Oa au okewa ndo utajua raha za ndoa.Nyinyi mna ndoa za namna gani kiasi simu mnazificha ficha, mkianza hivyo tu mnamkaribisha shetani, mie mke wangu akiitaka simu yangu ruksa muda wowote, wakati wowote, nami hivyo hivyo.
Naunga mkono hoja.Ukiwa na mke au mume halafu ukawa na vijitabia vya kuficha simu au password za simu yako au account yako ya bank bado hujapata mwenza sahihi. Ukiona hivyo heri utoke nje ya uwanja upate nafasi ya kujitafuta upya
Naunga mkono hoja.
Wanandoa wanaoendeleza maisha ya uptivate ktk simu na masuala mengine bado siyo wanandoa kamili, ni WAHUNI.
NDOA NI PAMOJA NA UAMINIFU
haupo kwenye ndoa wewe labda upo kwenye DOA, acha kutupiga chai.Nyinyi mna ndoa za namna gani kiasi simu mnazificha ficha, mkianza hivyo tu mnamkaribisha shetani, mie mke wangu akiitaka simu yangu ruksa muda wowote, wakati wowote, nami hivyo hivyo.
Iko siku tu kitaonekana wala usijione mjanja na maelezo yake huenda ukawa huna na ndio mwanzo wa mwanamke kukulipizia kisasi.Wajanja tunakiachaga ofsini kwenye droo au kwenye gari yaani hkitakiwi kionekane
Sababu ya kitoto sana hii, haya ma infinix tu ukiwa na la 5000maH kama si mtumiaji internet linakwenda hata siku 3 ndio walichaji.Watu wana hizo simu kwa sababu ya kukaa na charge muda mrefu...
Uko ulimwengu gani? Maana hata smart 5 inakaa na chaji sana..utakuwa unatumia f1Utakuwa huna mitandao yote,kiswaswadu hakiishi chaji haraka na ni rahisi kutumia kuliko hizo smartphone zenu kutwa kwenye chaji kama mtoto aliyedungwa sindano maumivu yake unambembeleza kwa nyonyo.
Sababu ya kitoto sana hii, haya ma infinix tu ukiwa na la 5000maH kama si mtumiaji internet linakwenda hata siku 3 ndio walichaji.
Ni sahihi kabisaBila uwazi na uaminifu Ile maana ya ndoa inakua imekufa
Kinachokua kinaendelea hapo ni utapeli na kutumiana tuuu
Na kwanini kuishi kitapeli hivyo 🤣🤣🤣
Justification ya.kuwa na kiswaswadu inakuwa haipo kama una infinixMzee baba bei ya infinix inafanana na kiswaswadu?
Ninavyoongea nina mke mzee, sipigi porojo naongea NINAYOISHI MIMI.Oa au okewa ndo utajua raha za ndoa.
Bila visanga hakuna utamu
Siwezi kukushikia fimbo.. Hutaki kuamini ni sawa pia.haupo kwenye ndoa wewe labda upo kwenye DOA, acha kutupiga chai.
Umenena vyemaNinavyoongea nina mke mzee, sipigi porojo naongea NINAYOISHI MIMI.
Halafu hapa mada sio visanga kwenye ndoa, kukoseana si ishu, mnakoseana watu mtaani mnaolala mbalimbali itakuwa nyinyi pika pakua, kitanda kimoja, kujambiana na kadhalika humo humo,
Mada ni simu ndani ya ndoa mzee.
Kwangu mke wangu simu zetu hazina kuficha ficha, simu msipoficha ficha inafika hatua hakuna hata kutiliana wasi. Kwetu hakufuna mipaka wala mimbwa kwenye simu zetu. Aishawahi ondoka na simu yangu kwa emergency, nishawahi ondoka na simu yake na kukaa nayo zaidi ya wiki, simu yake ishaharibika mara mbili nikasafiri nayo kuitengeneza, mwezi mzima watsap yake ipo on mimi ndio namueleza fulani kakucheki, groups zake za chuo zinaujumbe gani.
Nikung'ate sikio, najua huwa anapita humu, anaweza kuiona hii, kabla ya kumuoa mke wangu, nilihack simu yake, msgz, calls nilikuwa nikivipata kwa zaidi ya miezi 6 mfululizo, nilikuja kuifuta miezi mi3 mbele baada ya kuwa tumefunga ndoa.
Kama kubadilika abadilikie mbele ya safari na akibadilika basi ajue STRAIGHT RED CARD 🔴 inamuhusu
Iko siku tu kitaonekana wala usijione mjanja na maelezo yake huenda ukawa huna na ndio mwanzo wa mwanamke kukulipizia kisasi.