Mkoa wa Arusha unasifika pale mjini, lakini wilaya zake ni maskini mno, Ukisikia Arusha wala usitishike kabisa, shangai mkoa huu kuwa chini kwa kipato cha watu wake wakazidiwa hadi na Ruvuma.
Wilaya zilizopo mkoa wa Arusha zina hali mbaya, Wilaya kama ya Ngorongoro ambapo wakazi wake wakuu ni kabila dogo la Wasonjo makao makuu panaitwa Loliondo, huko kuna hali mbaya, hakuna barabara ya lami, hakuna umeme gridi ya Taifa, maji ni shida, watu wake hawana Elimu na ni maskini, mimba za utotoni zimejaa huko.
Wilaya zingine kama Monduli, Longido, Meru hakuna chochote cha maana, watu wa kule wengi ni wafugaji lakin bado wanaamini katika sifa za kuwa na mifugo mingi na sio kufanya maendeleo.
Ukitoa pale Arusha mjini na kidogo Karatu, wilaya nyingine hizo hali sio shwari kabisa.
Afisa tabibu;
Ngoja nikufungue macho kiranga;
1. Wasonjo ni kabila dogo mno linaloishi vijiji vichache mno huko Loliondo.
Kwa uchache wao huwezi kuifanya Ngorongoro yote kuwa maskini.
Wasonjo ni kweli wako nyuma mno, si ajabu kumkuta binti mbichi wa 15-20 miaka akitembea kifua wazi yaani matiti nje na amefunika tako na uke pekee...hiyo ni mila zao na wanafurahia kuwa hivyo.
2. Pili kabila lingine kubwa Ngorongoro ni wamaasai...hawa sifa zake zinajulikana duniani kote.
Masai sio maskini isipokuwa life style yao ndivyo ilivyo...mwenye ng'ombe zaidi ya 1,000 huwezi kumlinganisha na mkwere mlima mihogo Pwani.
3. Karatu watu sio duni, hao ni wakulima wakubwa sana tu...japo fukara nao wapo.
4. Monduli..hii pia ni Wilaya ya wafugaji walewale sawa na Ngorongoro.
5. Meru.
Wakazi wake ni wa Meru, asili yao inalandana na Wachaga hasa Wamachame, hili kabila ni wapambani sana.Ni miongoni mwa makabila yanayojali sana makazi bora mno.Kijana wa kimeru hawezi kuoa bila kujenga nyumba yake ya kisasa.Meru ndilo eneo la ukanda wa kijani...mazingira bora kabisa kuishi.
Pitia...Tengeru, Usa river hadi Kikatiti wakazi wake sio haba kabisa..isipokuwa ukanda wa chini ya usariver na chini ya kikatiti ukitokea mlimani, huko kuna ukame na ndiko makabila duni toka mikoa ya Dodoma, Singida na kwingineko huishi.
Nb: nimetembea nchi nzima...wilaya kwa wilaya...Arusha ni bora sana Kilimanjaro kuliko mikoa mingi hali ni tete.
Tunayaangalia mambo kwa wastani na sio kwa kijiji kimoja au kata.