Mkenya aliyekamatwa na dawa za kulevya Vietnam kunyongwa Machi 17, 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Margaret Nduta Macharia (37), raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na mwanaume kutoka Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John.

Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

Hata hivyo, Margaret akijitetea mahakamani nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku.
1742126235779.png
 
Margaret Nduta Macharia (37), raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na mwanaume kutoka Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John.

Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

Hata hivyo, Margaret akijitetea mahakamani nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku. View attachment 3272728
Tulishaambiwa kuwa tusipokee vifurushi kwa watu tusiowajua tukiwa Airport.
Pole yake
 
Mbona sura ni ya kiume hii!

Pole yake, kifo cha kujua mpaka dakika za kukata moto hakika kinauma sana.

Si kwake tu hata kwa wapendwa wake pia.
 
Margaret Nduta Macharia (37), raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na mwanaume kutoka Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John.

Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

Hata hivyo, Margaret akijitetea mahakamani nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku. View attachment 3272728
Muonekano wake kwenye hii picha ni kama amerukwa akili, hukumu ya kunyongwa sio mchezo!

Mungu ampe amani, maisha yana mengi japo alikuwa anatafuta kipato kwa njia haramu ila haiondoi ukweli kwamba alikuwa anapambania namna ya kuishi.
 
Back
Top Bottom