"Mkiwa na ugomvi wa mali muachie ukaanze upya"

Sasa kipi bora? Kwenda kutumikia kifungo maisha yake yote ni nafuu kuliko kuishi uraiani ukiwa huru lakini huna mali? I bet jamaa baada ya mwezi mmoja atakuwa anajilaumu sana. Hizi hasira hizi.... BTW kuna njia nyingine nyingi tu angeweza kutumia badala ya kumpiga risasi (na hapa tunajadili kama mwanamke ndiye mwenye makosa. Unaweza kukuta ukimbiwa kisa cha mwanamke kutaka kuandika jina lake unaweza kusema huyo jamaa ni zaidi ya shetani)
 
Mimi naomba kuuliza tu yule manzi ni kabila gani...!!?

Mana nisije ropoka apa nikaonekana naleta ukabila, mana ile ilikuwa "game of chance"
 
Hivi kwani ndoa ni lazima?
Mwache aende zake , wanawake wapo wengine wengi tu.
Kitendo cha kuua mwanamke sababu ya wivu sijuwi usaliti ni upuuzi wa hali ya juu.
 
Talaka ndy suluhusho, baadae mnakwenda mahakamani mali zigaiwe.
Hapo ni wivu wa mapenzi ndy chanzo cha yote wala sio nyymba wala mali.
 
Kwahyo ulitaka mwanamke aache nyumba yake?
Hapo inaonyesha mwanaume ni marioo,,
Na aliandikishwa nyumba wakati penzi bado jipya,, baadae ya penzi kuisha akataka kutolewa kwenye mali ndy tatizo lilipoanzia..
Hapo mwanaume ndy fala
Tunavyosikia.
Ni kuwa Mwanaume uchumi uliyumba.
Na akagundua kuna usaliti.
Na mwanamke akadai talaka.
 
Siwezi muachia mali yangu mwanamke mwenye tamaa,tofauti na kugawana hapo lazima nimpeleke ahera,Tena bila kuacha alama yoyote ile
Haya maneno unayoongea now sababu bado hujatenda tukio.
Baada ya kutenda tukio utatamani umwachie mali zote na uwe huru..
 
Kwahyo ulitaka mwanamke aache nyumba yake?
Hapo inaonyesha mwanaume ni marioo,,
Na aliandikishwa nyumba wakati penzi bado jipya,, baadae ya penzi kuisha akataka kutolewa kwenye mali ndy tatizo lilipoanzia..
Hapo mwanaume ndy fala
Mkuu tupate na ukweli wa upande wa muuaji pengine chanzo cha kifo ni marehemu mwenyewe wanawake we wasikie tu ni vile hawajakubadilikia hapo ulipo yahitaji hekima sana kuish na hao viumbe
 
Jamii yetu inakataa uhalisia inayoishi..

Kwamba unatafuta huku unajijengea picha za baadaye unataka uone watoto wako wakishika usukani wa kile ulichopigania kwenye ujana wako,, then mjinga mmoja kwa kushikiwa akili anazima maono...

Tuendelee kuchambua matukio ila si rahisi kihivyo...
 
Siwezi,kama wewe ni Ke njoo ujichanganye kwangu uone, nakumaliza bila kuacha alama,elewa neno bila kuacha alama
Hizo ni kauli kabla ya kutenda tukio..
Pia inaonyesha udhaifu wako ulipo.
Mwache aende zake fanya maisha yko.
 

Tuendelee na uchambuzi kwakuwa kuchambua matukio huwa ni rahisi sana,, iloa tutambue binadamu tuko tofauti kwenye uvumilivu wa vitu..
Ndo maana hata hao wanaoshauri watu nao wanashangaza watu kufanya yale yale wanaoshauri wenzao..
 
Wote mnaongea kwa kutumia hisia. Au huwa hamjui maana ya hisia, hata kuongea kwa hasira pia ni hisia.

Fair game ni kugawana, ila hakuna kitu kigumu kama kugawa mali isiyohamishika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…