Mkemia Mkuu: Mkojo wa Wema Sepetu ulikuwa na bangi

kituko,wanaokushitaki ndio wanaokupima na kutoa majibu wanayotaka ili wakutie hatiani..hii ina tofauti gani na kamati za makinikia tulizojundia wenyewe na kuwatuhumu wale wazungu?
 
Najaribu kuwaza labda aliingiliwa na mvuta bangi ambaye baada ya repture ....ikabaki manii yenye bang siku chache kabla ya kudakwa!!?
 
Doh nishajua kwanini Lissu alitakiwa kupima kojo! hahah kumbe Wema angeshtuka mara ya kwanza naye angegoma kupima mkojo??
 
Wakishavuta mibangi yao wanawaza kukaribishwa Ikulu. Magufuli kuwawekea 'boundary' tayari wanamuona hafai eti 'nazidi kumkumbuka JK'. [emoji28][emoji28][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doh nishajua kwanini Lissu alitakiwa kupima kojo! hahah kumbe Wema angeshtuka mara ya kwanza naye angegoma kupima mkojo??

Hata kama Wema anavuta na mkojo ulikuwa na bangi sijaona bado kesi ya kujibu sababu ya mihemko ya Jeshi la Polisi.

Nilishasema Jeshi la Polisi ni wahuni na hawana weledi wa kufanya kazi zao,

Utampimaje mtu mkojo bila ya kibali cha mahakama halafu upeleke mkojo huo ukawe ushahidi mahakani?

Kama bangi inakaa kwenye mkojo siku 28 walikuwa na haraka gani ya kupima bila kibali cha mahakama?

Japokuwa ana vyeti vyake vya chuo kikuu lakini Sirro ni Zero brain, ameweka tamaa ya madaraka mbele mpaka kasahau wajibu wake kama POLISI.
 
Huyu inadaiwa kakutwa mkojo wake una chembechembe za bangi na msokoto mmoja chumbani kwake. Wamekomaa nae kwenye case. Mwingine ni teja sugu, kakiri kwamba analamba ngada mwanzo mwisho. Kasamehewa na sasa ati ni balozi wa kuokoa vijana, akiandamana na RC majukwaani.

Nchi hii ni pasua kichwa kwelikweli. Full visasi na kukomoana.
Wala siyo nchi ndiyo pasua kichwa, ni haya majitu yaliyopewa dhamana ya kazi yanaendekeza masilahi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi inayomkabili mrembo Wema Sepetu jana aliendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo shahidi namba moja kwa upande wa mashtaka alitoa ushahidi wake na kusema kuwa mkojo wa mrembo huyo ulionyesha kuwa alivuta bangi
Shahidi huyo, Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akiongozwa na wakili wa serikali Constantine Kakula aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba namna alivyompima mtuhumiwa huyo na kubaini kuwa mkojo wake ulikuwa na bangi ambapo sampuli ya mkojo huo aliipokea Februari 8.

Shahidi alisema baada ya Wema kutoa sampuli ya mkojo huo ilipelekwa maabara ambapo lengo lilikuwa ni kuchunguza chembechembe za uwepo wa dawa za kulevya na ndipo walipobaini uwepo wa dawa za kulevya aina ya bangi. Baada ya kutoa ushahidi huo, Elias alitoa taarifa ya uchunguzi aliyoiandaa na kuisaini yeye mwenyewe na pia kuthibitishwa na kaimu mkemia mkuu wa serikali ili itumike kama kielelezo cha ushahidi.

Baada ya hoja hizo, upande wa utetezi unaoongozwa na Wakili Peter Kibatala aliitaka mahakama kutopokea taarifa hiyo kwa sababu uchunguzi haukufuata sheria kwani Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai inataka uchunguzi wa kitabibu kwa mtuhumiwa ambaye yupo chini ya ulinzi lazima upate kibali cha mahakama.

Aidha alitaka pia mahakama isipokee taarifa hiyo kwa sababu haikumbatanaishwa na fomu namba DCEA 001.

Akijibu hoja hizo, hakimu aliyekuwa mahakamani hapo alisema kuwa, fomu yenye namba 001 inatumiwa na Polisi wanaopeleka sampuli na fomu namba 009 ni taarifa ya mkemia, na kwamba fomu moja haitegemei nyingine kwa sababu huandaliwa na watu tofauti.

Hakimu pia aliipangua hoja ya Kibatala ya kibali cha mahakama ambapo alisema sheria haijasema kuwa wakati wote lazima Polisi waombe kibali hicho cha uchunguzi wa kitabibu, lakini pale ambapo mtuhumiwa atakuwa hayupo tayari, wanaweza kuomba kibali cha mahakama.

Kutokana na mvutano ulioibuka mahakamani hapo kuhusu taarifa hiyo ya uchunguzi, mahakama iliomba muda wa kupitia nyaraka hizo na kesi hiyo ikaahirishwa hadi Agosti 4 mwaka huu.

MY TAKE:
Hivi ule mchakamchaka ulikuwa kubaini wavuta bangi!!?au kulikuwa na visa kukomoa watu?Yaani hapa Tz kuna wangapi hawajawahi vuta bangi?anza na wasomi karibia 70%.mawaziri nawabunge karibia wote.nina uhakika hata mshua akipimwa mkojo kabangi hakakosekani
 
Mkuu usituunganishe watz wote kuwa ni wavuta bhangi wengine hatuvuti wala hatujawahi kuvuta bhangi. Pia elewa bhangi ni kati ya madawa ya kulevya ambayo yamepigwa marufuku kutumiwa Tanzania.
 
Maoni yake yenyewe ya kivuta bangi, wavuta bangi wanateteana, mwenzao aligoma kukojoa yaani sijui wamelogwa na nani hawa watu sikuhizi, wamekuwa wa kutetea na kukumbatia kila aina ya uovu kwa kweli wanaudhi sana.
 
Back
Top Bottom