Mkidharauliwa na ndugu huwa mnachukua hatua gani?

Morning wapendwa,

Hivi kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubiri matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau, mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha akijisikia.

Dogo anasoma chuo veta yupo likizo, iko chuo nilimtafutia mwenyewe, na kila akirudi likizo namchambulia nguo ambazo sizivai,yani ananinunia huku kakobeka nguo nilizompaga uko nyuma,na muangalia simmalizi dogo,nawaza nikipata kazi nimgawie zote zilizobaki Mimi nianze upya,bado anasoma najua anaweza akabanwa na ratiba za kununua nguo,kama mnavyojua wazazi Mara nyingi wanakupa ada na ela ya kula, lakini Leo ananidharau, na ana kazi ya kuficha vitu Mara afiche sabuni Mara sukari Mara mboga, chakula kikibaki anakubali kumpa mtu wa baki lakini anajua Mimi bado sijala, ananiharibu kisaikolojia siku nikipata kazi nikimuoneshea roho ngumu atasema kaka hanisaidii au atasemaje kutokana na izi tabia anazonioneshea saizi.

Na mda najishusha namchukulia kama dogo kama kumpa nilichonacho, lakini bado anaendelea na ratiba zake zile zile za kujinunisha, nakaaga nawaza siku Mungu akinisaidia kupata ajira au kuwa na kipato chochote kitakacho niingizia ela nije nimsaidie ata mahitaji ya shule lakini naona ananitengenezea mazingira ya kumchukia na kutotaka kumsaidia huko mbeleni kutokana na kiburi na jeuri zake.

Kuna mda napata hasira nasema akijaribu kunijibu chochote namkata vibao ,nimeamini usipokuwa na ela ata ndugu yako wa damu anakuchukia tu bila sababu,ungekuwa wewe ungefanyaje.
Tafuta Hela wewe.
 
Mithali 14:20 Masikini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri huwa na rafiki wengi.

Jibu lako lipo kwenye maandiko, mi naongezea tu tutafute hela
 
Wakati mnakula punguza matonge ama kula kidogo jazia na maji,unamtoa dogo kwenye reli [emoji851]
 
Mambo ya familia ni magumu sana...
We jikatae itajulikana mbele kwa mbele maana ajira zenyewe siku hizi hakuna tafuta plan b
 
Vyakula viko bei juu, anayewalisha akipiga hesabu asubuhi na mchana, debe la mahindi limeisha; hapo lazima aanzishe choko choko ili mpungue hapo nyumbani
 
Enjoy maisha kila siku kila mahali bila kujali opinion za wengine
 
Vitu vingine ukichukulia easy vinakuwa eazy tu, ukichukulia serious vinakuwa serious kweli kweli.

Mchukulie huyo ni pimbi tu, hana utimamu kichwani na nafsini kwake.
 
Hayo mbona ni ya kawaida sana kwenye Jamii.

Kikubwa ni kumuomba Mungu akupe subra, na pale utakapofanikiwa kamwe wala usiwaze kulipiza kisasi bali ndio iwe nafasi ya kumuonesha inavyopaswa kuwa...Mungu hutoa thawabu kwa yaliyo mema tu na sio visasi au uhasama.
Tunalipana hapahapa wengine hawawezi watajifunza kupitia yeye
 
Morning wapendwa,

Hivi kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubiri matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau, mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha akijisikia.

Dogo anasoma chuo veta yupo likizo, iko chuo nilimtafutia mwenyewe, na kila akirudi likizo namchambulia nguo ambazo sizivai,yani ananinunia huku kakobeka nguo nilizompaga uko nyuma,na muangalia simmalizi dogo,nawaza nikipata kazi nimgawie zote zilizobaki Mimi nianze upya,bado anasoma najua anaweza akabanwa na ratiba za kununua nguo,kama mnavyojua wazazi Mara nyingi wanakupa ada na ela ya kula, lakini Leo ananidharau, na ana kazi ya kuficha vitu Mara afiche sabuni Mara sukari Mara mboga, chakula kikibaki anakubali kumpa mtu wa baki lakini anajua Mimi bado sijala, ananiharibu kisaikolojia siku nikipata kazi nikimuoneshea roho ngumu atasema kaka hanisaidii au atasemaje kutokana na izi tabia anazonioneshea saizi.

Na mda najishusha namchukulia kama dogo kama kumpa nilichonacho, lakini bado anaendelea na ratiba zake zile zile za kujinunisha, nakaaga nawaza siku Mungu akinisaidia kupata ajira au kuwa na kipato chochote kitakacho niingizia ela nije nimsaidie ata mahitaji ya shule lakini naona ananitengenezea mazingira ya kumchukia na kutotaka kumsaidia huko mbeleni kutokana na kiburi na jeuri zake.

Kuna mda napata hasira nasema akijaribu kunijibu chochote namkata vibao ,nimeamini usipokuwa na ela ata ndugu yako wa damu anakuchukia tu bila sababu,ungekuwa wewe ungefanyaje.
Mkuu don't take it personal, wewe ishi maisha yako bila kujali matendo na maoni ya watu wengine, soma kitabu kimoja kinaitwa the four (4) agreements cha Don Miguel kitakusaidia pia jitahidi vitu vidogo kama sabuni uweze kujikidhi, chakula ukipata shukuru ukikosa pia shukuru ninachujua uwezi kukosa kula siku zote. Kuna stage kwenye maisha lazima upitie ili kukujenga. Pia kumbuka hakuna Hali ya kudumu kwenye maisha.
 
Back
Top Bottom