Wewe ni mwongo sana.Hapo vip!!
Katika pitapita zangu nilishuhudia machinga wakitaka kumchomea moto mfanyabiashara mmoja pale Ngulelo stand.
Na ugomvi ulianza baada ya mfanya biashara yule kuwambia waondoe mabanda mbele ya duka lake kwasababu anashindwa kufanya biashara.
Hao machinga walimvamia jamaa kama pilipili na kuuza kurusha matusi makubwa kwa yule mfanyabiashara..na ingekuwa sio polisi walikuwa wanataka kuchoma duka la yule mfanyabiashara.
Hili swala la kudhagaa kwa machinga tulisichukulie mzaha kabisa kwasababu wafanyabiashara wanaolipa kodi ya serikali wanapata wakati mgumu sana...kiasi kwamba wengine wanaamua kufunga biashara kwa mazingira hayo.
Nina imani tokea machinga waanze kuzagaa zagaa kunawafanyabiashara wengi wafunga biashara zao kwasababu ya tatizo hili na serikali ikapoteza mapato au kodi ambayo ingetumiwa na serikali kughara elimu,afya za hao watoto wamachinga.
Ki ukweli ule ugomvi wakuta kumshambulia yule mfanyabiashara wa ngulelo ulinigusa sana..haikuwa haki hata kidogo.
Nimeona niandike hili kwasababu serikali ipo kama inaogopa kuchukua hatua katika hili swala..pasipo kupepesa macho machinga ni tatizo.
Kwa ngulelo stendi hakuna maduka wala hakuna wamachinga walioweka biashara zao mbele ya maduka ya watu.Ngulelo gani wewe unayoisemea?