Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, baada ya kupima mkojo wa Wema Sepetu walibaini una bangi.
SHAHIDI wa kwanza, Mkemia Elias Mulima (40), katika kesi inayomkabili Wema Sepetu na wenzake, amedai mahakamani kuwa mshtakiwa huyo alifikishwa ofisini kwake akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi na baada ya kutoa sampuli ya mkojo wake, vipimo vilionyesha ni mtumiaji wa bangi.
Hatua hiyo ilizua mabishano ya kisheria baadaye.
Aidha, shahidi huyo alidai alipokea sampuli ya majani na baada ya kufanya vipimo alibaini kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi.
Shahidi huyo alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kalula.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ya wakili Kalula na shahidi:
Wakili: Shahidi unakumbuka Februari 6, mwaka huu ulikuwa wapi?
Shahidi: Nilikuwa ofisini.
Wakili: Je, siku hiyo nini kilitokea?
Shahidi: Siku hiyo nilipokea kielelezo kutoka jeshi la polisi kama sehemu ya majukumu yangu ya kazi.
Wakili: Ulipokea kutoka kwa nani?
Shahidi: Nilipokea kutoka kwa Koplo Robart.
Wakili: Je, kielelezo hicho kilikuwa kinahusu nini?
Shahidi: Kielelezo hicho kilikua sampuli ya misokoto idhaniwayo kuwa dawa za kulevya aina ya bangi ambacho kililetwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kuthibitisha kuwa ni dawa za kulevya au la.
Wakili: Nini kilifuata?
Shahidi: Nilipima uzito wa yale majani nikapata gramu 1.08, nilianza kufanyia uchunguzi wa awali kwa kuchanganya na dawa maalumu na majibu yalikuwa ni bangi. Nilifanya kipimo cha pili kupitia mitambo maalumu majibu yakaonyesha kuwa ni bangi.
Wakili: Shahidi, wewe kama mkemia bangi ina madhara gani kwa binadamu?
Shahidi: Bangi inasababisha mtumiaji kupata ulevi ambao hauwezi kutibika na husababisha mtumiaji kuharibikiwa akili.
Wakili: Shahidi iambie mahakama Februari 8, mwaka huu unakumbuka nini?
Shahidi: Nakumbuka niliandaa taarifa kuhusiana na uchunguzi wa sampuli ya dawa zidhaniwazo kuwa za kulevya aina ya bangi na majibu yalitoa kuwa majani yale ni bangi.
Wakili: Je, unakumbuka tukio gani jingine kutokea siku hiyo?
Shahidi: Nilipokea sampuli nyingine ya mkojo wa Wema Sepetu, ambaye aliletwa ofisini kwangu akiwa chini ya ulinzi wa Inspekta Willy na askari mwanamke, Marry.
“Nilimpa kontena maalumu na akiwa chini ya ulinzi wa Marry alikwenda kutoa mkojo na nilipoufanyia vipimo majibu yalionyesha kuwa na dawa za kulevya aina ya bangi” alidai shahidi huyo.
Shahidi alidai kuwa baada ya kumaliza kufanya vipimo aliandaa taarifa, kuiweka sahihi na ilihakikiwa na Kaimu Mkemia Mkuu.
Akifafanua zaidi alidai kuwa bangi inaonekana kwenye mkojo ikikaa muda wa siku 28.
Shahidi huyo aliomba mahakama kupokea taarifa zake mbili za uchunguzi wa bangi na mkojo.
Hata hivyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala alipinga mahakama kupokea taarifa hiyo kama kielelezo katika kesi hiyo kwa sababu ilikuwa na mapungufu ya kisheria.
Kibatala alidai kuwa taarifa hiyo haijakidhi matakwa ya kisheria kwa uchunguzi wa mtu aliyeko chini ya ulinzi kwamba ni lazima akaape mbele ya hakimu.
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulidai kuwa taarifa hiyo iko sahihi kisheria na kwamba mahakama itupilie mbali pingamizi la utetezi.
Hakimu Simba alisema baada ya kusikiliza hoja za pande zoe mbili mahakama yake itatoa uamuzi keshokutwa.
Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni wafanyakazi wake Angelina Msigwa na Matrida Abas.
Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa Februari 4, mwaka huu eneo la Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Katika Shitaka la pili, katika tarehe tofauti kati ya Februari Mosi na 3, mwaka huu, mahali pasipojulikana, jijini Dar es Salaam, Wema alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.
Washtakiwa walikana mashitaka na waliposomewa maelezo ya awali walikiri anuani zao na majina tu.
Chanzo: Nipashe
Huyu shaidi Mkemia anapaswa kwenda shule tena maana hajui upande mwingine wa matumizi ya bhangi kama dawa ya uponyaji kwa mwili wa binadamu. Yafuatayo ni mafao
While you might have heard many people say that weed can cause diseases, scientific researches and studies show that it can actually cure many diseases and physical problems. From helping fight
Glaucoma to controlling
epileptic seizures to helping
prevent cancer from spreading to
slowing Alzheimer’s to
easing multiple sclerosis pain to reducing
Hepatitis C side-effects to treating inflammatory bowels to
relieving arthritis pain to
helping you get through chemo to a lot more, scientific researches confirm the effectiveness of marijuana.
You might be wondering if medical marijuana has so many benefits, why isn’t it legal already? Well, the big pharmaceutical companies can crumble down if a naturally growing, dirt-cheap plant gets legal and starts curing diseases which can otherwise only be cured with their expensive medicines at this point. Despite all that, medical cannabis is becoming legal in most of the states very quick
Smoking weed isn’t actually that bad for your lungs, and smokers actually have improved lung function when compared to both cigarette smokers – and people who have never smoked either.
The researchers, writing in the Journal of the American Medical Association, say that the big drags taken by weed smokers may actually ‘train’ lungs to be more efficient.
We investigated the effects of cannabis smoked naturalistically on schizotypy and divergent thinking, a measure of creativity.
Smoking weed helps patients give up opiates such as heroin, a new study has found.
A study in the journal Obesity found that regular weed smokers are less likely to be obese than non-smokers.