Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Hata Kondoa Irangi atakaa.
 
Mawazo mfuu kuna watu wanaishi huko DODOMA na life lao ni nzuri wana mafanikio kukuzidi, wewe endelea kusifia mafanikio ya wanaume wengine hapo mjini
 
Sehemu ambayo niwahi kufika na kuona taabu kuishi ni Kasulu na Kibondo. Ilikuwa wakati wa mvua. Palikuwa pagumu sana kwangu.

Kasulu chakula kipo cha kutosha, bei chee...Sema mazingira yake mtihani sana, hasa kipindi cha mvua na ule udongo mwekundu ni mwendo kuteleza tu, gari linageuka lilikotoka bila hiyari, hakuna mzunguko mkubwa wa pesa. Uliokutana nao mtaa X ndio utakaokutana nao mtaa Y.
 
Wee acha tu. Huo udongo mwekundu huo... Wakati wa mvua ni bonge la tope lenye kunata. Linanatia kwenye sole ya viatu kama ulimbo. Kila ukitembea hatua 10 hivi, viatu vinakuwa kama tofali. Wakati wa kiangazi ni vumbi. Kwa kweli kuna sehemu ili uishi, inabidi uwe umezaliwa huko tu. Chakula kiko kila sehemu. Hakuna sehemu isiyokuwa na chakula. Mahitaji ya mwanadamu ni zaidi ya chakula.
 
Mkoa wowote nje ya Dsm hapana kwakweli, yaan kitakachonitoa Dsm ni njaa na fursa ila mchongo ukiisha au nikishiba kidogo narudi kwa base yangu uptown Dsm.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] vijana wa kigogo wakishavuna Ubuyu wanahamia kwenye uzinzi
Huwa naona wivu nikipita dom na ruaha mbuyuni.Yani unatafuta ngazi, unapanda juu ya mbuyu inaangusha mabuyu,unapasua kisha unapeleka sokoni.
Wakati sehemu zingine wanalima ardhi, wananunua mbegu, wananunua mbolea, wanapalilia, bado mvua inazingua na wanaweza wasivune mazao yao ya msimu.
 
Ambao mnalishwa na kula bure, lazima mchague pakuishi. Na ambao mna akili fupi lazima mchague pakuish maana hamuwez kufikirisha ubongo...
 
Wenye akili nzuri huwa wanakimbia sehemu ambazo wanajua zinarudisha maendeleo yao nyuma. Tuachane na mambo ya Tanzania. Kuna watu nimesoma nao kwa sasa wako USA, UK, Australia... wanaishi maisha ya dunia ya kwanza, siyo Sumbawanga. Hata ufanye nini huko Sumbawanga, hauwezi kuwafikia. Usifikiri eti wewe una akili kwa vile unakaa Kibondo.
Ambao mnalishwa na kula bure, lazima mchague pakuishi. Na ambao mna akili fupi lazima mchague pakuish maana hamuwez kufikirisha ubongo...
 
😂 Umesoma nao... Stupid mindset... sorry for nothing Mr idiot
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…