Mkeo ana bodaboda wake?

Mkeo ana bodaboda wake?

Honestly hata Mimi kuna dogo ametokea kuwa Boda sahihi sana kwangu, naeza mpatia pesa hata Mil 10 apeleke mahali na zinafika salama. Hata nikiwa na safari ya haraka inayohitaji Boda huwa nakuwa at peace kupanda Boda boda yake kuliko boda zingine.

Na huyu Dogo nimejuana naye kupitia kwa wife. [emoji28][emoji28]
Ndio maana muaminifu sana.

Heko kwa shemeji!
 
Shida akishalewa hawajielelewi
Kuna mmoja kastuka anaamka na bodaboda wake lodge..
Unaweza fikiri nadanganya Ila ni ukweli mtupu
Huyu inawezekana ana madhaifu yake tu baada ya pombe...... anafaa kulewa akiwa nyumbani!!!
 
Etiii??????

Umesema ATM Card....?????

Hapana aisee....


Mazoea kwenye pesa sitaki.......

Kumbe ujausoma huu Uzi wote
Wapo Hadi wadada humu wanawapa ATM card bodaboda wakawachukulie pesa..
Pitia Uzi uone
 
Sina.......


Ila baada ya kusoma huu uzi nimegundua kuna umuhimu wa kuwa na bodaboda wangu aisee

Mimi pia Jana nimechukua namba upya ila this time nahakikisha hafiki nyumbani wala hafahamu issue yangu yoyote
Yaani ni hello Njoo sehemu fulani nipeleke sehemu fulani shika pesa yako
Asante. Baaaasi
 
Mimi pia Jana nimechukua namba upya ila this time nahakikisha hafiki nyumbani wala hafahamu issue yangu yoyote
Yaani ni hello Njoo sehemu fulani nipeleke sehemu fulani shika pesa yako
Asante. Baaaasi
Bora ufanye hivyo.
Kuwe na mipaka
 
Nadhani Wanawake Hawajui Ni Nini Wanataka, Fikria Uwe Tajiri Watakusaliti Uwe Hauna Kipato Pia Utasalitiwa.. Kijana Wawatu Kutoka Ukingani Fredy Ngajiro Aka Fredy Vunjabei Kashalizwana Mobeto Hamisa, anabaki Tu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ukitaka Kuishi vizuri na kwa muda mrefu usiwafuatilie Hawa watu, ukiwa unamhitaji malizana naye kabisa kila mmoja ashike lake, hakuna mazoea, Kama yuko ndani tegemea akili zako, kwani ndio wa kwanza eti wanashauri ili wakuteke akili na pesa. Muhimu watoto wachache, wape malezi mazuri, Elimu Nzuri, wasaidie wafikie malengo yao. Tunza Pesa yako na mali yako, Kama Watoto wana akili andikisha mali kwa watoto.
 
Nilishangaa sana siku nilipomwambia mchepuko tupande daladala twende mnadani Msalato dodoma takriban KM 12 bibie kaniambia anamwita bodaboda wake tupande mshkaki hua anampeleka na kumfuata kwa elfu tatu
 
Nilishangaa sana siku nilipomwambia mchepuko tupande daladala twende mnadani Msalato dodoma takriban KM 12 bibie kaniambia anamwita bodaboda wake tupande mshkaki hua anampeleka na kumfuata kwa elfu tatu

Hahaha lazima ushangae ndo bodaboda hao
 
😂😂😂 huu uzi ulinipa sijui nikiwa wapi miye..

😀😀😀natamani bodaboda wangu auonee
 
Mkuu sababu haswa ya msingi ni hulka tu ya wamama, wadada kupenda kuwa na mtu wanayemuamini...

Kama kuna mengine zaidi ya hayo ni udhaifu tu wa kibinadamu..

Nje ya mada, hata sisi wanaume tuna barmaid wetu hao asipokuwepo bar vyombo havishuki

Au ukiwa maskani unajipata una kochi lako hilo au kiti chako hupati amani ukikaa pengine...
yaan hapo kwenye kiti nyumbani kama mm adi kikombe cha chai nisiponywea nnachokipenda sijisikii jmn
 
Sisi wenyewe wanaume tuna bodaboda ambae ukiwa na shida hata akisema yupo mbali lazima umsubiri,,,kwanza anajua mizigo yako yote na sio mropokaji,,lkn umtumie boda ni boda akifika kijiweni anatangaza yote


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
yaan hapo kwenye kiti nyumbani kama mm adi kikombe cha chai nisiponywea nnachokipenda sijisikii jmn
😂😂 Haka ka tabia ka wengi kumbe..Mimi mwenyewe nyumbani hua nakikombe changu siwezagi tumia kingine zaidi ya kile..Kuna Kochi langu Hilo hata mtu mwingine akikaa nikienda sebuleni atapisha..nikikaa sehsmu nyingine Sina Raha hata...na sahani pia 😂😂😂😂..
 
Back
Top Bottom