Mkenya aliyekamatwa na dawa za kulevya Vietnam kunyongwa Machi 17, 2025

Mkenya aliyekamatwa na dawa za kulevya Vietnam kunyongwa Machi 17, 2025

Unamuamini? Mpaka kufikia hukumu wameshamsoma amehusika na alikuwa anajua kila hatua
Nimeenda YouTube ndio nimesoma kwa urefu.
Kumbe alimpokea boss wake aliyekuwa anamfanyia kazi huko.
Akamwambia eti akifanikisha kufikisha mzigo salama, atapewa pesa.
Huenda kweli anajua.
Sijamuamini
 
Margaret Nduta Macharia (37), raia wa Kenya aliyekamatwa mwaka 2023 nchini Vietnam na dawa za kulevya kilogramu mbili za Cocaine, anatarajiwa kunyongwa hadi kufa kesho Jumatatu Machi 17, 2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, Margaret aliyepewa hukumu hiyo Machi 6, 2025 alisema alipewa mzigo huo wa dawa za kulevya na mwanaume kutoka Kenya aliyemtaja kwa jina moja la John.

Pia, taarifa hiyo inaeleza kuwa alifanikiwa kupita katika viwanja vitatu vya ndege bila kukamatwa, kabla ya kugundulika Vietnam. Viwanja hivyo ni; Jomo Kenyatta (Kenya), Bole (Ethiopia) na Hamad (Qatar).

Hata hivyo, Margaret akijitetea mahakamani nchini Vietnam alidai hakufahamu kama mzigo ule ulikuwa ni dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vietnam, Margaret atakula chakula chake cha mwisho kesho saa 1:30 usiku na kisha kunyongwa saa 2:30 za usiku. View attachment 3272728
Mwenyezimungu atujaalie kazi za halal na nyoyo zenye kutosheka Kwa tunachopata. Ni huruma sana hukumu hii 😭😭😭
 
Hii niliona jioni jioni hivi
 

Attachments

  • FB_IMG_1742135602284.jpg
    FB_IMG_1742135602284.jpg
    121.8 KB · Views: 29
Kuna vitu vya kipuuzi sana duniani, yaani Vietnam wameanza kuweka sheria zao pamoja na death penalty tokea 1985 na kufanya mabadiliko kwa kuongeza makosa mengine mwaka 1997, tunashangaa kuona watu wanapigwa death penalty?

Huu ni mwaka 2025 ukikubali kujiingiza kwenye hizi biashara lazma ukubali na consequences! Ni mtu mpumbavu pekee anaweza kujitoa mhanga kiasi hicho halafu ategemee kutoka salama, eti sijui tumuombee kwa Mungu atoke salama, yaani umekutwa na kete za Cocaine ama Heroine halafu wakusamehe kirahisi tu?! Sio Afrika huko! Huyu wamchape death penalty ili wengine wajifunze kupitia kwake.
 
Waafrika tuna vichwa vigumu kama panzi 😔 hivi nchi kama Vietnam, Saudi Arabia, Singapore, Indonesia, pamoja na Korea Kusini, unapata ujasiri upi wa kuingia na madawa ya kulevya hata kwa bahati mbaya, yaani upewe mkoba tu uingie nao kizembe, eti kilo 2?! Kuna watu wanakutwa na ½ ama ¼ ila shughuli yake sio ya kitoto.

Kwa sasa watu wanasema kuwa hakufahamu kuwa alibeba mzigo, je alivyopewa hakuona haja ya kuchungulia? Yaani nitoke JK Nyerere International Airport naenda UAE Dubai nipewe mkoba pale Goba na mtu kuwa niruke nao pipa mpaka Dubai?! Seriously?!

2022 pekee Vietnam wamewaleftisha in peace watu takribani 1000 huku wenye kesi kama ya huyu bi mdada wakiwa ni 68% ni mwendo wa kuagiza chakula pendwa, aidha makange ya mbuzi na ugali kisha lisaa limoja baadaye unatangulia mbele za haki.
 
Sasa anakula chakula cha mwisho kwa ajili ya nn?

Sidhani kama hata hamu ya kula ataipata.
Ndo principle yao! Kuna jamaa alikuwa ni mhindi walimdaka aisee aliagiza wali na kuku yaani alikuwa anatetemeka mwanzo mwisho
 
Ilibaki kidogo 2017 niingie mkenge, maisha haya sio mchezo, nilipigwa chale za kutosha na mganga nikiwa na huyo jamaa yangu alienipa deal la safari ya China Rip boss wangu sitasahau kamwe.
 
Ilibaki kidogo 2017 niingie mkenge, maisha haya sio mchezo, nilipigwa chale za kutosha na mganga nikiwa na huyo jamaa yangu alienipa deal la safari ya China Rip boss wangu sitasahau kamwe.
Hii story yako ungeifungulia Uzi kiongozi inaonesha Kuna vingi vya kujifunza
 
Ilibaki kidogo 2017 niingie mkenge, maisha haya sio mchezo, nilipigwa chale za kutosha na mganga nikiwa na huyo jamaa yangu alienipa deal la safari ya China Rip boss wangu sitasahau kamwe.
Uchawi mwisho Africa nje unadakwa tu hata uwe mganga
 
Back
Top Bottom