Mkeo au mumeo akiwa na simu kubwa na kile kidogo(kiswaswadu) kaa nacho mbali usiseme sijakwambia

Nyinyi mna ndoa za namna gani kiasi simu mnazificha ficha, mkianza hivyo tu mnamkaribisha shetani, mie mke wangu akiitaka simu yangu ruksa muda wowote, wakati wowote, nami hivyo hivyo.
Oa au okewa ndo utajua raha za ndoa.
Bila visanga hakuna utamu
 
...Sjui ni nani alihalalisha huu uhuni wa kusema simu ya mkeo/mumeo haikuhusu.

Sasa nini tafsiri ya mke au mume kuwa wanandoa au mwili mmoja?

Kitendo cha kuruhusu simu ya mke au mume kuwa private issue ni kuhalilisha shetani kufanya maangamizi.
 
Ukiwa na mke au mume halafu ukawa na vijitabia vya kuficha simu au password za simu yako au account yako ya bank bado hujapata mwenza sahihi. Ukiona hivyo heri utoke nje ya uwanja upate nafasi ya kujitafuta upya
Naunga mkono hoja.

Wanandoa wanaoendeleza maisha ya uptivate ktk simu na masuala mengine bado siyo wanandoa kamili, ni WAHUNI.

NDOA NI PAMOJA NA UAMINIFU
 
Watu wana hizo simu kwa sababu ya kukaa na charge muda mrefu...
 
Naunga mkono hoja.

Wanandoa wanaoendeleza maisha ya uptivate ktk simu na masuala mengine bado siyo wanandoa kamili, ni WAHUNI.

NDOA NI PAMOJA NA UAMINIFU

Bila uwazi na uaminifu Ile maana ya ndoa inakua imekufa
Kinachokua kinaendelea hapo ni utapeli na kutumiana tuuu

Na kwanini kuishi kitapeli hivyo 🤣🤣🤣
 
Nyinyi mna ndoa za namna gani kiasi simu mnazificha ficha, mkianza hivyo tu mnamkaribisha shetani, mie mke wangu akiitaka simu yangu ruksa muda wowote, wakati wowote, nami hivyo hivyo.
haupo kwenye ndoa wewe labda upo kwenye DOA, acha kutupiga chai.
 
Utakuwa huna mitandao yote,kiswaswadu hakiishi chaji haraka na ni rahisi kutumia kuliko hizo smartphone zenu kutwa kwenye chaji kama mtoto aliyedungwa sindano maumivu yake unambembeleza kwa nyonyo.
Uko ulimwengu gani? Maana hata smart 5 inakaa na chaji sana..utakuwa unatumia f1
 
Bila uwazi na uaminifu Ile maana ya ndoa inakua imekufa
Kinachokua kinaendelea hapo ni utapeli na kutumiana tuuu

Na kwanini kuishi kitapeli hivyo 🤣🤣🤣
Ni sahihi kabisa

Wanaosema simu ya mume/mke haitakiwi kuguswa ni matapeli

Maana nguzo pekee ya ndoa ni Uaminifu.

Uaminifu kila sehemu ikiwemo ktk mawasiliano.. bila uaminifu ni WIZI TU
 
Oa au okewa ndo utajua raha za ndoa.
Bila visanga hakuna utamu
Ninavyoongea nina mke mzee, sipigi porojo naongea NINAYOISHI MIMI.

Halafu hapa mada sio visanga kwenye ndoa, kukoseana si ishu, mnakoseana watu mtaani mnaolala mbalimbali itakuwa nyinyi pika pakua, kitanda kimoja, kujambiana na kadhalika humo humo,
Mada ni simu ndani ya ndoa mzee.

Kwangu mke wangu simu zetu hazina kuficha ficha, simu msipoficha ficha inafika hatua hakuna hata kutiliana wasi. Kwetu hakufuna mipaka wala mimbwa kwenye simu zetu. Aishawahi ondoka na simu yangu kwa emergency, nishawahi ondoka na simu yake na kukaa nayo zaidi ya wiki, simu yake ishaharibika mara mbili nikasafiri nayo kuitengeneza, mwezi mzima watsap yake ipo on mimi ndio namueleza fulani kakucheki, groups zake za chuo zinaujumbe gani.

Nikung'ate sikio, najua huwa anapita humu, anaweza kuiona hii, kabla ya kumuoa mke wangu, nilihack simu yake, msgz, calls nilikuwa nikivipata kwa zaidi ya miezi 6 mfululizo, nilikuja kuifuta miezi mi3 mbele baada ya kuwa tumefunga ndoa.

Kama kubadilika abadilikie mbele ya safari na akibadilika basi ajue STRAIGHT RED CARD 🔴 inamuhusu
 
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom