.............Yah mkuu nilichoandika wala sijakosea ila sijasema hanitengei chakula mezani au hanikaribishi na hata asiponikaribisha unadhani kwenye ndoa ni kitu cha kufuatilia hiki,utafuatilia mangapi na utahoji mangapi?kama amepika vizuri chakula na umekikuta mezani kimekamilika kuna haja gani tena kuulizana mbona hujanikaribisha?na huko kuhoji hoji sana vitu vidogo vidogo ndiko mnapokuta mmezusha vurugu zisizo na kichwa wala miguu unless uniambie unatafuta sababu za kumuacha maana maisha ya ndoa ni continuous viapo ni kuishi milele na kuvumiliana.
Falsafa yangu nayoiishi ktk ndoa yangu ni “sikuowa mke aje kunitumikia” bali kuwa msaidizi wangu pamoja na kuendeleza kizazi changu,nimesema mwanzo akifanya yote hayo ila family ilipoongezeka hayo hanifanyii na nilielewa wala sijawhi kuhoji niliona tu mwenyewe siku za weekend nikiwa home hiyo battle ya watoto humo ndani hakukaliki na kama mimi kukaa na watoto nusu saa tu siwezi yeye anakaa nao kutwa nzima itakuwaje?maana hawaelekezeki kirahisi.iko hivi;nina watoto mmoja 6 aged na mwengine mwaka 1/10,muda ninaoingia home kutoka job ni saa 20:00 usiku nikifika namkuta wife amemsimamia huyu mkubwa ili ale akalale kesho aamkie shule (bahati mbaya ni mtundu mno) akiachiwa upenyo ale mwenyewe chakula utakikuta kwenye basin la vyombo vichafu hakijaguswa hata kidogo.niambie wewe kama baba,utamwambia mkeo aache kumsimamia mtoto akakuandalie maji ya kuoga?je kabla hujamuowa hukuwa unaoga wewe,aliyekuwa anakuandalia maji ni nani?
Baada ya hapo aje kwa huyu mdogo naye amuogeshe kisha aanze kumpa chakula na huyu akiwa analishwa anataka azunguke nyumba nzima hatulii sehemu moja,muda huo ndo nimeshaoga na mimi nipo dinning nataka kula na pale mezani zana zote wezeshi za mimi kuendelea zipo unataka kuniambia nisijipakulie chakula nile ila niite kwa sauti ya mamlaka “wewe mwanamke njoo unipakulie chakula”,well ataweza kutii but vipi mtoto akipaliwa chakula kule aliko umeshafikiria hasara zake?au kuniandalia nguo asubuhi,huo muda wa kufanya hivyo sasa hana tena muda huo anautumia kwa mtoto ili awahi shule yani nilichoandika pale juu ni kitu nakiishi na nimekishuhudia na mke wangu kuweka house girl hataki nilihoji akanipa sababu zake,ukweli hazikuwa na mashiko ila ikabidi nielewe kiutu uzima maana mama mwenye nyumba ameshasema ning'ang'anizane naye kwa faida gani?na naridhika na maisha tunayoishi!
Maisha ya ndoa siyo bongo movie yanataka hekima na busara ukitaka kuamini kama baba na mama yako wapo pamoja mpaka sasa chunguza je bado mama anampelekea mzee maji bafuni?zile ni longolongo tu za uchanga wa penzi wala usizizingatie sana life likishakolea mbona utajikuta upo ndani ya ndoa ila unaishi as if upo kwenye u-bachelor na ukiwa mwelewa hakuna siku utapishana hovyo kauli na mkeo.