Afisa Tabibu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2021
- 511
- 848
Mkoa wa Arusha unasifika pale mjini, lakini wilaya zake ni masikini mno, Ukisikia Arusha wala usitishike kabisa, shangai mkoa huu kuwa chini kwa kipato cha watu wake wakazidiwa hadi na Ruvuma.
Wilaya zilizopo mkoa wa Arusha zina hali mbaya, Wilaya kama ya Ngorongoro ambapo wakazi wake wakuu ni kabila dogo la Wasonjo makao makuu panaitwa Loliondo, huko kuna hali mbaya, hakuna barabara ya lami, hakuna umeme gridi ya Taifa, maji ni shida, watu wake hawana Elimu na ni maskini, mimba za utotoni zimejaa huko.
Wilaya zingine kama Monduli, Longido, Meru hakuna chochote cha maana, watu wa kule wengi ni wafugaji lakin bado wanaamini katika sifa za kuwa na mifugo mingi na sio kufanya maendeleo.
Ukitoa pale Arusha mjini na kidogo Karatu, wilaya nyingine hizo hali sio shwari kabisa.