana nikampigia shemeji tena akasema amewahi kuamka ameenda kuhemea sokoni. Kumbuka ni mgeni huko na nina siku mbili sijaongea nae basi nikamuomba akirudi tu anitafute, nikapiga tena simu mara kadhaa hakuna majibu nikapiga nikapiga tena holla!

Akaja kunitafuta saa 12 jioni na sababu kibao ambazo hazina mashiko aiseee nikawa sijaelewa ikanibidi nikae kimya nisubiri arudi nimuulize vizuri.

Baada ya siku kuwadia akarudi kimyakimya nikashitukia tu huyu hapa. Sikuhoji sana nikawa mpole kesho yake nikamtazama usoni wife lakini nikagundua kama uso hauna nuru sana nikamuuliza una shida gani maana kama ana wasiwasi sana aisee

Basi akajibu kuwa yuko sawa lakini nikaona mabadiliko muda wa kula kuna namna anajilazimisha kula naona kabisa kuna jambo haliko sawa nikahofia jambo maana mke wangu akibeba ujauzito ni aina ya wanawake wale ambao huwa wana ugua sana nikahisi hizo dalili ila nikapotezea.

Sasa ikaja shida kuwa ananihitaji sana kimwili kitu ambacho si kawaida sana kwake nikashituka nikasema sifanyi nae mpaka anipe maelezo ya zile siku za holiday imagine mpaka analia eti amemiss aisee nikashituka.

Nikaenda kuna zahanati karibu nikaomba kipimo kimyakimya bana. Huwa anaingia na kopo la kukojolea coz chumba hakina choo cha ndani aisee ikafika usiku sana nikaamka nikapima mkojo sasa mimi kwa kweli kipimo kikanichanganya

Ikabidi nimtumie mshikaji wangu kwa picha kunisaidia kusoma oyaaaa,jibu sasa likawa hongera mzee unaenda kuongeza familia japo bado ni mdogo kama week 3 au mwezi hivi, aisee moyo ukafanya shwaaaah! Nikajikaza asubuhi nikamuita nikamuuliza wife una ujauzito? Akawaka ujauzito wa wapi?

Toka lini? Na kiaje? Basi bana kumbuka kipindi anaenda kwa dada yake alikuwa MP na sodo nilimnunulia mwenyewe na huwa ni utaratibu wangu basi nikamuangalia sana nikajikuta nalia mwenyewe nikamuuliza mke wangu umetafuta adhabu zimekosa umeamua kuniadhibu hivi hata kama nilikukosea?

Aisee akaanza kulia nikamuuliza hajibu chochote. Nikamuomba simu nikapitia namba nikabahatika kukuta namba moja amewasiliana nae zaidi ya mara 40 ndani ya siku 3.

Nikamuuliza huyu ni nani akanijibu bhana anaitwa (jina kapuni) ndiye mwenye ujauzito huu na tulikutana tarehe 23 nilienda Dar sasa ulivyoshituka nikashindwa kurudi tarehe 24 sababu ya usafiri ikanibidi nirudi 25

Imagine kumbe zile siku zote alikuwa sehemu na mshikaji huku mimi nahangaika kumtafuta basi sawa yote tisa ila kumi mshikaji akamuacha na mimba na ambayo kama nisingeshituka tayari ilikuwa ya kwangu.

Najiuliza wanawake huwa mnahitaji nini mke wangu sio mtumishi ila kwa nafasi yangu nilijaribu kutimiza kile naweza kwake ila ikawa hivyo.

Mpaka natuma ujumbe huu nilikaa kimya week nzima akaniambia anaondoka coz ameshindwa kujisamehe hata yeye mwenyewe so akarudi kwa mdogo wake na hata sikujaribu kumzuia kabisa but ndani ya ile week nikiwa kimya

Alitoa ujauzito nikawa namuangalia tu anavyohangaika alivyokaa sawa kaondoka mpaka sasa yuko huko na aliniomba akae na watoto kwani ni wadogo watanisumbua sana wakikuwa watarudi nikae nao kwani kuwahudumia wangenipa shida nikamruhusu kama alivyotaka.

Mpaka sasa niko mwenyewe natafakari sipati picha wapi nilikosea aisee.

View attachment 3561600
Huyo jamaa atakuwa ni ex wake walisoma wote secondary au chuo
 
Back
Top Bottom