Ninavyoongea nina mke mzee, sipigi porojo naongea NINAYOISHI MIMI.
Halafu hapa mada sio visanga kwenye ndoa, kukoseana si ishu, mnakoseana watu mtaani mnaolala mbalimbali itakuwa nyinyi pika pakua, kitanda kimoja, kujambiana na kadhalika humo humo,
Mada ni simu ndani ya ndoa mzee.
Kwangu mke wangu simu zetu hazina kuficha ficha, simu msipoficha ficha inafika hatua hakuna hata kutiliana wasi. Kwetu hakufuna mipaka wala mimbwa kwenye simu zetu. Aishawahi ondoka na simu yangu kwa emergency, nishawahi ondoka na simu yake na kukaa nayo zaidi ya wiki, simu yake ishaharibika mara mbili nikasafiri nayo kuitengeneza, mwezi mzima watsap yake ipo on mimi ndio namueleza fulani kakucheki, groups zake za chuo zinaujumbe gani.
Nikung'ate sikio, najua huwa anapita humu, anaweza kuiona hii, kabla ya kumuoa mke wangu, nilihack simu yake, msgz, calls nilikuwa nikivipata kwa zaidi ya miezi 6 mfululizo, nilikuja kuifuta miezi mi3 mbele baada ya kuwa tumefunga ndoa.
Kama kubadilika abadilikie mbele ya safari na akibadilika basi ajue STRAIGHT RED CARD 🔴 inamuhusu