Mkoa wa Kagera ni Mkoa masikini zaidi nchini Tanzania; tutaugeuza kituo cha biashara EAC

Nikisoma hicho kichwa cha habari nikionacho ni kwamba umeamua kuushambulia mkoa wa Kagera. Au umeamua kutupa taarifa kuwa ni mkoa masikini.
Nilitaraji ungejiuliza na kuja na mapendekezo ambayo ni tangible ya namna nzuri ya kutoka pale walipo, kinyume chake umekuja na cheap observations na propaganda za siasa za 'nipeni mimi muone'.
Kuna jamaa humu anaitwa Zitto nikisoma unayoandika na misimamo yako nabaki najiuliza, je ni coincidence tu kujiita vile au alijiita ili kufuata nyayo zako, maana nikiangalia namuona jamaa yaani zitto junior yupo mbali sana kiuchambuzi na maono kukuliko
 
Unataka kuwatapeli watu wa Kagera kama kawaida yako
 
Kwan Tanzania si ni nchi maskini wa kutupwa....kwa hiyo wasomi wa Tanzania wote ni maskini...
So wasomi wa Tanzania ni maskini.....
Umaskini una ngazi zake
Ngazi mtu mmoja mmoja Mpk Kitaifa
Tanzania Msomi ndo mtu wa ovyo na hatari sana
Kwa jamii ni Bora tu afe maskini na Elimu yake.
 
Hapo kwenye no 3 hapo waache ubaguzi wa kijinga na ujuaji....
Misifa mingi afu Maskini
 
Kama huna akili ya kufikiria usiwe unanijibu, Uwekezaji wa Serikali ndio umefanya Dar iwe inaongoza hizo pesa.
Fanyeni kazi na mtumie akili kujikwamua.....sera ya kutetea wanyonge ya baba yenu haikuwahi kuwa na manufaa ulimwenguni kote toka Soviet,Ujamaa mpaka Mwendazake. Zaidi inalea madikteta.


Zalisheni na muwe wabunifu. Serikali ya mkoloni iliifuata Dar na sio Dar kufuata serikali.
 
Zitto, tatizo la Kagera ni wana Kagera wenyewe; wavivu wakubwa, watu wa majungu, watu wa maneno matupu, watu wa majivuno na ujuaji.

Wakajifunze kwa watu wa Moshi jinsi wasivyosubiri serikali katika mambo ya maendeleo. Serikali zetu zipo nyuma ya wananchi siku zote na sio sawa kusubiri serikali kuleta maendeleo, endeleeni serikali itawakuta njiani.
 
Nimesoma kwa makini sana andiko la Mh.Zitto kuhusu mkoa wa Kagera. Nashukuru kwa kuweza kutukumbusha na kutujurisha kua mkoa wa Kagera ndiyo mkoa maskini kuliko yote Tanzania. Ingawa kama mwanasiasa na mtaalam wa uchumi ilibidi utusaidie tujue kua mkoa huo ni maskini kwa dhana na hoja zipi?
Je,mkoa wa Kagera ni maskini wa kipato cha mkoa au mtu na mtu?
Je, mkoa wa Kagera ni mkoa maskini kwa kukosa huduma muhimu kama makazi,shule na elimu,usafiri ,nishati na mlo/chakula?
Je,mkoa wa Kagera ni maskini kwakua unachangia pato kidogo kwenye pato la Taifa?
Je,mkoa wa Kagera ni maskini kwakua wakazi wake wanaishi maisha duni?
Je,tumeringanisha mkoa wa Kagera na mikoa mingine kwa kuangalia ata idadi ya watu?
Ungeweza kutuweka sawa katika ili nadhani tungepata sehemu ya kuanzia kujibu pamoja na kutafuta suluhu.
 
Hakuna mwanadamu asie jivuna,asiejua na asiekua na majungu. Labda awe amekufa.....
 
Inasikitisha sana kina Bojo wanashika mkia kwa umasikini wakati huku dar wanaendesha ma-range na wanakaa prime areas!
 
Kagera kuwa mkoa maskini kuliko mikoa mingine ni kwasababu Kagera ndio lango la shirki Tanzania nguvu za giza zote zinaanziaga mkoa huo na kwenda kuchakatwa kigoma kisha biashara inakwenda kufanyika Dar es salaam na kwasasa Dodoma.
 
Ni maskini kwa kuwa unachangia pato dogo la taifa kulinganisha na population yake....

Hayo mengine sijui huduma za kijamii nk kagera iko vzr tu...
Huoni anajichanganya kusema mkoa una huduma duni za elimu na wakati huo huo unatoa wasomi wengi...sasa hao wasomi walisomea migombani au vip.....kama sio ukichaa ni nini kuelewa hiv
 
Tuanze na Kijiji ulichotoka kina hali gani kwanza kabla ya hzo maneno zingine.
 
Safi sanaaa mkuuu noted
 
Vigezo vya umasikini sijui huwa vinaangalia vitu gani. Mimi naona watu wa Kagera wana unafuu wa maisha kuliko Morogoro
 
Mkoa ambao unaongoza kwa kuwa na wasomi wengi inakuwaje elimu iwe changamoto kwake ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…