Mkidharauliwa na ndugu huwa mnachukua hatua gani?

Mambo ya familia ni magumu sana...
We jikatae itajulikana mbele kwa mbele maana ajira zenyewe siku hizi hakuna tafuta plan b
Jamaa kama anasubiria ajira za serikali aisee anapoteza muda.

Jana nimetembela ajira portal kada zote ni (0)

Aisee.
 
Tufahamu kwanza kabila lako mkuu...Nyie sio Waha kweli?..
 
Mi ndugu akinipotezea,atajuta mbona ...napotezea mazima hata kumwangalia usoni naacha kabisa yaan kabisa
 
Huyo dogo anajua kuwa hupendezwi na tabia zake?kabla ya kumuhukumu mwambie kwanza,huenda hajui maisha au hajui kama hupendi tabia zake, mwambie wazi madhara ya tabia zake na baadae utakavyorudisha matokeo yake. Kwa kawaida kisasi kinauma sana kuliko tukio halisi. Kwa hiyo asije laumu baadae.
 
Morning wapendwa,

Hivi kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubiri matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau, mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha akijisikia.

Dogo anasoma chuo veta yupo likizo, iko chuo nilimtafutia mwenyewe, na kila akirudi likizo namchambulia nguo ambazo sizivai,yani ananinunia huku kakobeka nguo nilizompaga uko nyuma, na muangalia simmalizi dogo,nawaza nikipata kazi nimgawie zote zilizobaki Mimi nianze upya

Bado anasoma najua anaweza akabanwa na ratiba za kununua nguo,kama mnavyojua wazazi Mara nyingi wanakupa ada na ela ya kula, lakini Leo ananidharau, na ana kazi ya kuficha vitu Mara afiche sabuni Mara sukari Mara mboga, chakula kikibaki anakubali kumpa mtu wa baki lakini anajua Mimi bado sijala, ananiharibu kisaikolojia siku nikipata kazi nikimuoneshea roho ngumu atasema kaka hanisaidii au atasemaje kutokana na izi tabia anazonioneshea saizi.

Na mda najishusha namchukulia kama dogo kama kumpa nilichonacho, lakini bado anaendelea na ratiba zake zile zile za kujinunisha, nakaaga nawaza siku Mungu akinisaidia kupata ajira au kuwa na kipato chochote kitakacho niingizia ela nije nimsaidie ata mahitaji ya shule lakini naona ananitengenezea mazingira ya kumchukia na kutotaka kumsaidia huko mbeleni kutokana na kiburi na jeuri zake.

Kuna mda napata hasira nasema akijaribu kunijibu chochote namkata vibao, nimeamini usipokuwa na ela ata ndugu yako wa damu anakuchukia tu bila sababu, ungekuwa wewe ungefanyaje?
Cjasoma uzi wako nimeangalia headline tu nika pata wazo .... naomba wew n wengine someni hapa ... kwanza na wasalimuni nyote na amani ya MUNGU iwe pamoja nanyi ....katika maisha jitahidi kufanya kazi yako kwa bidii sali sana .... kama kuna watu aanao rudisha maendeleo ya wenzao nyuma basi ndugu ni namba moja jitahidi kuwa bize na maisha yako huku ukimtanguliza MUNGU kwanza mara nyingi ndugu ni watu wa lawama hawa bebeki...kama wamekutenga wala usifadhaike na we jitenge fanya mambo yako tena tumia hiyo fursa kama changamoto ya kukupa ari zaidi ...mfano mimi kwenye simu yangu kuna namba za MAMA yangu mzazi basi
 
Morning wapendwa,

Hivi kwa mfano haujaanza maisha kutokana labda na kusoma upo nyumbani unasubiri matokeo yako ili uendelee kuangalia mikakati mingine ya kimaisha hapo nyumbani unaishi na ndugu na wadogo zako baada ya muda wadogo zako wanaanza kukudharau, mfano kuna dogo hapa home kaninunua mwezi wa tatu sasa bila sababu yeyote ile kuna mda anaimba nyimbo za mafumbo na kuziimbisha akijisikia.

Dogo anasoma chuo veta yupo likizo, iko chuo nilimtafutia mwenyewe, na kila akirudi likizo namchambulia nguo ambazo sizivai,yani ananinunia huku kakobeka nguo nilizompaga uko nyuma, na muangalia simmalizi dogo,nawaza nikipata kazi nimgawie zote zilizobaki Mimi nianze upya

Bado anasoma najua anaweza akabanwa na ratiba za kununua nguo,kama mnavyojua wazazi Mara nyingi wanakupa ada na ela ya kula, lakini Leo ananidharau, na ana kazi ya kuficha vitu Mara afiche sabuni Mara sukari Mara mboga, chakula kikibaki anakubali kumpa mtu wa baki lakini anajua Mimi bado sijala, ananiharibu kisaikolojia siku nikipata kazi nikimuoneshea roho ngumu atasema kaka hanisaidii au atasemaje kutokana na izi tabia anazonioneshea saizi.

Na mda najishusha namchukulia kama dogo kama kumpa nilichonacho, lakini bado anaendelea na ratiba zake zile zile za kujinunisha, nakaaga nawaza siku Mungu akinisaidia kupata ajira au kuwa na kipato chochote kitakacho niingizia ela nije nimsaidie ata mahitaji ya shule lakini naona ananitengenezea mazingira ya kumchukia na kutotaka kumsaidia huko mbeleni kutokana na kiburi na jeuri zake.

Kuna mda napata hasira nasema akijaribu kunijibu chochote namkata vibao, nimeamini usipokuwa na ela ata ndugu yako wa damu anakuchukia tu bila sababu, ungekuwa wewe ungefanyaje?
Mimi huwa sichukui hatua yeyote!
 
Mdogo wako ni mdogo kwako uwe na hela au usiwe nazo. Kiafrika heshima Iko pale pale. Hizo huruma zako zitakuponza siku hata ukifanikiwa na ukazishika pesa zako bado atasema umeazima. Mwambie ukweli hata akanuna na kuvimba na kupasuka ila ukweli wake anaujua. Hiyo ni tabia ya kishubamiti kabisa. Pia usilipize hiyo mwachie Mungu ndo anaweza. We jitulilie tafuta kazi yako, Iko mradi unapokaa hujaambiwa Toka au nenda tulia zako.
 
Jitahidi utafute mishe ingawa pia dharau hazitoisha. Ila swala ni MUDA tu. Binafsi niliwahi kudharauliwa sana na watoto wa ndugu kuna mmoja aliniambia akifika unri wangu atakuwa mbali sana. Nilikuwa naumia ila MUDA umeongea. Naamini wote kwa hali walizonazo sasa ukilinganisha na mimi MUDA umewapa jibu na hawataki hata tuonane hovxo hovyo sasa hivi😀😀 Vumilia tu
 
Kwa maana iyo ww umeshindwa kuongea nae haya uliotuandikia hapa?
 
Nimeongea nae bado anaendelea kununa nikanwambia sijakufanyia chochote unaninunia bila sababu basi endelea tuone faida zake.
 
Back
Top Bottom