Mkeo ni wa kundi gani kati ya haya?


Mzee kuowa haimaanishi kwamba utaanza kuishi kifalme,liweke hili akilini mwako ngoja siku uowe kisha umtake mkeo mwaka wa kwanza mpaka wa 5 akufanyie aliyokuwa akikufanyia mkiwa mwaka wa 1 uone kama hujaanza safari kwa mshenga kulalamika nyumbani hakukaliki.

Kingine...usije uka-copy maisha anayoishi mwenzako kwenye ndoa yake ukataka uyapachike kwenye ndoa yako mapema sana utavuruga mipango yako,ishi kile kitakachokupa amani.vipi kama akawa anakufanyia yote hayo ila akawa anapika chakula kibovu,watoto kulala bila kuoga au kula na nyumba kutofanyiwa usafi utajisikiaje?na haya ukimuuliza atakwambia anafanya hivyo ili kukimbizana na kasi yako.

Pia huwa sioni logical kusubiri eti utengewe maji ya kuoga na mkeo,kweli hiki ni kitu cha kusubiri?
 
Japo ni single mom,na sijamuoa,lakini naishi nae huku nchi za watu.

Namba moja inamstahiki
 
Pole Sana mkuu
 
Mke hakupakulii chakula,hakuwekei maji ya kuoga,hakupasii nguo na umeamua kuchukulia simple tu.

Unafeli bro kweli kuna kipindi wake zetu wanabanwa na kazi sikatai lakini kwa hili hapana aisee..

Mimi nipo tiari nimsaidie kudek au kufua lakini sio kujipakulia chakula au kujipelekea maji bafuni et kisa watoto...ata hao watoto ipo siku watakushangaa haki! Labda ungesema siku moja moja unajisikiaga kufanya ivyo lakini Kama ni kila siku basi wewe bado ni single uliechangamka.
 
Mkuu nahisi tunashea mke mmoja au labda ni twin wake
 
Mkuu kwani kupelekewa maji wewe umekupatia maana gani? Muda huo unaomsaidia kudeki si bora ujipelekee hayo maji?
 
We jamaa unaonekana umetokea Pwani. Me nimeishi na Mshua na Maza toka nakua naona maza lazma aamke abandike maji ya kuoga alfajiri...

Ataandaa chai asubuhi mzee akitoka kuoga anavaa nguo zishapigwa pasi siku nyingi kisha anaenda mezani for breakfast. Mie nnje nishafagia na kuosha gari na ilikuwa kama utamaduni wetu. Mshua akirudi akapaki namshushia bag lake la ofisini napeleka chumbani kwake.

Kufua maza anafua nguo sox ananiachia mimi namsaidia. Akiwepo beki 3 anawasha jiko anabandika maji ila ni agizo la bi mkubwa. Kupika cha mshua bi mkubwa anapika mwenyewe. Mshua akiwa kazini madhe anasafisha room kwao. Sometimes ananiomba namsaidia kusafisha akiwa anaumwa au amechoka.

Sasa nikija kuoa mke asiwe kama ambavyo nimekuwa nikiona mazingira ya home au akashindwa ku cope na chores zake lazma tutashindwana tu. Japo mke sio mtumwa ila nimekuzwa kuwa Dominant! Ndio utamaduni wetu ulivyo na hakuna kitu mzee alikuwa anamaindi kama kunikuta jikoni nasaidia kazi 🤣🤣🤣
 
Sio kila mtu ana heater mkuu, wengine mpaka yapangwe mafiga 🤣🤣🤣🤣
 
Mke alifundishwa kwao, ukaoa kwa taratibu zote za kimila na kidini lazima awe na tabia hz ,huyu ndio Mke hasa wa kuita Mke

Nampenda Mke wangu hizi Sifa anazo ingawa wa kisasa
 
Mwanaume akifanyiwa hivi anakabidhi hadi pumbu, limbwata liko mikononi mwetu wanawake hatujui tu, nadhani nimemrithi bi mkubwa wako
 
Mwanaume akifanyiwa hivi anakabidhi hadi pumbu, limbwata liko mikononi mwetu wanawake hatujui tu, nadhani nimemrithi bi mkubwa wako
Hahahah sasa je na ndio michepuko inapopenyea hapo, ila wanawake wengi wajinga hawaelewi hili! Mwanaume anatakiwa apewe treatment special bana. Hata diet yake ni special!

Make a man feel like a man then umemaliza kazi wewe utapendwa hadi siku yako ya mwisho. Sema unachotaka hata dunia utapewa.

Sasa unakuta mke dharau, eti anajibu kwani we hauna mikono ama? That never works on me! Sana sana ntakuzabua nionekane katili.

In Addition ndoa inakaribia ku approach 40 years. Treatment is still the same sasa ambao wanahisi kuwa treated like a man ni kuwafanya utumwa na kunaisha watoto wakizaliwa waangalie walipoteleza.
 
Mkuu kwani kupelekewa maji wewe umekupatia maana gani? Muda huo unaomsaidia kudeki si bora ujipelekee hayo maji?
Mkuu Mimi sikatai wanaume kuwasaidia wake zetu kazi lakini pale inapokua ni lazima huifanye basi tofauti yako na mkeo ni kua karibu nae tu mean hujajitenga na ubachela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…