Hii ngoma bado haijavuja au safari hii wamekuwa makini kuliko miaka ya nyuma ambapo majedwali ya viwango vipya vya mishahara na makato kama PAYE huvuja?
Mara nyongeza ni shilingi 10,000 au 20,000 kwa wale ambao mishahara yao sio kima cha chini. Mtalia tena watumishi kama mlivyolia 2022.
Wewe kwani kuna aliyekutangazia makato kwenye simu yalipoongezeka.
Kuna makato makubwa yameongezeka ukituma na kupokea na kutoa pesa.
Yaani ni balaa .
Hayo makampuni yamekua ni makampuni ya kinyonyaji sana lakini hakuna anayejali.
Kazi ya serikali sio kutisha watu wanaokosoa au kupinga ili wananchi waiogope na kuinyanyenyekea kama Mungu.
Serikali kazi yake kubwa ni kulinda uchumi wa serikali na watu wake dhidi ya wanyonyaji .
Leo hii pamoja na watawala kulipwa fedha nyingi na marupurupu kibao lakini wamegeuka kuwa Wezi wakishirikiana na wanyonyaji kuwaibia wananchi na kuua mashirika ya umma .
Yaani leo hii Mabwanyenye ya kizanzibar yanaua kabisa uchumi wa Tanganyika kuneemesha waarabu na Wazanzibar wachache .
Nyie Wazanzibari mnataka watoto wetu baadae waishi kama wakimbikzi na watumwa kwenye nchi yao waliyopewa na Mungu ? Mnaona wakenya waliokumbatia sera na mifumo ya kinyonyaji jinsi watoto wao leo wanavyohangaika kwa kukosa ajira huku watu wachache wakiwemo familia za watawala na wazungu na waarabu nawasomalia na wahindi wakihodhi mali na uchumi wa Kenya na Vijana wa Kenya mamilion sasa wanarandaranda mitaani na kuandamana huku wakiharibu miundo Mbinu ? Hicho ndicho wazanzibari walioshika dola wanachotaka kutuachia miaka 20 ijayo katika nchi yetu na wao kumiliki mahoteli na majumba Zanzibar na Dubai na maviwanda ya mikate na vituo vya kuuza gesi Tanganyika ?
Kwa nini hamjali maisha ya watu wa chini wakati ndio wengi wanaopiga kura ? Au dharau yote ni kwa sababu mbaiba kura na hamtegemei kura zao ?
Yaani TTCL inaachwa ijifie tu wakati ni kampuni ya umma inayotoa gawia na kupokea Ruzuku na ukweli ni kwamba inapata faida .
TANESCO inayoingiza mabilioni kila Dakika katika uchumi wa kidigitali leo eti haipati faida wakati mpaka vijijini watu wananunua umeme kuchaji simu ,soko la kuchomelea vyuma ni kubwa kila mahali . Mashinde za compressor zipo kila mahali ,viwanda vimeongezeka na mahoteli na nyumba zenye umeme kila mahali . Ukiangalia Luku inayonunuliwa kwa siku ni nyingi tena kwa keshi lakini wanatupa takwimu za uongo kama miaka ile ya kusoma mita kianalogia na watu kujiunganishia umeme kinyemela na kutumia bila kulipa ?
Mikopo imeongezeka lakni bado mnaacha wananchi wananyonywa na mabeberu .
Mwendo Kasi mwaka wa uchaguzi ndio unafanya vibaya kwa makusudi kwa sababu tu Samia hana mtu wa kumpinga ndani ya chama na nje ya Chama . Kikwete ,Mwigulu ,Biteko ,Bashe na Samia wanaona ni sawa maana wao hata wakiambiwa walipie pumzi kwa mita watalipa kwao pesa sio shida .