Mkidharauliwa na ndugu huwa mnachukua hatua gani?

Tafuta Hela wewe.
 
Mithali 14:20 Masikini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri huwa na rafiki wengi.

Jibu lako lipo kwenye maandiko, mi naongezea tu tutafute hela
 
Wakati mnakula punguza matonge ama kula kidogo jazia na maji,unamtoa dogo kwenye reli [emoji851]
 
Mambo ya familia ni magumu sana...
We jikatae itajulikana mbele kwa mbele maana ajira zenyewe siku hizi hakuna tafuta plan b
 
Vyakula viko bei juu, anayewalisha akipiga hesabu asubuhi na mchana, debe la mahindi limeisha; hapo lazima aanzishe choko choko ili mpungue hapo nyumbani
 
Enjoy maisha kila siku kila mahali bila kujali opinion za wengine
 
Vitu vingine ukichukulia easy vinakuwa eazy tu, ukichukulia serious vinakuwa serious kweli kweli.

Mchukulie huyo ni pimbi tu, hana utimamu kichwani na nafsini kwake.
 
Tunalipana hapahapa wengine hawawezi watajifunza kupitia yeye
 
Mkuu don't take it personal, wewe ishi maisha yako bila kujali matendo na maoni ya watu wengine, soma kitabu kimoja kinaitwa the four (4) agreements cha Don Miguel kitakusaidia pia jitahidi vitu vidogo kama sabuni uweze kujikidhi, chakula ukipata shukuru ukikosa pia shukuru ninachujua uwezi kukosa kula siku zote. Kuna stage kwenye maisha lazima upitie ili kukujenga. Pia kumbuka hakuna Hali ya kudumu kwenye maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…