Mke wangu wa kwanza baada kuona naingiza pesa nyingi alijazwa upepo tuaachane ili apate pesa kirahisi

Kila siku tunaimba na kauli mbiu yetu ya kimalaika kataa kuoa kataa kuishi na Mwanamke kindoa au kinyumba
 
Sasa una solve financial issues . Akitokewa na rich guy akampa pesa ataliwa na Kuleta magonjwa ndani . Abit pointless . She will go after money soon or later
 
Siku dada zako wakiwa mashangazi ndio utajua chanzo ni nini
Na hivi viswahili vitarafa vyenu, vinaua sana maneno yenye heshima na kuyafanya yakose maana.

Shangazi (dadake baba) tulivyomnyenyekea na kumheshimu zamani, sasa 'Mashangazi' linatumika mbadala wa 'mashangingi'!

Shangazi Og tumwiteje kwa jina lenye hadhi yake?
 
Nimesoma na nimemuelewa,ila Maamuzi ya kugawana Mali "Matrimonial Properties,Au matrimonial Assets and liabilities" yanategenea na Vitu vingi sana..

Cha kwanza mi kuwa Ndoa Yake ilikuwa Halali (Legally)au ni "presumption of Marriage (Njoo tukae)"?

Cha pili kama ndoa ilikuwa halali Talaka ilitolewa na mahakama,Kama ndiyo ana hati ya Talaka?

Kama hana hati ya Talaka na talaka alitoa yeye na sio mahakama bado yupo kwenye vita kubwa mara Baada ya yeye kufariki..
Mke wake huyo wa kwanza atakuwa na haki ya kutaka mali na kudai mali hizo ni zake..

'Cuz mkristo haruhusiwi kuoa wake wawili ,So kama mahakama bado inatambua Ndoa hiyo itachukua only the first marriage ndo ndoa ya Kweli na hii ya pili itatupiliwa mbali..

Kwahyo mke wa pili hata akichuma Nini, Kama mke wa kwanza hakupewa Hati ya talaka na mahakama na Nyinyi ni wakristo "Basi bado kazi unayo"...

Sasa turudi kwa mke wa pili..
Bado swali ni lile lile amemuoa kama kamuoa Amehakikisha Yule mke wa kwanza kampa talaka ya "kimahakama" maana kama hajafanya hivyo ndoa hii ni batili...

MLA (Marriage Law Act) ina Prohibit subsisting marriage..
Ukisoma Kifungu cha 15 kifungu kidogo cha 1

15.(1) No man, while married by a monogamous marriage, shall contract another marriage.

Kuna Hukumu zipo anaweza akafatilia Hukumu kati ya "Violet Ishengoma Kahangwa and Jovin Mutabuzï v. thedministrator General and Mrs. Eudokia Hakangwa (1990) TLR 72....

Turudi kugawana mali "Matrimonial Properties"..
Ambayo imeelezewa kuanzia kifungu Cha 56 cha sheria hiyo mpaka kifungu cha 68...

Kama mwanamke hakuzitafuta mali ,Hakushiriki kutafuta mali, Hakuwepo kwenye utafutaji wa mali hawezi kurithi kitu chochote..

Unless kama alikuwa anakupa Mawazo kuhusu Kutafuta,Anakuliwaza unapotoka kwenye mahangaikp,Au unapika na unakula unapata nguvu ya kutafuta..

Na ikumbukwe kwamba hii inaenda kwa pande mbili sio moja...

Na ikumbukwe kugawana mali sio jambo rahisi hivyo..

section 114 (1) of the LMA inatupa mwanga kuwa.
"the assets envisaged thereat must firstly be matrimonial assets/ and secondly, they must have been acquired by them during the marriage by their joint efforts"

Usisahau sio mali tu hata madeni pia itabidi wagawane 50/50


Lakini hata hivyo kama ukinunua Nyumba kwa pesa yako na ukaiandika Jina lako wewe bila kushirikisha jina la mke hiyo mali itakuwa ya kwako na wala sio ya mke..According to LMA section 60..


Pia unaweza ukatafuta "Matrimonial Appeal No. 5 of 2014 kati ya MARCEL KICHUMISA (APPELLANT) VERSUS MARY VENANT KABIRIGI (Appeal from the decision of the High Court of Tanzania at Mwanza) kutoka kwenye case ya Primary Court in Matrimonial Cause No. 43 of 2013 seeking to be granted a divorce decree and division of matrimonial properties."

Uncle bright
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…