Mkidharauliwa na ndugu huwa mnachukua hatua gani?

Mambo ya familia ni magumu sana...
We jikatae itajulikana mbele kwa mbele maana ajira zenyewe siku hizi hakuna tafuta plan b
Jamaa kama anasubiria ajira za serikali aisee anapoteza muda.

Jana nimetembela ajira portal kada zote ni (0)

Aisee.
 
Tufahamu kwanza kabila lako mkuu...Nyie sio Waha kweli?..
 
Mi ndugu akinipotezea,atajuta mbona ...napotezea mazima hata kumwangalia usoni naacha kabisa yaan kabisa
 
Huyo dogo anajua kuwa hupendezwi na tabia zake?kabla ya kumuhukumu mwambie kwanza,huenda hajui maisha au hajui kama hupendi tabia zake, mwambie wazi madhara ya tabia zake na baadae utakavyorudisha matokeo yake. Kwa kawaida kisasi kinauma sana kuliko tukio halisi. Kwa hiyo asije laumu baadae.
 
Cjasoma uzi wako nimeangalia headline tu nika pata wazo .... naomba wew n wengine someni hapa ... kwanza na wasalimuni nyote na amani ya MUNGU iwe pamoja nanyi ....katika maisha jitahidi kufanya kazi yako kwa bidii sali sana .... kama kuna watu aanao rudisha maendeleo ya wenzao nyuma basi ndugu ni namba moja jitahidi kuwa bize na maisha yako huku ukimtanguliza MUNGU kwanza mara nyingi ndugu ni watu wa lawama hawa bebeki...kama wamekutenga wala usifadhaike na we jitenge fanya mambo yako tena tumia hiyo fursa kama changamoto ya kukupa ari zaidi ...mfano mimi kwenye simu yangu kuna namba za MAMA yangu mzazi basi
 
Mimi huwa sichukui hatua yeyote!
 
Mdogo wako ni mdogo kwako uwe na hela au usiwe nazo. Kiafrika heshima Iko pale pale. Hizo huruma zako zitakuponza siku hata ukifanikiwa na ukazishika pesa zako bado atasema umeazima. Mwambie ukweli hata akanuna na kuvimba na kupasuka ila ukweli wake anaujua. Hiyo ni tabia ya kishubamiti kabisa. Pia usilipize hiyo mwachie Mungu ndo anaweza. We jitulilie tafuta kazi yako, Iko mradi unapokaa hujaambiwa Toka au nenda tulia zako.
 
Jitahidi utafute mishe ingawa pia dharau hazitoisha. Ila swala ni MUDA tu. Binafsi niliwahi kudharauliwa sana na watoto wa ndugu kuna mmoja aliniambia akifika unri wangu atakuwa mbali sana. Nilikuwa naumia ila MUDA umeongea. Naamini wote kwa hali walizonazo sasa ukilinganisha na mimi MUDA umewapa jibu na hawataki hata tuonane hovxo hovyo sasa hivi😀😀 Vumilia tu
 
Kwa maana iyo ww umeshindwa kuongea nae haya uliotuandikia hapa?
 
Kwa maana iyo ww umeshindwa kuongea nae haya uliotuandikia hapa?
Nimeongea nae bado anaendelea kununa nikanwambia sijakufanyia chochote unaninunia bila sababu basi endelea tuone faida zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…