Sir_Mimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2013
- 7,171
- 15,760
Mke hakupakulii chakula,hakuwekei maji ya kuoga,hakupasii nguo na umeamua kuchukulia simple tu.
Unafeli bro kweli kuna kipindi wake zetu wanabanwa na kazi sikatai lakini kwa hili hapana aisee..
Mimi nipo tiari nimsaidie kudek au kufua lakini sio kujipakulia chakula au kujipelekea maji bafuni et kisa watoto...ata hao watoto ipo siku watakushangaa haki! Labda ungesema siku moja moja unajisikiaga kufanya ivyo lakini Kama ni kila siku basi wewe bado ni single uliechangamka.
Ukinisoma between the lines post zangu mbili hapo juu utaelewa hata hii uliyonikot nimetoa sababu zinazosababisha haya,nikuulize mkuu....
Kwa asili ya kazi yangu inanitaka nitoke home saa 12 kasoro asubuhi usually ni muda ambao watoto ktk familia nyingi huandaliwa wawahi shule so unataka kuniambia bahati mbaya ratiba zimegongana nikae nisubiri wife amuandae mtoto kisha ndiyo aniandalie mimi nguo?hahah dude...you must be kidding,huyo mke unamlipa kiasi gani kwa mwezi mkuu?maana hapo siyo mke tena bali umeajiri na kama ndoa yako bado changa huwezi kunielewa na mimi home sina house girl na hata angekuwepo mimi kama mwanaume sioni sababu kujilegeza eti mke aniandalie nguo wakati naziona na zimefuliwa tayari (kama hakuzifua ndo nitakuwa na chakusema).
Sijui una muda gani kwenye ndoa yako ila mimi miaka 8 imenitosha kuona mengi na kujifunza mengi that's why hapo chini nikasema “kuishi na mwanamke kunakutaka utumie akili nyingi”,muhimu mke anayajua majukumu yake ndani ya nyumba na anajua ni nini cha muhimu zaidi afanye ili nyumba iwe na amani (hapa nazungumzia masuala ya unyumba) siuoni bado ulazima wa mwanaume kulalamikia vitu vidogo vidogo kama ulivyoorodhesha hapo juu.so upo tayari asubuhi kabla ya kuondoka home wewe ukamate dekio ili wife akunyooshee tu shati lako?labda kama itakuwa masharti ya mganga sawa but hivi hivi mimi hiko kitu siezi fanya!